Ruka hadi kwenye maudhui
Beta

Uzi bado haujatafsiriwa kikamilifu kwa Kiswahili. Kile ambacho bado hakijatafsiriwa kinaonyeshwa kwa Kiingereza.

Zaburi 82

Sura hii ni sehemu ya: Boek III

1Mungu anaongoza kusanyiko kuu, anatoa hukumu miongoni mwa “miungu”: 2“Hata lini utaendelea kuwatetea wasio haki na kuonyesha upendeleo kwa waovu? 3Teteeni wanyonge na yatima, tunzeni haki za maskini na walioonewa. 4Mwokoeni mnyonge na mhitaji, wakomboeni kutoka mkononi mwa mwovu. 5“Hawajui lolote, hawaelewi lolote. Wanatembea gizani; misingi yote ya dunia imetikisika. 6“Nilisema, ‘Ninyi ni “miungu”; ninyi nyote ni wana wa Aliye Juu Sana.’ 7Lakini mtakufa kama wanadamu wa kawaida; mtaanguka kama mtawala mwingine yeyote.” 8Ee Mungu, inuka uihukumu nchi, kwa kuwa mataifa yote ni urithi wako.

Namba za mistari hufuata tafsiri uliyochagua, na katika sura chache zinaweza kutofautiana kwa mstari mmoja.

Urahisi wa kusoma

Chagua kinachokusaidia. Chaguo lako linahifadhiwa kwenye kifaa hiki.

Ukubwa wa maandishi

Unapendelea mipangilio ya kifaa chako mwenyewe (kukuza, kisoma skrini, hali ya giza)? Inafanya kazi hapa pia.