Ruka hadi kwenye maudhui
Beta

Uzi bado haujatafsiriwa kikamilifu kwa Kiswahili. Kile ambacho bado hakijatafsiriwa kinaonyeshwa kwa Kiingereza.

Zaburi 8

Sura hii ni sehemu ya: Boek I

1Ee Bwana, Bwana wetu, tazama jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani mwote! Umeuweka utukufu wako juu ya mbingu. 2Midomoni mwa watoto wachanga na wanyonyao umeamuru sifa, kwa sababu ya watesi wako, kumnyamazisha adui na mlipiza kisasi. 3Nikiziangalia mbingu zako, kazi ya vidole vyako, mwezi na nyota, ulizoziratibisha, 4mwanadamu ni kitu gani hata unamfikiria, binadamu ni nani hata unamjali? 5Umemfanya chini kidogo kuliko viumbe wa mbinguni, ukamvika taji ya utukufu na heshima. 6Umemfanya mtawala juu ya kazi za mikono yako; umeweka vitu vyote chini ya miguu yake. 7Mifugo na makundi yote pia, naam, na wanyama wa kondeni, 8ndege wa angani na samaki wa baharini, naam, kila kiogeleacho katika njia za bahari. 9Ee Bwana, Bwana wetu, tazama jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani mwote!

Namba za mistari hufuata tafsiri uliyochagua, na katika sura chache zinaweza kutofautiana kwa mstari mmoja.

Urahisi wa kusoma

Chagua kinachokusaidia. Chaguo lako linahifadhiwa kwenye kifaa hiki.

Ukubwa wa maandishi

Unapendelea mipangilio ya kifaa chako mwenyewe (kukuza, kisoma skrini, hali ya giza)? Inafanya kazi hapa pia.