Ruka hadi kwenye maudhui
Beta

Uzi bado haujatafsiriwa kikamilifu kwa Kiswahili. Kile ambacho bado hakijatafsiriwa kinaonyeshwa kwa Kiingereza.

Zaburi 148

Sura hii ni sehemu ya: Boek V

1Msifuni Bwana. Msifuni Bwana kutoka mbinguni, msifuni juu vileleni. 2Msifuni, enyi malaika wake wote, msifuni yeye, enyi jeshi lake lote la mbinguni. 3Msifuni yeye, enyi jua na mwezi, msifuni yeye, enyi nyota zote zingʼaazo. 4Msifuni yeye, enyi mbingu zilizo juu sana, na ninyi maji juu ya anga. 5Vilisifu jina la Bwana kwa maana aliamuru navyo vikaumbwa. 6Aliviweka mahali pake milele na milele, alitoa amri ambayo haibadiliki milele. 7Mtukuzeni Bwana kutoka duniani, ninyi viumbe vikubwa vya baharini na vilindi vyote vya bahari, 8umeme wa radi na mvua ya mawe, theluji na mawingu, pepo za dhoruba zinazofanya amri zake, 9ninyi milima na vilima vyote, miti ya matunda na mierezi yote, 10wanyama wa mwituni na mifugo yote, viumbe vidogo na ndege warukao, 11wafalme wa dunia na mataifa yote, ninyi wakuu na watawala wote wa dunia, 12wanaume vijana na wanawali, wazee na watoto. 13Wote na walisifu jina la Bwana, kwa maana jina lake pekee limetukuka, utukufu wake uko juu ya nchi na mbingu. 14Amewainulia watu wake pembe, sifa ya watakatifu wake wote, ya Israeli, watu walio karibu na moyo wake. Msifuni Bwana.

Namba za mistari hufuata tafsiri uliyochagua, na katika sura chache zinaweza kutofautiana kwa mstari mmoja.

Urahisi wa kusoma

Chagua kinachokusaidia. Chaguo lako linahifadhiwa kwenye kifaa hiki.

Ukubwa wa maandishi

Unapendelea mipangilio ya kifaa chako mwenyewe (kukuza, kisoma skrini, hali ya giza)? Inafanya kazi hapa pia.