1Ee Mungu, moyo wangu ni thabiti; nitaimba na kusifu kwa moyo wangu wote. 2Amka, kinubi na zeze! Nitayaamsha mapambazuko. 3Nitakusifu wewe, Ee Bwana, katikati ya mataifa; nitaimba habari zako, katikati ya jamaa za watu. 4Kwa maana upendo wako ni mkuu, ni juu kuliko mbingu; uaminifu wako unazifikia anga. 5Ee Mungu, utukuzwe juu ya mbingu, utukufu wako na uenee duniani kote. 6Tuokoe na utusaidie kwa mkono wako wa kuume, ili wale uwapendao wapate kuokolewa. 7Mungu amenena kutoka patakatifu pake: “Nitaigawa Shekemu kwa ushindi na kulipima Bonde la Sukothi. 8Gileadi ni yangu, Manase ni yangu, Efraimu ni kofia yangu ya chuma, nayo Yuda ni fimbo yangu ya utawala. 9Moabu ni sinia langu la kunawia, juu ya Edomu natupa kiatu changu; nashangilia kwa kushindwa kwa Ufilisti.” 10Ni nani atakayenipeleka hadi mji wenye ngome? Ni nani atakayeniongoza hadi nifike Edomu? 11Ee Mungu, si ni wewe uliyetukataa sisi, na hutoki tena na majeshi yetu? 12Tuletee msaada dhidi ya adui, kwa maana msaada wa mwanadamu haufai kitu. 13Kwa msaada wa Mungu tutapata ushindi, naye atawaponda adui zetu.
1My heart is steadfast, God. I will sing and I will make music with my soul. 2Wake up, harp and lyre! I will wake up the dawn. 3I will give thanks to you, Yahweh, among the nations. I will sing praises to you among the peoples. 4For your loving kindness is great above the heavens. Your faithfulness reaches to the skies. 5Be exalted, God, above the heavens! Let your glory be over all the earth. 6That your beloved may be delivered, save with your right hand, and answer us. 7God has spoken from his sanctuary: “In triumph, I will divide Shechem, and measure out the valley of Succoth. 8Gilead is mine. Manasseh is mine. Ephraim also is my helmet. Judah is my scepter. 9Moab is my wash pot. I will toss my sandal on Edom. I will shout over Philistia.” 10Who will bring me into the fortified city? Who has led me to Edom? 11Haven’t you rejected us, God? You don’t go out, God, with our armies. 12Give us help against the enemy, for the help of man is vain. 13Through God, we will do valiantly. For it is he who will tread down our enemies.
1Een lied, een psalm van David. 2O God! mijn hart is bereid; ik zal zingen en psalmzingen, ook mijn eer. 3Waak op, gij luit en harp! ik zal in den dageraad opwaken. 4Ik zal U loven onder de volken, o HEERE! en ik zal U psalmzingen onder de natien. 5Want Uw goedertierenheid is groot tot boven de hemelen, en Uw waarheid tot aan de bovenste wolken. 6Verhef U, o God! boven de hemelen, en Uw eer over de ganse aarde. 7Opdat Uw beminden bevrijd worden; geef heil door Uw rechterhand, en verhoor ons. 8God heeft gesproken in Zijn heiligdom, dies zal ik van vreugde opspringen; ik zal Sichem delen, en het dal van Sukkoth zal ik afmeten. 9Gilead is mijn, Manasse is mijn, en Efraim is de sterkte mijns hoofds; Juda is mijn wetgever. 10Moab is mijn waspot; op Edom zal ik mijn schoen werpen; over Palestina zal ik juichen. 11Wie zal mij voeren in een vaste stad? Wie zal mij leiden tot in Edom? 12Zult Gij het niet zijn, o God! Die ons verstoten hadt, en Die niet uittoogt, o God! met onze heirkrachten? 13Geef Gij ons hulp uit de benauwdheid; want des mensen heil is ijdelheid. In God zullen wij kloeke daden doen, en Hij zal onze wederpartijders vertreden.
Bonyeza Enter ili kuuwekea mstari huu rangi, kuandika maelezo au kuunakili. Vitufe vya mishale vinakupeleka kwenye mstari unaofuata.
Namba za mistari hufuata tafsiri uliyochagua, na katika sura chache zinaweza kutofautiana kwa mstari mmoja.