Ruka hadi kwenye maudhui
Beta

Uzi bado haujatafsiriwa kikamilifu kwa Kiswahili. Kile ambacho bado hakijatafsiriwa kinaonyeshwa kwa Kiingereza.

Zaburi 122

Sura hii ni sehemu ya: Boek V

1Nilishangilia pamoja na wale walioniambia, “Twende nyumbani ya Bwana.” 2Ee Yerusalemu, miguu yetu imesimama malangoni mwako. 3Yerusalemu imejengwa vyema kama mji ambao umeshikamanishwa pamoja. 4Huko ndiko makabila hukwea, makabila ya Bwana, kulisifu jina la Bwana kulingana na maagizo waliopewa Israeli. 5Huko viti vya enzi vya hukumu hukaa, viti vya enzi vya nyumba ya Daudi. 6Omba kwa ajili ya amani ya Yerusalemu: “Wote wakupendao na wawe salama. 7Amani na iwepo ndani ya kuta zako na usalama ndani ya ngome zako.” 8Kwa ajili ya ndugu zangu na marafiki, nitasema, “Amani iwe ndani yako.” 9Kwa ajili ya nyumba ya Bwana Mungu wetu, nitatafuta mafanikio yako.

Namba za mistari hufuata tafsiri uliyochagua, na katika sura chache zinaweza kutofautiana kwa mstari mmoja.

Urahisi wa kusoma

Chagua kinachokusaidia. Chaguo lako linahifadhiwa kwenye kifaa hiki.

Ukubwa wa maandishi

Unapendelea mipangilio ya kifaa chako mwenyewe (kukuza, kisoma skrini, hali ya giza)? Inafanya kazi hapa pia.