Ruka hadi kwenye maudhui
Beta

Uzi bado haujatafsiriwa kikamilifu kwa Kiswahili. Kile ambacho bado hakijatafsiriwa kinaonyeshwa kwa Kiingereza.

Zaburi 75

Sura hii ni sehemu ya: Boek III

1Ee Mungu, tunakushukuru, tunakushukuru wewe, kwa kuwa jina lako li karibu; watu husimulia matendo yako ya ajabu. 2Unasema, “Ninachagua wakati maalum; ni mimi nihukumuye kwa haki. 3Wakati dunia na watu wake wote inapotetemeka, ni mimi ninayezishikilia nguzo zake imara. 4Kwa wale wenye majivuno ninasema, ‘Msijisifu tena,’ kwa wale waovu, ‘Msiinue pembe zenu. 5Msiinue pembe zenu dhidi ya mbingu; msiseme kwa shingo zilizonyooshwa.’” 6Hakuna yeyote atokaye mashariki wala magharibi au kutoka jangwani awezaye kumkweza mwanadamu. 7Bali Mungu ndiye ahukumuye: Humshusha huyu na kumkweza mwingine. 8Mkononi mwa Bwana kuna kikombe kilichojaa mvinyo unaotoka povu uliochanganywa na vikolezo; huumimina, nao waovu wote wa dunia hunywa mpaka tone la mwisho. 9Bali mimi, nitatangaza hili milele; nitaimba sifa kwa Mungu wa Yakobo. 10Nitazikatilia mbali pembe za waovu wote, bali pembe za wenye haki zitainuliwa juu.

Namba za mistari hufuata tafsiri uliyochagua, na katika sura chache zinaweza kutofautiana kwa mstari mmoja.

Urahisi wa kusoma

Chagua kinachokusaidia. Chaguo lako linahifadhiwa kwenye kifaa hiki.

Ukubwa wa maandishi

Unapendelea mipangilio ya kifaa chako mwenyewe (kukuza, kisoma skrini, hali ya giza)? Inafanya kazi hapa pia.