1Sifa ni kwa Bwana Mwamba wangu, aifundishaye mikono yangu vita, na vidole vyangu kupigana. 2Yeye ni Mungu wangu wa upendo na boma langu, ngome yangu na mwokozi wangu, ngao yangu ninayemkimbilia, ambaye huwatiisha mataifa chini yangu. 3Ee Bwana, mwanadamu ni nini hata umjali, Binadamu ni nini hata umfikirie? 4Mwanadamu ni kama pumzi, siku zake ni kama kivuli kinachopita. 5Ee Bwana, pasua mbingu zako, ushuke, gusa milima ili itoe moshi. 6Peleka umeme uwatawanye adui, lenga mishale yako uwashinde. 7Nyoosha mkono wako kutoka juu, nikomboe na kuniokoa kutoka maji makuu, kutoka mikononi mwa wageni 8ambao vinywa vyao vimejaa uongo, na mikono yao ya kuume ni midanganyifu. 9Ee Mungu, nitakuimbia wimbo mpya, kwa zeze yenye nyuzi kumi nitakuimbia, 10kwa Yule awapaye wafalme ushindi, ambaye humwokoa Daudi, mtumishi wake kutokana na upanga hatari. 11Nikomboe na uniokoe kutoka mikononi mwa wageni ambao vinywa vyao vimejaa uongo, na mikono yao ya kuume ni midanganyifu. 12Kisha wana wetu wakati wa ujana wao watakuwa kama mimea iliyotunzwa vizuri, binti zetu watakuwa kama nguzo zilizoviringwa kurembesha jumba la kifalme. 13Ghala zetu zitajazwa aina zote za mahitaji. Kondoo zetu watazaa kwa maelfu, kwa makumi ya maelfu katika mashamba yetu; 14maksai wetu watakokota mizigo mizito. Hakutakuwa na kubomoka kuta, hakuna kuchukuliwa mateka, wala kilio cha taabu katika barabara zetu. 15Heri watu ambao hili ni kweli; heri wale ambao Bwana ni Mungu wao.
1Blessed be Yahweh, my rock, who teaches my hands to war, and my fingers to battle: 2my loving kindness, my fortress, my high tower, my deliverer, my shield, and he in whom I take refuge; who subdues my people under me. 3Yahweh, what is man, that you care for him? Or the son of man, that you think of him? 4Man is like a breath. His days are like a shadow that passes away. 5Part your heavens, Yahweh, and come down. Touch the mountains, and they will smoke. 6Throw out lightning, and scatter them. Send out your arrows, and rout them. 7Stretch out your hand from above, rescue me, and deliver me out of great waters, out of the hands of foreigners; 8whose mouths speak deceit, Whose right hand is a right hand of falsehood. 9I will sing a new song to you, God. On a ten-stringed lyre, I will sing praises to you. 10You are he who gives salvation to kings, who rescues David, his servant, from the deadly sword. 11Rescue me, and deliver me out of the hands of foreigners, whose mouths speak deceit, whose right hand is a right hand of falsehood. 12Then our sons will be like well-nurtured plants, our daughters like pillars carved to adorn a palace. 13Our barns are full, filled with all kinds of provision. Our sheep produce thousands and ten thousands in our fields. 14Our oxen will pull heavy loads. There is no breaking in, and no going away, and no outcry in our streets. 15Happy are the people who are in such a situation. Happy are the people whose God is Yahweh.
1Een psalm van David. Gezegend zij de HEERE, mijn Rotssteen, Die mijn handen onderwijst ten strijde, mijn vingeren ten oorlog; 2Mijn Goedertierenheid en mijn Burg, mijn Hoog Vertrek en mijn Bevrijder voor mij, mijn Schild, en op Wien ik mij betrouwe; Die mijn volk aan mij onderwerpt! 3O HEERE! wat is de mens, dat Gij hem kent, het kind des mensen, dat Gij het acht? 4De mens is der ijdelheid gelijk; zijn dagen zijn als een voorbijgaande schaduw. 5Neig Uw hemelen, HEERE! en daal neder; raak de bergen aan, dat zij roken. 6Bliksem bliksem, en verstrooi hen; zend Uw pijlen uit, en verdoe hen. 7Steek Uw handen van de hoogte uit; ontzet mij, en ruk mij uit de grote wateren, uit de hand der vreemden; 8Welker mond leugen spreekt, en hun rechterhand is een rechterhand der valsheid. 9O God! ik zal U een nieuw lied zingen; met de luit en het tiensnarig instrument zal ik U psalmzingen. 10Gij, die den koningen overwinning geeft, Die Zijn knecht David ontzet van het boze zwaard; 11Ontzet mij en red mij van de hand der vreemden, welker mond leugen spreekt, en hun rechterhand is een rechterhand der valsheid; 12Opdat onze zonen zijn als planten, welke groot geworden zijn in hun jeugd; onze dochter als hoekstenen, uitgehouwen naar de gelijkenis van een paleis. 13Dat onze winkelen vol zijnde, den enen voorraad na den anderen uitgeven; dat onze kudden bij duizenden werpen, ja, bij tienduizenden op onze hoeven vermenigvuldigen. 14Dat onze ossen wel geladen zijn; dat geen inbreuk, noch uitval, noch gekrijs zij op onze straten. 15Welgelukzalig is het volk, dien het alzo gaat; welgelukzalig is het volk, wiens God de HEERE is.
Bonyeza Enter ili kuuwekea mstari huu rangi, kuandika maelezo au kuunakili. Vitufe vya mishale vinakupeleka kwenye mstari unaofuata.
Namba za mistari hufuata tafsiri uliyochagua, na katika sura chache zinaweza kutofautiana kwa mstari mmoja.