Ruka hadi kwenye maudhui
Beta

Uzi bado haujatafsiriwa kikamilifu kwa Kiswahili. Kile ambacho bado hakijatafsiriwa kinaonyeshwa kwa Kiingereza.

Zaburi 56

Sura hii ni sehemu ya: Boek II

1Ee Mungu unihurumie, maana watu wananifuatia vikali; mchana kutwa wanazidisha mashambulizi yao. 2Wasingiziaji wangu wananifuatia mchana kutwa, wengi wananishambulia kwa kiburi chao. 3Wakati ninapoogopa, nitakutumaini wewe. 4Katika Mungu, ambaye neno lake ninalisifu, katika Mungu ninatumaini; sitaogopa. Mwanadamu apatikanaye na kufa, atanitenda nini? 5Mchana kutwa wanayageuza maneno yangu, siku zote wanapanga shauri la kunidhuru. 6Wananifanyia hila, wanajificha, wanatazama hatua zangu, wakiwa na shauku ya kuutoa uhai wangu. 7Wasiepuke kwa vyovyote, Ee Mungu, katika hasira yako yaangushe mataifa. 8Andika maombolezo yangu, orodhesha machozi yangu katika gombo lako: je, haya hayapo katika kumbukumbu zako? 9Ndipo adui zangu watarudi nyuma ninapoita msaada. Kwa hili nitajua kwamba Mungu yuko upande wangu. 10Katika Mungu, ambaye neno lake ninalisifu, katika Bwana, ambaye neno lake ninalisifu, 11katika Mungu ninatumaini, sitaogopa. Mwanadamu anaweza kunitenda nini? 12Ee Mungu, nina nadhiri kwako, nitakutolea wewe sadaka zangu za shukrani. 13Kwa kuwa umeniokoa toka kwenye mauti na miguu yangu kwenye kujikwaa, ili niweze kuenenda mbele za Mungu katika nuru ya uzima.

Namba za mistari hufuata tafsiri uliyochagua, na katika sura chache zinaweza kutofautiana kwa mstari mmoja.

Urahisi wa kusoma

Chagua kinachokusaidia. Chaguo lako linahifadhiwa kwenye kifaa hiki.

Ukubwa wa maandishi

Unapendelea mipangilio ya kifaa chako mwenyewe (kukuza, kisoma skrini, hali ya giza)? Inafanya kazi hapa pia.