Ruka hadi kwenye maudhui
Beta

Uzi bado haujatafsiriwa kikamilifu kwa Kiswahili. Kile ambacho bado hakijatafsiriwa kinaonyeshwa kwa Kiingereza.

Zaburi 149

Sura hii ni sehemu ya: Boek V

1Msifuni Bwana. Mwimbieni Bwana wimbo mpya, sifa zake katika kusanyiko la watakatifu. 2Israeli na washangilie katika Muumba wao, watu wa Sayuni na wafurahi katika Mfalme wao. 3Na walisifu jina lake kwa kucheza na wampigie muziki kwa matari na kinubi. 4Kwa maana Bwana anapendezwa na watu wake, anawavika wanyenyekevu taji ya wokovu. 5Watakatifu washangilie katika heshima hii, na waimbe kwa shangwe vitandani mwao. 6Sifa za Mungu na ziwe vinywani mwao na upanga ukatao kuwili mikononi mwao, 7ili walipize mataifa kisasi na adhabu juu ya mataifa, 8wawafunge wafalme wao kwa minyororo, wakuu wao kwa pingu za chuma, 9ili kuwafanyia hukumu iliyoandikwa dhidi yao. Huu ndio utukufu wa watakatifu wake wote. Msifuni Bwana.

Namba za mistari hufuata tafsiri uliyochagua, na katika sura chache zinaweza kutofautiana kwa mstari mmoja.

Urahisi wa kusoma

Chagua kinachokusaidia. Chaguo lako linahifadhiwa kwenye kifaa hiki.

Ukubwa wa maandishi

Unapendelea mipangilio ya kifaa chako mwenyewe (kukuza, kisoma skrini, hali ya giza)? Inafanya kazi hapa pia.