1Ninampenda Bwana kwa maana amesikia sauti yangu; amesikia kilio changu ili anihurumie. 2Kwa sababu amenitegea sikio lake, nitamwita siku zote za maisha yangu. 3Kamba za mauti zilinizunguka, maumivu makuu ya kuzimu yalinipata, nikalemewa na taabu na huzuni. 4Ndipo nikaliitia jina la Bwana: “Ee Bwana, niokoe!” 5Bwana ni mwenye neema na haki, Mungu wetu ni mwingi wa huruma. 6Bwana huwalinda wanyenyekevu, nilipokuwa katika shida kubwa, aliniokoa. 7Ee nafsi yangu, tulia tena, kwa kuwa Bwana amekuwa mwema kwako. 8Kwa kuwa wewe, Ee Bwana, umeniokoa nafsi yangu na mauti, macho yangu kutokana na machozi, miguu yangu kutokana na kujikwaa, 9ili niweze kutembea mbele za Bwana, katika nchi ya walio hai. 10Niliamini, kwa hiyo nilisema, “Mimi nimeteseka sana.” 11Katika taabu yangu nilisema, “Wanadamu wote ni waongo.” 12Nimrudishie Bwana nini kwa wema wake wote alionitendea? 13Nitakiinua kikombe cha wokovu na kulitangaza jina la Bwana. 14Nitazitimiza nadhiri zangu kwa Bwana mbele za watu wake wote. 15Kifo cha watakatifu kina thamani machoni pa Bwana. 16Ee Bwana, hakika mimi ni mtumishi wako, mimi ni mtumishi wako, mwana wa mjakazi wako; umeniweka huru toka katika minyororo yangu. 17Nitakutolea dhabihu ya kukushukuru na kuliita jina la Bwana. 18Nitazitimiza nadhiri zangu kwa Bwana mbele za watu wake wote, 19katika nyua za nyumba ya Bwana, katikati yako, ee Yerusalemu. Msifuni Bwana.
1I love Yahweh, because he listens to my voice, and my cries for mercy. 2Because he has turned his ear to me, therefore I will call on him as long as I live. 3The cords of death surrounded me, the pains of Sheol got a hold of me. I found trouble and sorrow. 4Then I called on Yahweh’s name: “Yahweh, I beg you, deliver my soul.” 5Yahweh is Gracious and righteous. Yes, our God is merciful. 6Yahweh preserves the simple. I was brought low, and he saved me. 7Return to your rest, my soul, for Yahweh has dealt bountifully with you. 8For you have delivered my soul from death, my eyes from tears, and my feet from falling. 9I will walk before Yahweh in the land of the living. 10I believed, therefore I said, “I was greatly afflicted.” 11I said in my haste, “All men are liars.” 12What will I give to Yahweh for all his benefits toward me? 13I will take the cup of salvation, and call on Yahweh’s name. 14I will pay my vows to Yahweh, yes, in the presence of all his people. 15Precious in the sight of Yahweh is the death of his saints. 16Yahweh, truly I am your servant. I am your servant, the son of your handmaid. You have freed me from my chains. 17I will offer to you the sacrifice of thanksgiving, and will call on Yahweh’s name. 18I will pay my vows to Yahweh, yes, in the presence of all his people, 19in the courts of Yahweh’s house, in your midst, Jerusalem. Praise Yah!
1Ik heb lief, want de HEERE hoort mijn stem, mijn smekingen; 2Want Hij neigt Zijn oor tot mij; dies zal ik Hem in mijn dagen aanroepen. 3De banden des doods hadden mij omvangen, en de angsten der hel hadden mij getroffen; ik vond benauwdheid en droefenis. 4Maar ik riep den Naam des HEEREN aan, zeggende: Och HEERE! bevrijd mijn ziel. 5De HEERE is genadig en rechtvaardig, en onze God is ontfermende. 6De HEERE bewaart de eenvoudigen; ik was uitgeteerd, doch Hij heeft mij verlost. 7Mijn ziel! keer weder tot uw rust, want de HEERE heeft aan u welgedaan. 8Want Gij, HEERE! hebt mijn ziel gered van de dood, mijn ogen van tranen, mijn voet van aanstoot. 9Ik zal wandelen voor het aangezicht des HEEREN, in de landen der levenden. 10Ik heb geloofd, daarom sprak ik; ik ben zeer bedrukt geweest. 11Ik zeide in mijn haasten: Alle mensen zijn leugenaars. 12Wat zal ik den HEERE vergelden voor al Zijn weldaden aan mij bewezen? 13Ik zal den beker der verlossingen opnemen, en den Naam des HEEREN aanroepen. 14Mijn geloften zal ik den HEERE betalen, nu, in de tegenwoordigheid van al Zijn volk. 15Kostelijk is in de ogen des HEEREN de dood Zijner gunstgenoten. 16Och, HEERE! zekerlijk ik ben Uw knecht, ik ben Uw knecht, een zoon Uwer dienstmaagd; Gij hebt mijn banden losgemaakt. 17Ik zal U offeren, offerande van dankzegging, en den Naam des HEEREN aanroepen. 18Mijn geloften zal ik den HEERE betalen, nu, in de tegenwoordigheid van al Zijn volk. 19In de voorhoven van het huis des HEEREN, in het midden van u, o Jeruzalem! Hallelujah!
Bonyeza Enter ili kuuwekea mstari huu rangi, kuandika maelezo au kuunakili. Vitufe vya mishale vinakupeleka kwenye mstari unaofuata.
Namba za mistari hufuata tafsiri uliyochagua, na katika sura chache zinaweza kutofautiana kwa mstari mmoja.