1Hakika Mungu ni mwema kwa Israeli, kwa wale ambao mioyo yao ni safi. 2Bali kwangu mimi, miguu yangu ilikuwa karibu kuteleza; nilikuwa karibu mguu wangu kuachia uliposimama. 3Kwa maana niliwaonea wivu wenye kujivuna nilipoona kufanikiwa kwa waovu. 4Wao hawana taabu, miili yao ina afya na nguvu. 5Hawapati shida zinazowataabisha watu wengine, wala hawapati mapigo kama wanadamu wengine. 6Kwa hiyo kiburi ni mkufu wao, wamejivika jeuri. 7Uovu hutoka katika mioyo yao iliyokufa ganzi, majivuno maovu kutoka mioyoni mwao hauna kikomo. 8Hudhihaki na kusema kwa ukorofi, katika majivuno yao wanatishia kutesa. 9Vinywa vyao huweka madai hata kwa mbingu, nazo ndimi zao humiliki duniani. 10Kwa hiyo watu wao huwageukia na kunywa maji tele. 11Wanasema, “Mungu awezaje kujua? Je, Yeye Aliye Juu Sana anayo maarifa?” 12Hivi ndivyo walivyo waovu: siku zote hawajali, wanaongezeka katika utajiri. 13Hakika nimeuweka moyo wangu safi bure, ni bure nimenawa mikono yangu nisiwe na hatia. 14Mchana kutwa nimetaabika, nimeadhibiwa kila asubuhi. 15Kama ningesema, “Nitasema hivi,” ningelikuwa nimewasaliti watoto wako. 16Nilipojaribu kuelewa haya yote, yalikuwa magumu kwangu kuelewa. 17Mpaka nilipoingia patakatifu pa Mungu, ndipo nilipotambua mwisho wao. 18Hakika unawaweka mahali pa utelezi, unawaangusha chini kwa uharibifu. 19Tazama jinsi wanavyoangamizwa ghafula, wanatoweshwa kabisa na vitisho! 20Kama ndoto mtu aamkapo, hivyo wakati uinukapo, Ee Bwana, utawatowesha kama ndoto. 21Wakati moyo wangu ulipohuzunishwa, na roho yangu ilipotiwa uchungu, 22nilikuwa mpumbavu na mjinga, nilikuwa mnyama mkatili mbele yako. 23Hata hivyo niko pamoja nawe siku zote, umenishika mkono wangu wa kuume. 24Unaniongoza kwa shauri lako, hatimaye utaniingiza katika utukufu. 25Nani niliye naye mbinguni ila wewe? Dunia haina chochote ninachokitamani ila wewe. 26Mwili na moyo wangu vyaweza kushindwa, bali Mungu ni nguvu ya moyo wangu na fungu langu milele. 27Wale walio mbali nawe wataangamia, unawaangamiza wote wasio waaminifu kwako. 28Lakini kwangu mimi, ni vyema kuwa karibu na Mungu. Nimemfanya Bwana Mwenyezi kimbilio langu; nami nitayasimulia matendo yako yote.
1Surely God is good to Israel, to those who are pure in heart. 2But as for me, my feet were almost gone. My steps had nearly slipped. 3For I was envious of the arrogant, when I saw the prosperity of the wicked. 4For there are no struggles in their death, but their strength is firm. 5They are free from burdens of men, neither are they plagued like other men. 6Therefore pride is like a chain around their neck. Violence covers them like a garment. 7Their eyes bulge with fat. Their minds pass the limits of conceit. 8They scoff and speak with malice. In arrogance, they threaten oppression. 9They have set their mouth in the heavens. Their tongue walks through the earth. 10Therefore their people return to them, and they drink up waters of abundance. 11They say, “How does God know? Is there knowledge in the Most High?” 12Behold, these are the wicked. Being always at ease, they increase in riches. 13Surely in vain I have cleansed my heart, and washed my hands in innocence, 14For all day long have I been plagued, and punished every morning. 15If I had said, “I will speak thus”; behold, I would have betrayed the generation of your children. 16When I tried to understand this, it was too painful for me; 17Until I entered God’s sanctuary, and considered their latter end. 18Surely you set them in slippery places. You throw them down to destruction. 19How they are suddenly destroyed! They are completely swept away with terrors. 20As a dream when one wakes up, so, Lord, when you awake, you will despise their fantasies. 21For my soul was grieved. I was embittered in my heart. 22I was so senseless and ignorant. I was a brute beast before you. 23Nevertheless, I am continually with you. You have held my right hand. 24You will guide me with your counsel, and afterward receive me to glory. 25Whom do I have in heaven? There is no one on earth whom I desire besides you. 26My flesh and my heart fails, but God is the strength of my heart and my portion forever. 27For, behold, those who are far from you shall perish. You have destroyed all those who are unfaithful to you. 28But it is good for me to come close to God. I have made the Lord Yahweh my refuge, that I may tell of all your works.
