Ruka hadi kwenye maudhui
Beta

Uzi bado haujatafsiriwa kikamilifu kwa Kiswahili. Kile ambacho bado hakijatafsiriwa kinaonyeshwa kwa Kiingereza.

Zaburi 85

Sura hii ni sehemu ya: Boek III

1Ee Bwana, ulionyesha wema kwa nchi yako. Ulimrejeshea Yakobo baraka zake. 2Ulisamehe uovu wa watu wako, na kufunika dhambi zao zote. 3Uliweka kando ghadhabu yako yote na umegeuka na kuiacha hasira yako kali. 4Ee Mungu Mwokozi wetu, uturejeshe tena, nawe uiondoe chuki yako juu yetu. 5Je, utatukasirikia milele? Utaendeleza hasira yako kwa vizazi vyote? 6Je, hutatuhuisha tena, ili watu wako wakufurahie? 7Utuonyeshe upendo wako usiokoma, Ee Bwana, utupe wokovu wako. 8Nitasikiliza lile atakalosema Mungu aliye Bwana; anaahidi amani kwa watu wake, watakatifu wake: lakini nao wasirudie upumbavu. 9Hakika wokovu wake uko karibu na wale wamchao, ili utukufu wake udumu katika nchi yetu. 10Upendo na uaminifu hukutana pamoja, haki na amani hubusiana. 11Uaminifu huchipua kutoka nchi, haki hutazama chini kutoka mbinguni. 12Naam, hakika Bwana atatoa kilicho chema, nayo nchi yetu itazaa mavuno yake. 13Haki itatangulia mbele yake na kutengeneza njia kwa ajili ya hatua zake.

Namba za mistari hufuata tafsiri uliyochagua, na katika sura chache zinaweza kutofautiana kwa mstari mmoja.

Urahisi wa kusoma

Chagua kinachokusaidia. Chaguo lako linahifadhiwa kwenye kifaa hiki.

Ukubwa wa maandishi

Unapendelea mipangilio ya kifaa chako mwenyewe (kukuza, kisoma skrini, hali ya giza)? Inafanya kazi hapa pia.