Ruka hadi kwenye maudhui
Beta

Uzi bado haujatafsiriwa kikamilifu kwa Kiswahili. Kile ambacho bado hakijatafsiriwa kinaonyeshwa kwa Kiingereza.

Zaburi 95

Sura hii ni sehemu ya: Boek IV

1Njooni, tumwimbie Bwana kwa furaha; tumfanyie kelele za shangwe Mwamba wa wokovu wetu. 2Tuje mbele zake kwa shukrani, tumtukuze kwa vinanda na nyimbo. 3Kwa kuwa Bwana ni Mungu mkuu, mfalme mkuu juu ya miungu yote. 4Mkononi mwake mna vilindi vya dunia, na vilele vya milima ni mali yake. 5Bahari ni yake, kwani ndiye aliifanya, na mikono yake iliumba nchi kavu. 6Njooni, tusujudu, tumwabudu, tupige magoti mbele za Bwana Muumba wetu, 7kwa maana yeye ndiye Mungu wetu, na sisi ni watu wa malisho yake, kondoo chini ya utunzaji wake. Kama mkiisikia sauti yake leo, 8msiifanye mioyo yenu migumu kama mlivyofanya kule Meriba, kama mlivyofanya siku ile kule Masa jangwani, 9ambapo baba zenu walinijaribu na kunipima, ingawa walikuwa wameyaona matendo yangu. 10Kwa miaka arobaini nilikasirikia kizazi kile, nikasema, “Hawa ni taifa ambalo mioyo yao imepotoka, nao hawajazijua njia zangu.” 11Hivyo nikatangaza kwa kiapo katika hasira yangu, “Kamwe hawataingia rahani mwangu.”

Namba za mistari hufuata tafsiri uliyochagua, na katika sura chache zinaweza kutofautiana kwa mstari mmoja.

Urahisi wa kusoma

Chagua kinachokusaidia. Chaguo lako linahifadhiwa kwenye kifaa hiki.

Ukubwa wa maandishi

Unapendelea mipangilio ya kifaa chako mwenyewe (kukuza, kisoma skrini, hali ya giza)? Inafanya kazi hapa pia.