1Een psalm van Asaf. Immers is God Israel goed, dengenen, die rein van harte zijn. 2Maar mij aangaande, mijn voeten waren bijna uitgeweken; mijn treden waren bijkans uitgeschoten. 3Want ik was nijdig op de dwazen, ziende der goddelozen vrede. 4Want er zijn geen banden tot hun dood toe, en hun kracht is fris. 5Zij zijn niet in de moeite als andere mensen, en worden met andere mensen niet geplaagd. 6Daarom omringt hen de hovaardij als een keten; het geweld bedekt hen als een gewaad. 7Hun ogen puilen uit van vet; zij gaan de inbeeldingen des harten te boven. 8Zij mergelen de lieden uit, en spreken boselijk van verdrukking; zij spreken uit de hoogte. 9Zij zetten hun mond tegen den hemel, en hun tong wandelt op de aarde. 10Daarom keert zich Zijn volk hiertoe, als hun wateren eens vollen bekers worden uitgedrukt, 11Dat zij zeggen: Hoe zou het God weten, en zou er wetenschap zijn bij den Allerhoogste? 12Ziet, dezen zijn goddeloos; nochtans hebben zij rust in de wereld; zij vermenigvuldigen het vermogen. 13Immers heb ik tevergeefs mijn hart gezuiverd, en mijn handen in onschuld gewassen. 14Dewijl ik den gansen dag geplaagd ben, en mijn straffing is er alle morgens. 15Indien ik zou zeggen: Ik zal ook alzo spreken; ziet, zo zou ik trouweloos zijn aan het geslacht Uwer kinderen. 16Nochtans heb ik gedacht om dit te mogen verstaan; maar het was moeite in mijn ogen; 17Totdat ik in Gods heiligdommen inging, en op hun einde merkte. 18Immers zet Gij hen op gladde plaatsen; Gij doet hen vallen in verwoestingen. 19Hoe worden zij als in een ogenblik tot verwoesting, nemen een einde, worden te niet van verschrikkingen! 20Als een droom na het ontwaken! Als Gij opwaakt, o Heere, dan zult Gij hun beeld verachten. 21Als mijn hart opgezwollen was, en ik in mijn nieren geprikkeld werd, 22Toen was ik onvernuftig, en wist niets; ik was een groot beest bij U. 23Ik zal dan geduriglijk bij U zijn; Gij hebt mijn rechterhand gevat; 24Gij zult mij leiden door Uw raad; en daarna zult Gij mij in heerlijkheid opnemen. 25Wien heb ik nevens U in den hemel? Nevens U lust mij ook niets op de aarde! 26Bezwijkt mijn vlees en mijn hart, zo is God de Rotssteen mijns harten, en mijn Deel in eeuwigheid. 27Want ziet, die verre van U zijn, zullen vergaan; Gij roeit uit, al wie van U afhoereert. 28Maar mij aangaande, het is mij goed nabij God te wezen; ik zet mijn betrouwen op den Heere HEERE, om al Uw werken te vertellen.
Bonyeza Enter ili kuuwekea mstari huu rangi, kuandika maelezo au kuunakili. Vitufe vya mishale vinakupeleka kwenye mstari unaofuata.
Namba za mistari hufuata tafsiri uliyochagua, na katika sura chache zinaweza kutofautiana kwa mstari mmoja.