Ruka hadi kwenye maudhui
Beta

Uzi bado haujatafsiriwa kikamilifu kwa Kiswahili. Kile ambacho bado hakijatafsiriwa kinaonyeshwa kwa Kiingereza.

Zaburi 36

Sura hii ni sehemu ya: Boek I

1Kuna neno moyoni mwangu kuhusu hali ya dhambi ya mwovu. Hakuna hofu ya Mungu mbele ya macho yake. 2Kwa kuwa machoni pake mwenyewe hujisifu mno hata hawezi kugundua au kuichukia dhambi yake. 3Maneno ya kinywa chake ni maovu na ya udanganyifu, ameacha kuwa mwenye hekima na kutenda mema. 4Hata kitandani mwake hupanga hila mbaya, hujitia katika njia ya dhambi na hakatai lililo baya. 5Upendo wako, Ee Bwana, unafika hadi mbinguni, uaminifu wako hadi kwenye anga. 6Haki yako ni kama milima mikubwa, hukumu zako ni kama kilindi kikuu. Ee Bwana, wewe huwahifadhi mwanadamu na mnyama. 7Upendo wako usiokoma ni wa thamani mno! Watu wakuu na wadogo hujificha uvulini wa mbawa zako. 8Wanajifurahisha katika wingi nyumbani mwako, nawe utawanywesha katika mto wa furaha zako. 9Kuwa pamoja nawe ni kijito cha uzima, katika nuru yako twaona nuru. 10Dumisha upendo wako kwa wale wanaokujua wewe, haki yako kwa wale walio wanyofu wa moyo. 11Mguu wa mwenye kiburi usije dhidi yangu, wala mkono wa mwovu usinifukuze. 12Angalia jinsi watenda mabaya walivyoanguka: wametupwa chini, hawawezi kuinuka!

Namba za mistari hufuata tafsiri uliyochagua, na katika sura chache zinaweza kutofautiana kwa mstari mmoja.

Urahisi wa kusoma

Chagua kinachokusaidia. Chaguo lako linahifadhiwa kwenye kifaa hiki.

Ukubwa wa maandishi

Unapendelea mipangilio ya kifaa chako mwenyewe (kukuza, kisoma skrini, hali ya giza)? Inafanya kazi hapa pia.