Ruka hadi kwenye maudhui
Beta

Uzi bado haujatafsiriwa kikamilifu kwa Kiswahili. Kile ambacho bado hakijatafsiriwa kinaonyeshwa kwa Kiingereza.

Zaburi 113

Sura hii ni sehemu ya: Boek V

1Msifuni Bwana. Enyi watumishi wa Bwana msifuni, lisifuni jina la Bwana. 2Jina la Bwana na lisifiwe, sasa na hata milele. 3Kuanzia mawio ya jua hadi machweo yake, jina la Bwana linapaswa kusifiwa. 4Bwana ametukuka juu ya mataifa yote, utukufu wake juu ya mbingu. 5Ni nani aliye kama Bwana Mungu wetu, Yeye ambaye ameketi juu kwenye kiti cha enzi, 6ambaye huinama atazame chini aone mbingu na nchi? 7Huwainua maskini kutoka mavumbini, na kuwanyanyua wahitaji kutoka kwenye jalala, 8huwaketisha pamoja na wakuu, pamoja na wakuu wa watu wake. 9Humjalia mwanamke tasa kutulia nyumbani mwake, akiwa mama watoto mwenye furaha. Msifuni Bwana.

Namba za mistari hufuata tafsiri uliyochagua, na katika sura chache zinaweza kutofautiana kwa mstari mmoja.

Urahisi wa kusoma

Chagua kinachokusaidia. Chaguo lako linahifadhiwa kwenye kifaa hiki.

Ukubwa wa maandishi

Unapendelea mipangilio ya kifaa chako mwenyewe (kukuza, kisoma skrini, hali ya giza)? Inafanya kazi hapa pia.