1Mwanangu, kama umekuwa mdhamini wa jirani yako, ikiwa umeshika mikono kwa kuweka ahadi kwa ajili ya mwingine, 2kama umetegwa na ulichosema, umenaswa kwa maneno ya kinywa chako, 3basi fanya hivi mwanangu, ili ujiweke huru, kwa kuwa umeanguka mikononi mwa jirani yako: Nenda ukajinyenyekeshe kwake; msihi jirani yako! 4Usiruhusu usingizi machoni pako, usiruhusu kope zako zisinzie. 5Jiweke huru, kama swala mkononi mwa mwindaji, kama ndege kutoka kwenye mtego wa mwindaji. 6Ewe mvivu, mwendee mchwa; zitafakari njia zake ukapate hekima! 7Kwa maana yeye hana msimamizi, wala mwangalizi, au mtawala, 8lakini hujiwekea akiba wakati wa kiangazi na hukusanya chakula chake wakati wa mavuno. 9Ewe mvivu, utalala hata lini? Utaamka lini kutoka usingizi wako? 10Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo, bado kukunja mikono kidogo upate kupumzika: 11hivyo umaskini utakuja juu yako kama mnyangʼanyi, na kupungukiwa kutakujia kama mtu mwenye silaha. 12Mtu mbaya sana na mlaghai, ambaye huzungukazunguka na maneno ya upotovu, 13ambaye anakonyeza kwa jicho lake, anayetoa ishara kwa miguu yake na kuashiria kwa vidole vyake, 14ambaye hupanga ubaya kwa udanganyifu moyoni mwake: daima huchochea fitina. 15Kwa hiyo maafa yatamkumba ghafula; ataangamizwa mara, pasipo msaada. 16Kuna vitu sita anavyovichukia Bwana, naam, viko saba vilivyo chukizo kwake: 17macho ya kiburi, ulimi udanganyao, mikono imwagayo damu isiyo na hatia, 18moyo uwazao mipango miovu, miguu iliyo myepesi kukimbilia uovu, 19shahidi wa uongo ambaye humwaga uongo, na mtu ambaye huchochea fitina kati ya ndugu. 20Mwanangu, zishike amri za baba yako, wala usiyaache mafundisho ya mama yako. 21Yafunge katika moyo wako daima, yakaze kuizunguka shingo yako. 22Wakati utembeapo, yatakuongoza; wakati ulalapo, yatakulinda; wakati uamkapo, yatazungumza nawe. 23Kwa maana amri hizi ni taa, mafundisho haya ni mwanga na maonyo ya maadili ni njia ya uzima, 24yakikulinda na mwanamke aliyepotoka, kutokana na maneno laini ya mwanamke aliyepotoka. 25Moyo wako usitamani uzuri wake wala macho yake yasikuteke, 26kwa maana kahaba atakufanya uwe maskini, hata ukose kipande cha mkate, naye mwanamke mzinzi huwinda maisha yako hasa. 27Je, mtu aweza kuchotea moto kwenye paja lake bila nguo zake kuungua? 28Je, mtu aweza kutembea juu ya makaa ya moto yanayowaka bila miguu yake kuungua? 29Ndivyo alivyo mtu alalaye na mke wa mwanaume mwingine; hakuna yeyote amgusaye huyo mwanamke ambaye hataadhibiwa. 30Watu hawamdharau mwizi kama akiiba kukidhi njaa yake wakati ana njaa. 31Pamoja na hayo, kama akikamatwa, lazima alipe mara saba, ingawa inamgharimu utajiri wote wa nyumba yake. 32Lakini mwanaume aziniye na mwanamke hana akili kabisa; yeyote afanyaye hivyo hujiangamiza mwenyewe. 33Mapigo na aibu ni fungu lake na aibu yake haitafutika kamwe; 34kwa maana wivu huamsha ghadhabu ya mume, naye hataonyesha huruma alipizapo kisasi. 35Hatakubali fidia yoyote; atakataa malipo, hata yakiwa makubwa kiasi gani.
