Ruka hadi kwenye maudhui
Beta

Uzi bado haujatafsiriwa kikamilifu kwa Kiswahili. Kile ambacho bado hakijatafsiriwa kinaonyeshwa kwa Kiingereza.

Zaburi 81

Sura hii ni sehemu ya: Boek III

1Mwimbieni kwa furaha, Mungu aliye nguvu yetu; mpigieni kelele za shangwe Mungu wa Yakobo! 2Anzeni wimbo, pigeni matari, pigeni kinubi na zeze kwa sauti nzuri. 3Pigeni baragumu za pembe za kondoo dume wakati wa Mwandamo wa Mwezi, na wakati wa mwezi mpevu, katika siku ya Sikukuu yetu; 4hii ni amri kwa Israeli, agizo la Mungu wa Yakobo. 5Aliiweka iwe kama sheria kwa Yosefu alipotoka dhidi ya Misri, huko tulikosikia lugha ambayo hatukuielewa. 6Asema, “Nimeondoa mzigo mabegani mwao; mikono yao iliwekwa huru kutoka kwenye kikapu. 7Katika shida yako uliniita nami nikakuokoa, nilikujibu katika mawingu yenye ngurumo; nilikujaribu katika maji ya Meriba. 8“Enyi watu wangu, sikieni, nami nitawaonya: laiti kama mngenisikiliza, ee Israeli! 9Hamtakuwa na mungu mgeni miongoni mwenu; msimsujudie mungu wa kigeni. 10Mimi ni Bwana Mungu wako, niliyekutoa nchi ya Misri. Panua sana kinywa chako nami nitakijaza. 11“Lakini watu wangu hawakutaka kunisikiliza; Israeli hakutaka kunitii. 12Basi niliwaacha katika ukaidi wa mioyo yao wafuate mashauri yao wenyewe. 13“Laiti kama watu wangu wangalinisikiliza, kama Israeli wangalifuata njia zangu, 14ningaliwatiisha adui zao kwa haraka, na kuugeuza mkono wangu dhidi ya watesi wao! 15Wale wanaomchukia Bwana wangalinyenyekea mbele zake, na adhabu yao ingedumu milele. 16Bali ninyi mngalilishwa ngano iliyo bora, na kuwatosheleza kwa asali itokayo kwenye mwamba.”

Namba za mistari hufuata tafsiri uliyochagua, na katika sura chache zinaweza kutofautiana kwa mstari mmoja.

Urahisi wa kusoma

Chagua kinachokusaidia. Chaguo lako linahifadhiwa kwenye kifaa hiki.

Ukubwa wa maandishi

Unapendelea mipangilio ya kifaa chako mwenyewe (kukuza, kisoma skrini, hali ya giza)? Inafanya kazi hapa pia.