Ruka hadi kwenye maudhui
Beta

Uzi bado haujatafsiriwa kikamilifu kwa Kiswahili. Kile ambacho bado hakijatafsiriwa kinaonyeshwa kwa Kiingereza.

Zaburi 87

Sura hii ni sehemu ya: Boek III

1Ameuweka msingi wake katika mlima mtakatifu; 2Bwana anayapenda malango ya Sayuni kuliko makao yote ya Yakobo. 3Mambo matukufu yanasemwa juu yako, ee mji wa Mungu: 4“Nitaweka kumbukumbu ya Rahabu na Babeli miongoni mwa wale wanaonikubali mimi: Ufilisti pia na Tiro, pamoja na Kushi, nami nitasema, ‘Huyu alizaliwa Sayuni.’” 5Kuhusu Sayuni itasemwa hivi, “Huyu na yule walizaliwa humo, naye Aliye Juu Sana mwenyewe atamwimarisha.” 6Bwana ataandika katika orodha ya mataifa: “Huyu alizaliwa Sayuni.” 7Watakapokuwa wanapiga vinanda wataimba, “Chemchemi zangu zote ziko kwako.”

Namba za mistari hufuata tafsiri uliyochagua, na katika sura chache zinaweza kutofautiana kwa mstari mmoja.

Urahisi wa kusoma

Chagua kinachokusaidia. Chaguo lako linahifadhiwa kwenye kifaa hiki.

Ukubwa wa maandishi

Unapendelea mipangilio ya kifaa chako mwenyewe (kukuza, kisoma skrini, hali ya giza)? Inafanya kazi hapa pia.