1Mwimbieni Bwana wimbo mpya; mwimbieni Bwana dunia yote. 2Mwimbieni Bwana, lisifuni jina lake; tangazeni wokovu wake siku baada ya siku. 3Tangazeni utukufu wake katikati ya mataifa, matendo yake ya ajabu miongoni mwa mataifa yote. 4Kwa kuwa Bwana ni mkuu mwenye kustahili kusifiwa kuliko wote; yeye ni wa kuogopwa kuliko miungu yote. 5Kwa maana miungu yote ya mataifa ni sanamu, lakini Bwana aliziumba mbingu. 6Fahari na enzi viko mbele yake; nguvu na utukufu vimo patakatifu pake. 7Mpeni Bwana, enyi jamaa za mataifa, mpeni Bwana utukufu na nguvu. 8Mpeni Bwana utukufu unaostahili jina lake; leteni sadaka na mje katika nyua zake. 9Mwabuduni Bwana katika uzuri wa utakatifu wake; dunia yote na itetemeke mbele zake. 10Katikati ya mataifa semeni, “Bwana anatawala.” Ulimwengu ameuweka imara, hauwezi kusogezwa; atawahukumu watu kwa uadilifu. 11Mbingu na zishangilie, nchi na ifurahi; bahari na ivume, na vyote vilivyomo ndani yake; 12mashamba na yashangilie, pamoja na vyote vilivyomo ndani yake. Kisha miti yote ya msituni itaimba kwa furaha; 13itaimba mbele za Bwana kwa maana anakuja, anakuja kuihukumu dunia. Ataihukumu dunia kwa haki, na mataifa katika kweli yake.
1Sing to Yahweh a new song! Sing to Yahweh, all the earth. 2Sing to Yahweh! Bless his name! Proclaim his salvation from day to day! 3Declare his glory among the nations, his marvelous works among all the peoples. 4For great is Yahweh, and greatly to be praised! He is to be feared above all gods. 5For all the gods of the peoples are idols, but Yahweh made the heavens. 6Honor and majesty are before him. Strength and beauty are in his sanctuary. 7Ascribe to Yahweh, you families of nations, ascribe to Yahweh glory and strength. 8Ascribe to Yahweh the glory due to his name. Bring an offering, and come into his courts. 9Worship Yahweh in holy array. Tremble before him, all the earth. 10Say among the nations, “Yahweh reigns.” The world is also established. It can’t be moved. He will judge the peoples with equity. 11Let the heavens be glad, and let the earth rejoice. Let the sea roar, and its fullness! 12Let the field and all that is in it exult! Then all the trees of the woods shall sing for joy 13before Yahweh; for he comes, for he comes to judge the earth. He will judge the world with righteousness, the peoples with his truth.
1Zingt den HEERE een nieuw lied; zingt de HEERE, gij ganse aarde! 2Zingt den HEERE, looft Zijn Naam; boodschapt Zijn heil van dag tot dag. 3Vertelt onder de heidenen Zijn eer, onder alle volken Zijn wonderen. 4Want de HEERE is groot, en zeer te prijzen; Hij is vreselijk boven alle goden. 5Want al de goden der volken zijn afgoden; maar de HEERE heeft de hemelen gemaakt. 6Majesteit en heerlijkheid zijn voor Zijn aangezicht, sterkte en sieraad in Zijn heiligdom. 7Geeft den HEERE, gij geslachten der volken! geeft den HEERE eer en sterkte. 8Geeft den HEERE de eer Zijns Naams; brengt offer, en komt in Zijn voorhoven. 9Aanbidt den HEERE in de heerlijkheid des heiligdoms; schrikt voor Zijn aangezicht, gij ganse aarde. 10Zegt onder de heidenen: De HEERE regeert; ook zal de wereld bevestigd worden, zij zal niet bewogen worden; Hij zal de volken richten in alle rechtmatigheid. 11Dat de hemelen zich verblijden, en de aarde zich verheuge, dat de zee bruise met haar volheid. 12Dat het veld huppele van vreugde met al wat er in is, dat dan al de bomen des wouds juichen. 13Voor het aangezicht des HEEREN; want Hij komt, want Hij komt, om de aarde te richten; Hij zal de wereld richten met gerechtigheid, en de volken met Zijn waarheid.
Bonyeza Enter ili kuuwekea mstari huu rangi, kuandika maelezo au kuunakili. Vitufe vya mishale vinakupeleka kwenye mstari unaofuata.
Namba za mistari hufuata tafsiri uliyochagua, na katika sura chache zinaweza kutofautiana kwa mstari mmoja.