Ruka hadi kwenye maudhui
Beta

Uzi bado haujatafsiriwa kikamilifu kwa Kiswahili. Kile ambacho bado hakijatafsiriwa kinaonyeshwa kwa Kiingereza.

Zaburi 121

Sura hii ni sehemu ya: Boek V

1Nayainua macho yangu nitazame vilima, msaada wangu utatoka wapi? 2Msaada wangu hutoka kwa Bwana, Muumba wa mbingu na dunia. 3Hatauacha mguu wako uteleze, yeye akulindaye hatasinzia, 4hakika, yeye alindaye Israeli hatasinzia wala hatalala usingizi. 5Bwana anakulinda, Bwana ni uvuli wako mkono wako wa kuume, 6jua halitakudhuru mchana, wala mwezi wakati wa usiku. 7Bwana atakukinga na madhara yote, atayalinda maisha yako, 8Bwana atakulinda unapoingia na unapotoka, tangu sasa na hata milele.

Namba za mistari hufuata tafsiri uliyochagua, na katika sura chache zinaweza kutofautiana kwa mstari mmoja.

Urahisi wa kusoma

Chagua kinachokusaidia. Chaguo lako linahifadhiwa kwenye kifaa hiki.

Ukubwa wa maandishi

Unapendelea mipangilio ya kifaa chako mwenyewe (kukuza, kisoma skrini, hali ya giza)? Inafanya kazi hapa pia.