Ruka hadi kwenye maudhui
Beta

Uzi bado haujatafsiriwa kikamilifu kwa Kiswahili. Kile ambacho bado hakijatafsiriwa kinaonyeshwa kwa Kiingereza.

Zaburi 76

Sura hii ni sehemu ya: Boek III

1Katika Yuda, Mungu anajulikana, jina lake ni kuu katika Israeli. 2Hema lake liko Salemu, makao yake katika Sayuni. 3Huko alivunja mishale imetametayo, ngao na panga, silaha za vita. 4Wewe unangʼaa kwa mwanga, mwenye fahari zaidi ya milima yenye utajiri wa wanyama pori. 5Mashujaa hulala wametekwa nyara, hulala usingizi wao wa mwisho; hakuna hata mmoja wa watu wa vita anayeweza kuinua mikono yake. 6Kwa kukemea kwako, Ee Mungu wa Yakobo, farasi na gari la vita vilikaa kimya. 7Wewe peke yako ndiye wa kuogopwa. Ni nani awezaye kusimama mbele yako unapokasirika? 8Kutoka mbinguni ulitamka hukumu, nayo nchi ikaogopa, ikawa kimya: 9wakati wewe, Ee Mungu, ulipoinuka kuhukumu, kuwaokoa wote walioonewa katika nchi. 10Hakika ghadhabu yako dhidi ya wanadamu inakuletea sifa, na masalia ya ghadhabu yako unajifunga mshipi. 11Wekeni nadhiri kwa Bwana Mungu wenu na kuzitimiza; nchi zote za jirani na walete zawadi kwa Yule astahiliye kuogopwa. 12Huvunja roho za watawala; anaogopwa na wafalme wa dunia.

Namba za mistari hufuata tafsiri uliyochagua, na katika sura chache zinaweza kutofautiana kwa mstari mmoja.

Urahisi wa kusoma

Chagua kinachokusaidia. Chaguo lako linahifadhiwa kwenye kifaa hiki.

Ukubwa wa maandishi

Unapendelea mipangilio ya kifaa chako mwenyewe (kukuza, kisoma skrini, hali ya giza)? Inafanya kazi hapa pia.