Ruka hadi kwenye maudhui
Beta

Uzi bado haujatafsiriwa kikamilifu kwa Kiswahili. Kile ambacho bado hakijatafsiriwa kinaonyeshwa kwa Kiingereza.

Zaburi 21

Sura hii ni sehemu ya: Boek I

1Ee Bwana, mfalme huzifurahia nguvu zako. Tazama jinsi ilivyo kuu furaha yake kwa ushindi unaompa! 2Umempa haja ya moyo wake na hukumzuilia maombi ya midomo yake. 3Ulimkaribisha kwa baraka tele na kumvika taji ya dhahabu safi kichwani pake. 4Alikuomba maisha, nawe ukampa, wingi wa siku milele na milele. 5Kutokana na ushindi uliompa, utukufu wake ni mkubwa, umeweka juu yake fahari na utukufu. 6Hakika umempa baraka za milele, umemfanya awe na furaha kwa shangwe ya uwepo wako. 7Kwa kuwa mfalme anamtumaini Bwana; kwa upendo usiokoma wa Aliye Juu Sana hatatikiswa. 8Mkono wako utawashika adui zako wote, mkono wako wa kuume utawakamata adui zako. 9Wakati utakapojitokeza utawafanya kama tanuru ya moto. Katika ghadhabu yake Bwana atawameza, moto wake utawateketeza. 10Utawaangamiza wazao wao kutoka duniani, uzao wao kutoka wanadamu. 11Ingawa watapanga mabaya dhidi yako na kutunga hila, hawawezi kufanikiwa, 12kwa kuwa utawafanya wakimbie utakapowalenga usoni pao kwa mshale kutoka kwenye upinde wako. 13Ee Bwana, utukuzwe katika nguvu zako, tutaimba na kusifu nguvu zako.

Namba za mistari hufuata tafsiri uliyochagua, na katika sura chache zinaweza kutofautiana kwa mstari mmoja.

Urahisi wa kusoma

Chagua kinachokusaidia. Chaguo lako linahifadhiwa kwenye kifaa hiki.

Ukubwa wa maandishi

Unapendelea mipangilio ya kifaa chako mwenyewe (kukuza, kisoma skrini, hali ya giza)? Inafanya kazi hapa pia.