Ruka hadi kwenye maudhui
Beta

Uzi bado haujatafsiriwa kikamilifu kwa Kiswahili. Kile ambacho bado hakijatafsiriwa kinaonyeshwa kwa Kiingereza.

Zaburi 29

Sura hii ni sehemu ya: Boek I

1Mpeni Bwana, enyi mashujaa, mpeni Bwana utukufu na nguvu. 2Mpeni Bwana utukufu unaostahili jina lake; mwabuduni Bwana katika uzuri wa utakatifu wake. 3Sauti ya Bwana iko juu ya maji; Mungu wa utukufu hupiga radi, Bwana hupiga radi juu ya maji makuu. 4Sauti ya Bwana ina nguvu; sauti ya Bwana ni tukufu. 5Sauti ya Bwana huvunja mierezi; Bwana huvunja vipande vipande mierezi ya Lebanoni. 6Hufanya Lebanoni irukaruke kama ndama, Sirioni urukaruke kama mwana nyati. 7Sauti ya Bwana hupiga kwa miali ya umeme wa radi. 8Sauti ya Bwana hutikisa jangwa; Bwana hutikisa Jangwa la Kadeshi. 9Sauti ya Bwana huzalisha ayala, na huuacha msitu wazi. Hekaluni mwake wote wasema, “Utukufu!” 10Bwana huketi akiwa ametawazwa juu ya gharika; Bwana ametawazwa kuwa Mfalme milele. 11Bwana huwapa watu wake nguvu; Bwana huwabariki watu wake kwa kuwapa amani.

Namba za mistari hufuata tafsiri uliyochagua, na katika sura chache zinaweza kutofautiana kwa mstari mmoja.

Urahisi wa kusoma

Chagua kinachokusaidia. Chaguo lako linahifadhiwa kwenye kifaa hiki.

Ukubwa wa maandishi

Unapendelea mipangilio ya kifaa chako mwenyewe (kukuza, kisoma skrini, hali ya giza)? Inafanya kazi hapa pia.