1Mtu mwovu hukimbia ingawa hakuna yeyote anayemfukuza, bali wenye haki ni wajasiri kama simba. 2Wakati nchi inapokuwa na uasi, inakuwa na viongozi wengi, bali mwenye ufahamu na maarifa hudumisha utaratibu. 3Mtu maskini amwoneaye yeye aliye maskini zaidi ni kama mvua ya dhoruba isiyosaza mazao. 4Wale waiachao sheria huwasifu waovu, bali wale waishikao sheria huwapinga. 5Watu wabaya hawaelewi haki, bali wale wamtafutao Bwana wanaielewa kikamilifu. 6Afadhali maskini ambaye mwenendo wake hauna lawama kuliko tajiri ambaye njia zake ni potovu. 7Yeye ashikaye sheria ni mwana mwenye ufahamu, bali rafiki wa walafi humwaibisha baba yake. 8Yeye aongezaye utajiri wake kwa riba kubwa mno hukusanya kwa ajili ya mwingine, ambaye atawahurumia maskini. 9Kama mtu yeyote akikataa kusikia sheria, hata maombi yake ni chukizo. 10Yeye ambaye humwongoza mwenye haki kwenye mapito mabaya, ataanguka kwenye mtego wake mwenyewe, bali wasio na lawama watapokea urithi mwema. 11Mtu tajiri anaweza kuwa na hekima machoni pake mwenyewe, bali mtu maskini mwenye ufahamu atamfichua. 12Mwenye haki ashindapo, kuna furaha kubwa, bali waovu watawalapo, watu hujificha. 13Yeye afichaye dhambi zake hatafanikiwa, bali yeyote aziungamaye na kuziacha hupata rehema. 14Amebarikiwa mtu ambaye siku zote humcha Bwana, bali yeye afanyaye moyo wake kuwa mgumu huangukia kwenye taabu. 15Kama simba angurumaye au dubu ashambuliaye, ndivyo alivyo mtu mwovu atawalaye wanyonge. 16Mtawala dhalimu hana akili, bali yeye achukiaye mapato ya udhalimu atafurahia maisha marefu. 17Mtu mwenye kusumbuliwa na hatia ya kuua atakuwa mtoro mpaka kufa; mtu yeyote na asimsaidie. 18Yeye ambaye mwenendo wake hauna lawama hulindwa salama, bali yeye ambaye njia zake ni potovu ataanguka ghafula. 19Yeye alimaye shamba lake atakuwa na chakula tele, bali yule afuataye mambo ya upuzi atakuwa na umaskini wa kumtosha. 20Mtu mwaminifu atabarikiwa sana, bali yeye atamaniye kupata utajiri kwa haraka hataacha kuadhibiwa. 21Kuonyesha upendeleo si vizuri, hata hivyo mtu atafanya kosa kwa kipande cha mkate. 22Mtu mchoyo ana tamaa ya kupata utajiri, naye hana habari kuwa umaskini unamngojea. 23Yeye amkemeaye mtu mwishoni hupata kibali zaidi, kuliko mwenye maneno ya kusifu isivyostahili. 24Yeye amwibiaye babaye au mamaye na kusema, “Si kosa,” yeye ni mwenzi wa yule aharibuye. 25Mtu mwenye tamaa huchochea fitina, bali yule amtegemeaye Bwana atafanikiwa. 26Yeye ajitumainiaye mwenyewe ni mpumbavu, bali yeye atembeaye katika hekima hulindwa salama. 27Yeye ampaye maskini hatapungukiwa na kitu chochote, bali yeye awafumbiaye maskini macho hupata laana nyingi. 28Wakati waovu watawalapo, watu huenda mafichoni, bali waovu wanapoangamia, wenye haki hufanikiwa.
1The wicked flee when no one pursues; but the righteous are as bold as a lion. 2In rebellion, a land has many rulers, but order is maintained by a man of understanding and knowledge. 3A needy man who oppresses the poor is like a driving rain which leaves no crops. 4Those who forsake the law praise the wicked; but those who keep the law contend with them. 5Evil men don’t understand justice; but those who seek Yahweh understand it fully. 6Better is the poor who walks in his integrity, than he who is perverse in his ways, and he is rich. 7Whoever keeps the law is a wise son; but he who is a companion of gluttons shames his father. 8He who increases his wealth by excessive interest gathers it for one who has pity on the poor. 9He who turns away his ear from hearing the law, even his prayer is an abomination. 10Whoever causes the upright to go astray in an evil way, he will fall into his own trap; but the blameless will inherit good. 11The rich man is wise in his own eyes; but the poor who has understanding sees through him. 12When the righteous triumph, there is great glory; but when the wicked rise, men hide themselves. 13He who conceals his sins doesn’t prosper, but whoever confesses and renounces them finds mercy. 14Blessed is the man who always fears; but one who hardens his heart falls into trouble. 15As a roaring lion or a charging bear, so is a wicked ruler over helpless people. 16A tyrannical ruler lacks judgment. One who hates ill-gotten gain will have long days. 17A man who is tormented by life blood will be a fugitive until death; no one will support him. 18Whoever walks blamelessly is kept safe; but one with perverse ways will fall suddenly. 19One who works his land will have an abundance of food; but one who chases fantasies will have his fill of poverty. 20A faithful man is rich with blessings; but one who is eager to be rich will not go unpunished. 21To show partiality is not good; yet a man will do wrong for a piece of bread. 22A stingy man hurries after riches, and doesn’t know that poverty waits for him. 23One who rebukes a man will afterward find more favor than one who flatters with the tongue. 24Whoever robs his father or his mother, and says, “It’s not wrong.” He is a partner with a destroyer. 25One who is greedy stirs up strife; but one who trusts in Yahweh will prosper. 26One who trusts in himself is a fool; but one who walks in wisdom is kept safe. 27One who gives to the poor has no lack; but one who closes his eyes will have many curses. 28When the wicked rise, men hide themselves; but when they perish, the righteous thrive.
