Ruka hadi kwenye maudhui
Beta

Uzi bado haujatafsiriwa kikamilifu kwa Kiswahili. Kile ambacho bado hakijatafsiriwa kinaonyeshwa kwa Kiingereza.

Zaburi 114

Sura hii ni sehemu ya: Boek V

1Wakati Israeli walipotoka Misri, nyumba ya Yakobo kutoka kwa watu wa lugha ngeni, 2Yuda alifanywa makao matakatifu ya Mungu, Israeli akawa milki yake. 3Bahari ilitazama ikakimbia, Yordani ulirudi nyuma, 4milima ilirukaruka kama kondoo dume, vilima kama wana-kondoo. 5Ee bahari, ni nini kilichokufanya ukakimbia, nawe, ee Yordani, ukarudi nyuma, 6enyi milima mkarukaruka kama kondoo dume, enyi vilima, kama wana-kondoo? 7Ee dunia, tetemeka mbele za Bwana, mbele za Mungu wa Yakobo, 8aliyegeuza mwamba kuwa dimbwi la maji, mwamba mgumu kuwa chemchemi za maji.

Namba za mistari hufuata tafsiri uliyochagua, na katika sura chache zinaweza kutofautiana kwa mstari mmoja.

Urahisi wa kusoma

Chagua kinachokusaidia. Chaguo lako linahifadhiwa kwenye kifaa hiki.

Ukubwa wa maandishi

Unapendelea mipangilio ya kifaa chako mwenyewe (kukuza, kisoma skrini, hali ya giza)? Inafanya kazi hapa pia.