Ruka hadi kwenye maudhui
Beta

Uzi bado haujatafsiriwa kikamilifu kwa Kiswahili. Kile ambacho bado hakijatafsiriwa kinaonyeshwa kwa Kiingereza.

Zaburi 91

Sura hii ni sehemu ya: Boek IV

1Yeye akaaye mahali pa salama pake Yeye Aliye Juu Sana, atadumu katika uvuli wake Mwenyezi. 2Nitasema kumhusu Bwana, “Yeye ndiye kimbilio langu na ngome yangu, Mungu wangu, ambaye ninamtumaini.” 3Hakika yeye ataniokoa na mtego wa mwindaji, na maradhi ya kuambukiza ya kuua. 4Atakufunika kwa manyoya yake, chini ya mbawa zake utapata kimbilio, uaminifu wake utakuwa ngao na kinga yako. 5Hutaogopa vitisho vya usiku, wala mshale urukao mchana, 6wala maradhi ya kuambukiza yanayonyemelea gizani, wala tauni iharibuyo adhuhuri. 7Ijapo watu elfu wataangukia kando yako, kumi elfu mkono wako wa kuume, lakini haitakukaribia wewe. 8Utatazama tu kwa macho yako na kuona adhabu ya waovu. 9Kama ukimfanya Aliye Juu Sana kuwa makao yako: naam, Bwana ambaye ni kimbilio langu, 10basi hakuna madhara yatakayokupata wewe, hakuna maafa yataikaribia hema yako. 11Kwa kuwa atawaagiza malaika zake kwa ajili yako, wakulinde katika njia zako zote. 12Mikononi mwao watakuinua, ili usijikwae mguu wako kwenye jiwe. 13Utawakanyaga simba na nyoka wakali, simba mkubwa na nyoka utawaponda kwa miguu. 14Bwana asema, “Kwa kuwa ananipenda, nitamwokoa; nitamlinda, kwa kuwa analikiri Jina langu. 15Ataniita, nami nitamjibu; nitakuwa pamoja naye katika taabu, nitamwokoa na kumheshimu. 16Kwa siku nyingi nitamshibisha na kumwonyesha wokovu wangu.”

Namba za mistari hufuata tafsiri uliyochagua, na katika sura chache zinaweza kutofautiana kwa mstari mmoja.

Urahisi wa kusoma

Chagua kinachokusaidia. Chaguo lako linahifadhiwa kwenye kifaa hiki.

Ukubwa wa maandishi

Unapendelea mipangilio ya kifaa chako mwenyewe (kukuza, kisoma skrini, hali ya giza)? Inafanya kazi hapa pia.