Ruka hadi kwenye maudhui
Beta

Uzi bado haujatafsiriwa kikamilifu kwa Kiswahili. Kile ambacho bado hakijatafsiriwa kinaonyeshwa kwa Kiingereza.

Zaburi 132

Sura hii ni sehemu ya: Boek V

1Ee Bwana, mkumbuke Daudi na taabu zote alizozistahimili. 2Aliapa kiapo kwa Bwana na akaweka nadhiri kwa Yule Mwenye Nguvu wa Yakobo: 3“Sitaingia nyumbani mwangu au kwenda kitandani mwangu: 4sitaruhusu usingizi katika macho yangu, wala kope zangu kusinzia, 5mpaka nitakapompatia Bwana mahali, makao kwa ajili ya Yule Mwenye Nguvu wa Yakobo.” 6Tulisikia habari hii huko Efrathi, tulikutana nayo katika mashamba ya Yaara: 7“Twendeni kwenye makao yake, na tuabudu kwenye kiti cha kuwekea miguu yake; 8inuka, Ee Bwana, uje mahali pako pa kupumzikia, wewe na Sanduku la nguvu zako. 9Makuhani wako na wavikwe haki, watakatifu wako na waimbe kwa furaha.” 10Kwa ajili ya Daudi mtumishi wako, usimkatae mpakwa mafuta wako. 11Bwana alimwapia Daudi kiapo, kiapo cha uhakika ambacho hatakitangua: “Nitamweka mmoja wa wazao wako mwenyewe katika kiti chako cha enzi, 12kama wanao watashika Agano langu na sheria ninazowafundisha, ndipo wana wao watarithi kiti chako cha enzi milele na milele.” 13Kwa maana Bwana ameichagua Sayuni, amepaonea shauku pawe maskani yake: 14“Hapa ni mahali pangu pa kupumzika milele na milele; hapa ndipo nitakapoketi nikitawala, kwa sababu nimepaonea shauku: 15Nitambariki kwa kumpa mahitaji tele: nitashibisha maskini wake kwa chakula. 16Nitawavika makuhani wake wokovu, nao watakatifu wake watadumu wakiimba kwa furaha. 17“Hapa nitamchipushia Daudi pembe, na kuweka taa kwa ajili ya masiya wangu. 18Adui zake nitawavika aibu, bali taji kichwani pake itangʼaa sana.”

Namba za mistari hufuata tafsiri uliyochagua, na katika sura chache zinaweza kutofautiana kwa mstari mmoja.

Urahisi wa kusoma

Chagua kinachokusaidia. Chaguo lako linahifadhiwa kwenye kifaa hiki.

Ukubwa wa maandishi

Unapendelea mipangilio ya kifaa chako mwenyewe (kukuza, kisoma skrini, hali ya giza)? Inafanya kazi hapa pia.