1My son, if you have become collateral for your neighbor, if you have struck your hands in pledge for a stranger; 2You are trapped by the words of your mouth. You are ensnared with the words of your mouth. 3Do this now, my son, and deliver yourself, since you have come into the hand of your neighbor. Go, humble yourself. Press your plea with your neighbor. 4Give no sleep to your eyes, nor slumber to your eyelids. 5Free yourself, like a gazelle from the hand of the hunter, like a bird from the snare of the fowler. 6Go to the ant, you sluggard. Consider her ways, and be wise; 7which having no chief, overseer, or ruler, 8provides her bread in the summer, and gathers her food in the harvest. 9How long will you sleep, sluggard? When will you arise out of your sleep? 10A little sleep, a little slumber, a little folding of the hands to sleep: 11so your poverty will come as a robber, and your scarcity as an armed man. 12A worthless person, a man of iniquity, is he who walks with a perverse mouth; 13who winks with his eyes, who signals with his feet, who motions with his fingers; 14in whose heart is perverseness, who devises evil continually, who always sows discord. 15Therefore his calamity will come suddenly. He will be broken suddenly, and that without remedy. 16There are six things which Yahweh hates; yes, seven which are an abomination to him: 17haughty eyes, a lying tongue, hands that shed innocent blood; 18a heart that devises wicked schemes, feet that are swift in running to mischief, 19a false witness who utters lies, and he who sows discord among brothers. 20My son, keep your father’s commandment, and don’t forsake your mother’s teaching. 21Bind them continually on your heart. Tie them around your neck. 22When you walk, it will lead you. When you sleep, it will watch over you. When you awake, it will talk with you. 23For the commandment is a lamp, and the law is light. Reproofs of instruction are the way of life, 24to keep you from the immoral woman, from the flattery of the wayward wife’s tongue. 25Don’t lust after her beauty in your heart, neither let her captivate you with her eyelids. 26For a prostitute reduces you to a piece of bread. The adulteress hunts for your precious life. 27Can a man scoop fire into his lap, and his clothes not be burned? 28Or can one walk on hot coals, and his feet not be scorched? 29So is he who goes in to his neighbor’s wife. Whoever touches her will not be unpunished. 30Men don’t despise a thief, if he steals to satisfy himself when he is hungry: 31but if he is found, he shall restore seven times. He shall give all the wealth of his house. 32He who commits adultery with a woman is void of understanding. He who does it destroys his own soul. 33He will get wounds and dishonor. His reproach will not be wiped away. 34For jealousy arouses the fury of the husband. He won’t spare in the day of vengeance. 35He won’t regard any ransom, neither will he rest content, though you give many gifts.
1Mijn zoon! zo gij voor uw naaste borg geworden zijt, voor een vreemde uw hand toegeklapt hebt; 2Gij zijt verstrikt met de redenen uws monds; gij zijt gevangen met de redenen uws monds. 3Doe nu dit, mijn zoon! en red u, dewijl gij in de hand uws naasten gekomen zijt; ga, onderwerp uzelven, en sterk uw naaste. 4Laat uw ogen geen slaap toe, noch uw oogleden sluimering. 5Red u, als een ree uit de hand des jagers, en als een vogel uit de hand des vogelvangers. 6Ga tot de mier, gij luiaard! zie haar wegen, en word wijs; 7Dewelke, geen overste, ambtman noch heerser hebbende, 8Haar brood bereidt in den zomer, haar spijs vergadert in den oogst. 9Hoe lang zult gij, luiaard, nederliggen? Wanneer zult gij van uw slaap opstaan? 10Een weinig slapens, een weinig sluimerens, een weinig handvouwens, al nederliggende; 11Zo zal uw armoede u overkomen als een wandelaar, en uw gebrek als een gewapend man. 12Een Belialsmens, een ondeugdzaam man gaat met verkeerdheid des monds om; 13Wenkt met zijn ogen, spreekt met zijn voeten, leert met zijn vingeren; 14In zijn hart zijn verkeerdheden, hij smeedt te aller tijd kwaad; hij werpt twisten in. 15Daarom zal zijn verderf haastelijk komen; hij zal schielijk verbroken worden, dat er geen genezen aan zij. 16Deze zes haat de HEERE; ja, zeven zijn Zijn ziel een gruwel: 17Hoge ogen, een valse tong, en handen, die onschuldig bloed vergieten; 18Een hart, dat ondeugdzame gedachten smeedt; voeten, die zich haasten, om tot kwaad te lopen; 19Een vals getuige, die leugenen blaast; en die tussen broederen krakelen inwerpt. 20Mijn zoon, bewaar het gebod uws vaders, en verlaat de wet uwer moeder niet. 21Bind ze steeds aan uw hart, hecht ze aan uw hals. 22Als gij wandelt, zal dat u geleiden; als gij nederligt, zal het over u de wacht houden; als gij wakker wordt, zal hetzelve met u spreken. 23Want het gebod is een lamp, en de wet is een licht, en de bestraffingen der tucht zijn de weg des levens; 24Om u te bewaren voor de kwade vrouw, voor het gevlei der vreemde tong. 25Begeer haar schoonheid niet in uw hart, en laat ze u niet vangen met haar oogleden. 26Want door een vrouw, die een hoer is, komt men tot een stuk broods; en eens mans huisvrouw jaagt de kostelijke ziel. 27Zal iemand vuur in zijn boezem nemen, dat zijn klederen niet verbrand worden? 28Zal iemand op kolen gaan, dat zijn voeten niet branden? 29Alzo die tot zijns naasten huisvrouw ingaat; al wie haar aanroert, zal niet onschuldig gehouden worden. 30Men doet een dief geen verachting aan, als hij steelt om zijn ziel te vullen, dewijl hij honger heeft; 31En gevonden zijnde, vergeldt hij het zevenvoudig; hij geeft al het goed van zijn huis. 32Maar die met een vrouw overspel doet, is verstandeloos; hij verderft zijn ziel, die dat doet; 33Plage en schande zal hij vinden, en zijn smaad zal niet uitgewist worden. 34Want jaloersheid is een grimmigheid des mans; en in den dag der wraak zal hij niet verschonen. 35Hij zal geen verzoening aannemen; en hij zal niet bewilligen, ofschoon gij het geschenk vergroot.
Bonyeza Enter ili kuuwekea mstari huu rangi, kuandika maelezo au kuunakili. Vitufe vya mishale vinakupeleka kwenye mstari unaofuata.
Namba za mistari hufuata tafsiri uliyochagua, na katika sura chache zinaweza kutofautiana kwa mstari mmoja.