Ruka hadi kwenye maudhui
Beta

Uzi bado haujatafsiriwa kikamilifu kwa Kiswahili. Kile ambacho bado hakijatafsiriwa kinaonyeshwa kwa Kiingereza.

Zaburi 49

Sura hii ni sehemu ya: Boek II

1Sikieni haya, enyi mataifa yote, sikilizeni, ninyi wote mkaao dunia hii. 2Wakubwa kwa wadogo, matajiri na maskini pamoja: 3Kinywa changu kitasema maneno ya hekima, usemi wa moyo wangu utatoa ufahamu. 4Nitatega sikio langu nisikilize mithali, nitafafanua kitendawili kwa zeze: 5Kwa nini niogope siku mbaya zinapokuja, wakati wadanganyifu waovu wanaponizunguka, 6wale wanaotegemea mali zao na kujivunia utajiri wao mwingi? 7Hakuna mwanadamu awaye yote awezaye kuukomboa uhai wa mwingine, au kumpa Mungu fidia kwa ajili yake. 8Fidia ya uhai ni gharama kubwa, hakuna malipo yoyote yanayotosha, 9ili kwamba aishi milele na asione uharibifu. 10Wote wanaona kwamba watu wenye hekima hufa; wajinga na wapumbavu vivyo hivyo huangamia na kuwaachia wengine mali zao. 11Makaburi yao yatabaki kuwa nyumba zao za milele, makao yao vizazi vyote; ingawa walikuwa na mashamba na kuyaita kwa majina yao. 12Lakini mwanadamu, licha ya utajiri wake, hadumu; anafanana na mnyama aangamiaye. 13Hii ndiyo hatima ya wale wanaojitumainia wenyewe, pia ya wafuasi wao, waliothibitisha misemo yao. 14Kama kondoo, wamewekewa kwenda kaburini, nacho kifo kitawala. Wanyofu watawatawala asubuhi, maumbile yao yataozea kaburini, mbali na majumba yao makubwa ya fahari. 15Lakini Mungu atakomboa uhai wangu na kaburi, hakika atanichukua kwake. 16Usitishwe mtu anapotajirika, fahari ya nyumba yake inapoongezeka, 17kwa maana hatachukua chochote atakapokufa, fahari yake haitashuka pamoja naye. 18Ingawa alipokuwa akiishi alijihesabu kuwa heri, na wanadamu wanakusifu unapofanikiwa, 19atajiunga na kizazi cha baba zake, ambao hawataona kamwe nuru ya uzima. 20Mwanadamu mwenye utajiri bila ufahamu ni kama wanyama waangamiao.

Namba za mistari hufuata tafsiri uliyochagua, na katika sura chache zinaweza kutofautiana kwa mstari mmoja.

Urahisi wa kusoma

Chagua kinachokusaidia. Chaguo lako linahifadhiwa kwenye kifaa hiki.

Ukubwa wa maandishi

Unapendelea mipangilio ya kifaa chako mwenyewe (kukuza, kisoma skrini, hali ya giza)? Inafanya kazi hapa pia.