Ruka hadi kwenye maudhui
Beta

Uzi bado haujatafsiriwa kikamilifu kwa Kiswahili. Kile ambacho bado hakijatafsiriwa kinaonyeshwa kwa Kiingereza.

Zaburi 6

Sura hii ni sehemu ya: Boek I

1Ee Bwana, usinikemee katika hasira yako, wala usiniadhibu katika ghadhabu yako. 2Unirehemu Bwana, kwa maana nimedhoofika; Ee Bwana, uniponye, kwa maana mifupa yangu ina maumivu makali. 3Nafsi yangu ina uchungu mwingi. Mpaka lini, Ee Bwana, mpaka lini? 4Geuka Ee Bwana, unikomboe, uniokoe kwa sababu ya fadhili zako. 5Hakuna mtu anayekukumbuka akiwa amekufa. Ni nani awezaye kukusifu akiwa kuzimu? 6Nimechakaa kwa kulia kwa huzuni; usiku kucha nafurikisha kitanda changu kwa machozi; nimelowesha viti vyangu vya fahari kwa machozi. 7Macho yangu yamedhoofika kwa kuhuzunika, yamedhoofika kwa sababu ya adui zangu wote. 8Kaeni mbali nami, ninyi nyote mtendao mabaya, kwa maana Bwana amesikia kulia kwangu. 9Bwana amesikia kilio changu kwa huruma, Bwana amekubali sala yangu. 10Adui zangu wote wataaibika na kufadhaika, watarudi nyuma kwa aibu ya ghafula.

Namba za mistari hufuata tafsiri uliyochagua, na katika sura chache zinaweza kutofautiana kwa mstari mmoja.

Urahisi wa kusoma

Chagua kinachokusaidia. Chaguo lako linahifadhiwa kwenye kifaa hiki.

Ukubwa wa maandishi

Unapendelea mipangilio ya kifaa chako mwenyewe (kukuza, kisoma skrini, hali ya giza)? Inafanya kazi hapa pia.