1Ee Bwana, nithibitishe katika haki, maana nimeishi maisha yasiyo na lawama; nimemtumainia Bwana bila kusitasita. 2Ee Bwana, unijaribu, unipime, uuchunguze moyo wangu na mawazo yangu; 3kwa maana upendo wako uko mbele yangu daima, nami natembea siku zote katika kweli yako. 4Siketi pamoja na watu wadanganyifu, wala siandamani na wanafiki, 5ninachukia kusanyiko la watenda mabaya na ninakataa kuketi pamoja na waovu. 6Ninanawa mikono yangu kwa kuwa sina hatia, naikaribia madhabahu yako, Ee Bwana, 7nikitangaza sifa yako kwa sauti kubwa, huku nikisimulia matendo yako ya ajabu. 8Ee Bwana, naipenda nyumba yako mahali unakoishi, mahali ambapo utukufu wako hukaa. 9Usiiondoe nafsi yangu pamoja na watenda dhambi, wala uhai wangu pamoja na wamwagao damu, 10ambao mikononi mwao kuna mipango miovu, ambao mikono yao ya kuume imejaa rushwa. 11Bali mimi ninaishi maisha yasiyo na lawama; nikomboe na unihurumie. 12Miguu yangu imesimama katika uwanja tambarare; katika kusanyiko kuu nitamsifu Bwana.
1Judge me, Yahweh, for I have walked in my integrity. I have trusted also in Yahweh without wavering. 2Examine me, Yahweh, and prove me. Try my heart and my mind. 3For your loving kindness is before my eyes. I have walked in your truth. 4I have not sat with deceitful men, neither will I go in with hypocrites. 5I hate the assembly of evildoers, and will not sit with the wicked. 6I will wash my hands in innocence, so I will go about your altar, Yahweh; 7that I may make the voice of thanksgiving to be heard, and tell of all your wondrous works. 8Yahweh, I love the habitation of your house, the place where your glory dwells. 9Don’t gather my soul with sinners, nor my life with bloodthirsty men; 10in whose hands is wickedness, their right hand is full of bribes. 11But as for me, I will walk in my integrity. Redeem me, and be merciful to me. 12My foot stands in an even place. In the congregations I will bless Yahweh.
1Een psalm van David! Doe mij recht, HEERE! want ik wandel in mijn oprechtigheid; en ik vertrouw op den HEERE, ik zal niet wankelen. 2Proef mij, HEERE, en verzoek mij; toets mijn nieren en mijn hart. 3Want Uw goedertierenheid is voor mijn ogen, en ik wandel in Uw waarheid. 4Ik zit niet bij ijdele lieden, en met bedekte lieden ga ik niet om. 5Ik haat de vergadering der boosdoeners, en bij de goddelozen zit ik niet. 6Ik was mijn handen in onschuld, en ik ga rondom uw altaar, o HEERE! 7Om te doen horen de stem des lofs, en om te vertellen al Uw wonderen. 8HEERE! ik heb lief de woning van Uw huis, en de plaats des tabernakels Uwer eer. 9Raap mijn ziel niet weg met de zondaren, noch mijn leven met de mannen des bloeds; 10In welker handen schandelijk bedrijf is, en welker rechterhand vol geschenken is. 11Maar ik wandel in mijn oprechtigheid, verlos mij dan en wees mij genadig. 12Mijn voet staat op effen baan; ik zal den HEERE loven in de vergaderingen.
Bonyeza Enter ili kuuwekea mstari huu rangi, kuandika maelezo au kuunakili. Vitufe vya mishale vinakupeleka kwenye mstari unaofuata.
Namba za mistari hufuata tafsiri uliyochagua, na katika sura chache zinaweza kutofautiana kwa mstari mmoja.