Ruka hadi kwenye maudhui
Beta

Uzi bado haujatafsiriwa kikamilifu kwa Kiswahili. Kile ambacho bado hakijatafsiriwa kinaonyeshwa kwa Kiingereza.

Zaburi 129

Sura hii ni sehemu ya: Boek V

1Wamenionea mno tangu ujana wangu; Israeli na aseme sasa: 2wamenionea mno tangu ujana wangu, lakini bado hawajanishinda. 3Wakulima wamelima mgongo wangu, na kufanya mifereji yao mirefu. 4Lakini Bwana ni mwenye haki; amenifungua toka kamba za waovu. 5Wale wote waichukiao Sayuni na warudishwe nyuma kwa aibu. 6Wawe kama majani juu ya paa, ambayo hunyauka kabla hayajakua; 7kwa hayo mvunaji hawezi kujaza vitanga vyake, wala akusanyaye kujaza mikono yake. 8Wale wapitao karibu na wasiseme, “Baraka ya Bwana iwe juu yako; tunakubariki katika jina la Bwana.”

Namba za mistari hufuata tafsiri uliyochagua, na katika sura chache zinaweza kutofautiana kwa mstari mmoja.

Urahisi wa kusoma

Chagua kinachokusaidia. Chaguo lako linahifadhiwa kwenye kifaa hiki.

Ukubwa wa maandishi

Unapendelea mipangilio ya kifaa chako mwenyewe (kukuza, kisoma skrini, hali ya giza)? Inafanya kazi hapa pia.