1Mpigieni Mungu kelele za shangwe, dunia yote! 2Imbeni utukufu wa jina lake; mpeni sifa zake kwa utukufu! 3Mwambieni Mungu, “Jinsi gani yalivyo ya kutisha matendo yako! Uwezo wako ni mkuu mno kiasi kwamba adui wananyenyekea mbele zako. 4Dunia yote yakusujudia, wanakuimbia wewe sifa, wanaliimbia sifa jina lako.” 5Njooni mwone yale Mungu aliyoyatenda, mambo ya kutisha aliyoyatenda miongoni mwa wanadamu! 6Alifanya bahari kuwa nchi kavu, wakapita kati ya maji kwa miguu, njooni, tumshangilie. 7Yeye hutawala kwa uwezo wake milele, macho yake huangalia mataifa yote: waasi wasithubutu kujiinua dhidi yake. 8Enyi mataifa, msifuni Mungu wetu, sauti ya sifa yake isikike, 9ameyahifadhi maisha yetu na kuizuia miguu yetu kuteleza. 10Ee Mungu, wewe ulitujaribu, ukatusafisha kama fedha. 11Umetuingiza kwenye nyavu na umetubebesha mizigo mizito migongoni mwetu. 12Uliwaruhusu watu watukalie vichwani, tulipita kwenye moto na kwenye maji, lakini ulituleta kwenye nchi iliyojaa utajiri tele. 13Nitakuja hekaluni mwako na sadaka za kuteketezwa na kukutimizia nadhiri zangu: 14nadhiri ambazo midomo yangu iliahidi na nilizotamka kwa kinywa changu nilipokuwa katika shida. 15Nitakutolea dhabihu za wanyama wanono na sadaka za kondoo dume, nitakutolea mafahali na mbuzi. 16Njooni msikilize ninyi nyote mnaomcha Mungu, nami niwaambie aliyonitendea. 17Nilimlilia kwa kinywa changu, sifa zake zilikuwa katika ulimi wangu. 18Kama ningekuwa nimeyaficha maovu moyoni mwangu, Bwana asingekuwa amenisikiliza; 19lakini hakika Mungu amenisikiliza na amesikia sauti yangu katika maombi. 20Sifa apewe Mungu, ambaye hakulikataa ombi langu wala kunizuilia upendo wake!
1Make a joyful shout to God, all the earth! 2Sing to the glory of his name! Offer glory and praise! 3Tell God, “How awesome are your deeds! Through the greatness of your power, your enemies submit themselves to you. 4All the earth will worship you, and will sing to you; they will sing to your name.” Selah. 5Come, and see God’s deeds— awesome work on behalf of the children of men. 6He turned the sea into dry land. They went through the river on foot. There, we rejoiced in him. 7He rules by his might forever. His eyes watch the nations. Don’t let the rebellious rise up against him. Selah. 8Praise our God, you peoples! Make the sound of his praise heard, 9who preserves our life among the living, and doesn’t allow our feet to be moved. 10For you, God, have tested us. You have refined us, as silver is refined. 11You brought us into prison. You laid a burden on our backs. 12You allowed men to ride over our heads. We went through fire and through water, but you brought us to the place of abundance. 13I will come into your temple with burnt offerings. I will pay my vows to you, 14which my lips promised, and my mouth spoke, when I was in distress. 15I will offer to you burnt offerings of fat animals, with the offering of rams, I will offer bulls with goats. Selah. 16Come, and hear, all you who fear God. I will declare what he has done for my soul. 17I cried to him with my mouth. He was extolled with my tongue. 18If I cherished sin in my heart, the Lord wouldn’t have listened. 19But most certainly, God has listened. He has heard the voice of my prayer. 20Blessed be God, who has not turned away my prayer, nor his loving kindness from me.
1Een lied, een psalm, voor den opperzangmeester. Juicht Gode, gij ganse aarde! 2Psalmzingt de eer Zijns Naams; geeft eer Zijn lof. 3Zegt tot God: Hoe vreselijk zijt Gij in Uw werken! Om de grootheid Uwer sterkte zullen zich Uw vijanden geveinsdelijk aan U onderwerpen. 4De ganse aarde aanbidde U, en psalmzinge U; zij psalmzinge Uw Naam. Sela. 5Komt en ziet Gods daden; Hij is vreselijk van werking aan de mensenkinderen. 6Hij heeft de zee veranderd in het droge; zij zijn te voet doorgegaan door de rivier; daar hebben wij ons in Hem verblijd. 7Hij heerst eeuwiglijk met Zijn macht; Zijn ogen houden wacht over de heidenen; laat de afvalligen niet verhoogd worden. Sela. 8Looft, gij volken! onzen God; en laat horen de stem Zijns roems. 9Die onze zielen in het leven stelt, en niet toelaat, dat onze voet wankele. 10Want Gij hebt ons beproefd, o God! Gij hebt ons gelouterd, gelijk men het zilver loutert; 11Gij hadt ons in het net gebracht; Gij hadt een engen band om onze lenden gelegd; 12Gij hadt den mens op ons hoofd doen rijden; wij waren in het vuur en in het water gekomen; maar Gij hebt ons uitgevoerd in een overvloeiende verversing. 13Ik zal met brandofferen in Uw huis gaan; ik zal U mijn geloften betalen, 14Die mijn lippen hebben geuit, en mijn mond heeft uitgesproken, als mij bange was. 15Brandofferen van mergbeesten zal ik U offeren, met rookwerk van rammen; ik zal runderen met bokken bereiden. Sela. 16Komt, hoort toe, o allen gij, die God vreest, en ik zal vertellen, wat Hij aan mijn ziel gedaan heeft. 17Ik riep tot Hem met mijn mond, en Hij werd verhoogd onder mijn tong. 18Had ik naar ongerechtigheid met mijn hart gezien, de Heere zou niet gehoord hebben. 19Maar zeker, God heeft gehoord; Hij heeft gemerkt op de stem mijns gebeds. 20Geloofd zij God, Die mijn gebed niet heeft afgewend, noch Zijn goedertierenheid van mij.
Bonyeza Enter ili kuuwekea mstari huu rangi, kuandika maelezo au kuunakili. Vitufe vya mishale vinakupeleka kwenye mstari unaofuata.
Namba za mistari hufuata tafsiri uliyochagua, na katika sura chache zinaweza kutofautiana kwa mstari mmoja.