Ruka hadi kwenye maudhui
Beta

Uzi bado haujatafsiriwa kikamilifu kwa Kiswahili. Kile ambacho bado hakijatafsiriwa kinaonyeshwa kwa Kiingereza.

Zaburi 128

Sura hii ni sehemu ya: Boek V

1Heri ni wale wote wamchao Bwana, waendao katika njia zake. 2Utakula matunda ya kazi yako; baraka na mafanikio vitakuwa vyako. 3Mke wako atakuwa kama mzabibu uzaao ndani ya nyumba yako; wana wako watakuwa kama machipukizi ya mizeituni kuizunguka meza yako. 4Hivyo ndivyo atakavyobarikiwa mtu amchaye Bwana. 5Bwana na akubariki kutoka Sayuni siku zote za maisha yako, na uone mafanikio ya Yerusalemu, 6nawe ujaliwe kuishi uone watoto wa watoto wako. Amani iwe juu ya Israeli.

Namba za mistari hufuata tafsiri uliyochagua, na katika sura chache zinaweza kutofautiana kwa mstari mmoja.

Urahisi wa kusoma

Chagua kinachokusaidia. Chaguo lako linahifadhiwa kwenye kifaa hiki.

Ukubwa wa maandishi

Unapendelea mipangilio ya kifaa chako mwenyewe (kukuza, kisoma skrini, hali ya giza)? Inafanya kazi hapa pia.