Ruka hadi kwenye maudhui
Beta

Uzi bado haujatafsiriwa kikamilifu kwa Kiswahili. Kile ambacho bado hakijatafsiriwa kinaonyeshwa kwa Kiingereza.

Zaburi 47

Sura hii ni sehemu ya: Boek II

1Pigeni makofi, enyi mataifa yote, mpigieni Mungu kelele za shangwe! 2Jinsi gani alivyo wa kutisha, Bwana Aliye Juu Sana, Mfalme mkuu juu ya dunia yote! 3Ametiisha mataifa chini yetu watu wengi chini ya miguu yetu. 4Alituchagulia urithi wetu, fahari ya Yakobo, aliyempenda. 5Mungu amepaa kwa kelele za shangwe, Bwana kwa sauti za tarumbeta. 6Mwimbieni Mungu sifa, imbeni sifa, mwimbieni sifa Mfalme wetu, imbeni sifa. 7Kwa kuwa Mungu ni mfalme wa dunia yote, mwimbieni zaburi za sifa. 8Mungu anatawala juu ya mataifa, Mungu ameketi juu ya kiti chake cha enzi kitakatifu. 9Wakuu wa mataifa wanakusanyika kama watu wa Mungu wa Abrahamu, kwa kuwa wafalme wa dunia ni mali ya Mungu; yeye ametukuka sana.

Namba za mistari hufuata tafsiri uliyochagua, na katika sura chache zinaweza kutofautiana kwa mstari mmoja.

Urahisi wa kusoma

Chagua kinachokusaidia. Chaguo lako linahifadhiwa kwenye kifaa hiki.

Ukubwa wa maandishi

Unapendelea mipangilio ya kifaa chako mwenyewe (kukuza, kisoma skrini, hali ya giza)? Inafanya kazi hapa pia.