1De goddelozen vlieden, waar geen vervolger is; maar elk rechtvaardige is moedig, als een jonge leeuw. 2Om de overtreding des lands zijn deszelfs vorsten vele; maar om verstandige en wetende mensen zal insgelijks verlenging wezen. 3Een arm man, die de geringen verdrukt, is een wegvagende regen, zodat er geen brood zij. 4Die de wet verlaten, prijzen de goddelozen; maar die de wet bewaren, mengen zich in strijd tegen hen. 5De kwade lieden verstaan het recht niet; maar die den HEERE zoeken, verstaan alles. 6De arme, wandelende in zijn oprechtheid, is beter, dan die verkeerd is van wegen, al is hij rijk. 7Die de wet bewaart, is een verstandig zoon; maar die der vraten metgezel is, beschaamt zijn vader. 8Die zijn goed vermeerdert met woeker en met overwinst, vergadert dat voor dengene, die zich des armen ontfermt. 9Die zijn oor afwendt van de wet te horen, diens gebed zelfs zal een gruwel zijn. 10Die de oprechten doet dwalen op een kwaden weg, zal zelf in zijn gracht vallen; maar de vromen zullen het goede beerven. 11Een rijk man is wijs in zijn ogen; maar de arme, die verstandig is, doorzoekt hem. 12Als de rechtvaardigen opspringen van vreugde, is er grote heerlijkheid; maar als de goddelozen opkomen, wordt de mens nauw gezocht. 13Die zijn overtredingen bedekt, zal niet voorspoedig zijn; maar die ze bekent en laat, zal barmhartigheid verkrijgen. 14Welgelukzalig is de mens, die geduriglijk vreest; maar die zijn hart verhardt, zal in het kwaad vallen. 15De goddeloze, heersende over een arm volk, is een brullende leeuw, en een beer, die ginds en weder loopt. 16Een vorst, die van alle verstand gebrek heeft, is ook veelvoudig in verdrukkingen; maar die de gierigheid haat, zal de dagen verlengen. 17Een mens, gedrukt om het bloed ener ziel, zal naar den kuil toevlieden; men ondersteune hem niet! 18Die oprecht wandelt, zal behouden worden; maar die zich verkeerdelijk gedraagt in twee wegen, zal in den enen vallen. 19Die zijn land bouwt, zal met brood verzadigd worden; maar die ijdele mensen volgt, zal met armoede verzadigd worden. 20Een gans getrouw man zal veelvoudig zijn in zegeningen; maar die haastig is, om rijk te worden, zal niet onschuldig wezen. 21De aangezichten te kennen, is niet goed; want een man zal om een stuk broods overtreden. 22Die zich haast naar goed, is een man van een boos oog; maar hij weet niet, dat het gebrek hem overkomen zal. 23Die een mens bestraft, zal achterna gunst vinden, meer dan die met de tong vleit. 24Wie zijn vader of zijn moeder berooft, en zegt: Het is geen overtreding; die is des verdervenden mans gezel. 25Die grootmoedig is, verwekt gekijf; maar die op den HEERE vertrouwt, zal vet worden. 26Die op zijn hart vertrouwt, die is een zot; maar die in wijsheid wandelt, die zal ontkomen. 27Die den armen geeft, zal geen gebrek hebben; maar die zijn ogen verbergt, zal veel vervloekt worden. 28Als de goddelozen opkomen, verbergt zich de mens; maar als zij omkomen, vermenigvuldigen de rechtvaardigen.
Bonyeza Enter ili kuuwekea mstari huu rangi, kuandika maelezo au kuunakili. Vitufe vya mishale vinakupeleka kwenye mstari unaofuata.
Namba za mistari hufuata tafsiri uliyochagua, na katika sura chache zinaweza kutofautiana kwa mstari mmoja.