1Sikia, Ee Bwana, kusihi kwangu kwa haki, sikiliza kilio changu. Tega sikio kwa ombi langu, halitoki kwenye midomo ya udanganyifu. 2Hukumu yangu na itoke kwako, macho yako na yaone yale yaliyo haki. 3Ingawa unauchunguza moyo wangu na kunikagua usiku, ingawa umenijaribu, hutaona chochote. Nimeamua kwamba kinywa changu hakitatenda dhambi. 4Kuhusu matendo ya wanadamu: kwa neno la midomo yako, nimejiepusha na njia za wenye jeuri. 5Hatua zangu zimeshikamana na njia zako; nyayo zangu hazikuteleza. 6Ee Mungu, ninakuita, kwa kuwa utanijibu, nitegee sikio lako na usikie ombi langu. 7Uonyeshe ajabu ya upendo wako mkuu, wewe uokoaye kwa mkono wako wa kuume wale wanaokukimbilia kutokana na adui zao. 8Nilinde kama mboni ya jicho lako, unifiche chini ya kivuli cha mbawa zako 9kutokana na waovu wanaonishambulia, kutokana na adui wauaji wanaonizunguka. 10Huifunga mioyo yao iliyo migumu, vinywa vyao hunena kwa majivuno. 11Wamenifuatia nyayo zangu, sasa wamenizingira, wakiwa macho, waniangushe chini. 12Wamefanana na simba mwenye njaa awindaye, kama simba mkubwa anyemeleaye mafichoni. 13Inuka, Ee Bwana, pambana nao, uwaangushe, niokoe kutokana na waovu kwa upanga wako. 14Ee Bwana, mkono wako uniokoe na watu wa jinsi hii, kutokana na watu wa ulimwengu huu ambao fungu lao liko katika maisha haya. Na wapate adhabu ya kuwatosha. Watoto wao na wapate zaidi ya hayo, hukumu na iendelee kwa watoto wa watoto wao. 15Na mimi katika haki nitauona uso wako, niamkapo, nitaridhika kwa kuona sura yako.
1Hear, Yahweh, my righteous plea; Give ear to my prayer, that doesn’t go out of deceitful lips. 2Let my sentence come out of your presence. Let your eyes look on equity. 3You have proved my heart. You have visited me in the night. You have tried me, and found nothing. I have resolved that my mouth shall not disobey. 4As for the works of men, by the word of your lips, I have kept myself from the ways of the violent. 5My steps have held fast to your paths. My feet have not slipped. 6I have called on you, for you will answer me, God. Turn your ear to me. Hear my speech. 7Show your marvelous loving kindness, you who save those who take refuge by your right hand from their enemies. 8Keep me as the apple of your eye. Hide me under the shadow of your wings, 9from the wicked who oppress me, my deadly enemies, who surround me. 10They close up their callous hearts. With their mouth they speak proudly. 11They have now surrounded us in our steps. They set their eyes to cast us down to the earth. 12He is like a lion that is greedy of his prey, as it were a young lion lurking in secret places. 13Arise, Yahweh, confront him. Cast him down. Deliver my soul from the wicked by your sword; 14from men by your hand, Yahweh, from men of the world, whose portion is in this life. You fill the belly of your cherished ones. Your sons have plenty, and they store up wealth for their children. 15As for me, I shall see your face in righteousness. I shall be satisfied, when I awake, with seeing your form.
1Een gebed van David. HEERE! hoor de gerechtigheid, merk op mijn geschrei, neem ter ore mijn gebed, met onbedriegelijke lippen gesproken. 2Laat mijn recht van voor Uw aangezicht uitgaan, laat Uw ogen de billijkheden aanschouwen. 3Gij hebt mijn hart geproefd, des nachts bezocht, Gij hebt mij getoetst. Gij vindt niets; hetgeen ik gedacht heb, overtreedt mijn mond niet. 4Aangaande de handelingen des mensen, ik heb mij, naar het woord Uwer lippen, gewacht voor de paden des inbrekers; 5Houdende mijn gangen in Uw sporen, opdat mijn voetstappen niet zouden wankelen. 6Ik roep U aan, omdat Gij mij verhoort; o God! neig Uw oor tot mij; hoor mijn rede. 7Maak Uw weldadigheden wonderbaar, Gij, Die verlost degenen, die op U betrouwen, van degenen, die tegen Uw rechterhand opstaan! 8Bewaar mij als het zwart des oogappels, verberg mij onder de schaduw Uwer vleugelen, 9Voor het aangezicht der goddelozen, die mij verwoesten, mijner doodsvijanden, die mij omringen. 10Met hun vet besluiten zij zich, met hun mond spreken zij hovaardelijk. 11In onzen gang hebben zij ons nu omsingeld, zij zetten hun ogen op ons ter aarde nederbukkende. 12Hij is gelijk als een leeuw, die begeert te roven, en als een jonge leeuw, zittende in verborgen plaatsen. 13Sta op, HEERE, kom zijn aangezicht voor, vel hem neder; bevrijd mijn ziel met Uw zwaard van den goddeloze; 14Met Uw hand van de lieden, o HEERE! van de lieden, die van de wereld zijn, welker deel in dit leven is, welker buik Gij vervult met Uw verborgen schat; de kinderen worden verzadigd, en zij laten hun overschot hun kinderkens achter. 15Maar ik zal Uw aangezicht in gerechtigheid aanschouwen, ik zal verzadigd worden met Uw beeld, als ik zal opwaken.
Bonyeza Enter ili kuuwekea mstari huu rangi, kuandika maelezo au kuunakili. Vitufe vya mishale vinakupeleka kwenye mstari unaofuata.
Namba za mistari hufuata tafsiri uliyochagua, na katika sura chache zinaweza kutofautiana kwa mstari mmoja.