1Mithali za Solomoni: Mwana mwenye hekima huleta furaha kwa baba yake, lakini mwana mpumbavu huleta huzuni kwa mama yake. 2Hazina zilizopatikana kwa njia mbaya hazifai, lakini uadilifu huokoa kutoka mautini. 3Bwana hawaachi waadilifu kukaa njaa, lakini hupinga tamaa ya mtu mwovu. 4Mikono mivivu hufanya mtu kuwa maskini lakini mikono yenye bidii huleta utajiri. 5Yeye akusanyaye mazao wakati wa kiangazi ni mwana mwenye hekima, lakini yeye alalaye wakati wa mavuno ni mwana mwenye kuaibisha. 6Baraka huwa taji kichwani mwa mwenye haki, lakini jeuri hufunika kinywa cha mwovu. 7Kumbukumbu ya mwenye haki itakuwa baraka, lakini jina la mwovu litaoza. 8Mwenye hekima moyoni hupokea maagizo, lakini mpumbavu apayukaye huangamia. 9Mtu mwadilifu hutembea salama, lakini mtu aendaye katika njia zilizopotoka atagunduliwa. 10Yeye akonyezaye kwa nia mbaya husababisha huzuni, naye mpumbavu apayukaye huangamia. 11Kinywa cha mwenye haki ni chemchemi ya uzima, lakini jeuri hufunika kinywa cha mwovu. 12Chuki huchochea faraka, lakini upendo husitiri mabaya yote. 13Hekima hupatikana katika midomo ya wenye kupambanua, lakini fimbo ni kwa ajili ya mgongo wake asiye na ufahamu. 14Wenye hekima huhifadhi maarifa, bali kinywa cha mpumbavu hualika maangamizi. 15Mali ya tajiri ni mji wake wenye ngome, bali ufukara ni maangamizi ya maskini. 16Ujira wa wenye haki huwaletea uzima, lakini mapato ya waovu huwaletea adhabu. 17Anayekubali kuadibishwa yuko katika njia ya uzima, lakini yeyote anayepuuza maonyo hupotosha wengine. 18Yeye afichaye chuki yake ana midomo ya uongo, na yeyote anayeeneza uchonganishi ni mpumbavu. 19Wakati maneno ni mengi, dhambi haikosekani, lakini yeye ambaye huzuia ulimi wake ni mwenye busara. 20Ulimi wa mwenye haki ni fedha iliyo bora, bali moyo wa mwovu una thamani ndogo. 21Midomo ya mwenye haki hulisha wengi, lakini wapumbavu hufa kwa kukosa ufahamu. 22Baraka ya Bwana hutajirisha, wala haichanganyi huzuni. 23Mpumbavu hufurahia tabia mbaya, lakini mtu mwenye ufahamu hupendezwa na hekima. 24Kile anachoogopa mwovu ndicho kitakachompata; kile anachoonea shauku mwenye haki atapewa. 25Tufani inapopita, waovu hutoweka, lakini wenye haki husimama imara milele. 26Kama siki ilivyo kwa meno na moshi kwa macho, ndivyo alivyo mvivu kwa wale waliomtuma. 27Kumcha Bwana huongeza urefu wa maisha, lakini miaka ya mwovu inafupishwa. 28Tarajio la mwenye haki ni furaha, bali matumaini ya mwovu huwa si kitu. 29Njia ya Bwana ni kimbilio kwa wenye haki, lakini ni maangamizi ya wale watendao mabaya. 30Kamwe wenye haki hawataondolewa, bali waovu hawatasalia katika nchi. 31Kinywa cha mwenye haki hutoa hekima, bali ulimi wa upotovu utakatwa. 32Midomo ya wenye haki inajua kile kinachofaa, bali kinywa cha mwovu hujua kile kilichopotoka tu.
1The proverbs of Solomon. A wise son makes a glad father; but a foolish son brings grief to his mother. 2Treasures of wickedness profit nothing, but righteousness delivers from death. 3Yahweh will not allow the soul of the righteous to go hungry, but he thrusts away the desire of the wicked. 4He becomes poor who works with a lazy hand, but the hand of the diligent brings wealth. 5He who gathers in summer is a wise son, but he who sleeps during the harvest is a son who causes shame. 6Blessings are on the head of the righteous, but violence covers the mouth of the wicked. 7The memory of the righteous is blessed, but the name of the wicked will rot. 8The wise in heart accept commandments, but a chattering fool will fall. 9He who walks blamelessly walks surely, but he who perverts his ways will be found out. 10One winking with the eye causes sorrow, but a chattering fool will fall. 11The mouth of the righteous is a spring of life, but violence covers the mouth of the wicked. 12Hatred stirs up strife, but love covers all wrongs. 13Wisdom is found on the lips of him who has discernment, but a rod is for the back of him who is void of understanding. 14Wise men lay up knowledge, but the mouth of the foolish is near ruin. 15The rich man’s wealth is his strong city. The destruction of the poor is their poverty. 16The labor of the righteous leads to life. The increase of the wicked leads to sin. 17He is in the way of life who heeds correction, but he who forsakes reproof leads others astray. 18He who hides hatred has lying lips. He who utters a slander is a fool. 19In the multitude of words there is no lack of disobedience, but he who restrains his lips does wisely. 20The tongue of the righteous is like choice silver. The heart of the wicked is of little worth. 21The lips of the righteous feed many, but the foolish die for lack of understanding. 22Yahweh’s blessing brings wealth, and he adds no trouble to it. 23It is a fool’s pleasure to do wickedness, but wisdom is a man of understanding’s pleasure. 24What the wicked fear, will overtake them, but the desire of the righteous will be granted. 25When the whirlwind passes, the wicked is no more; but the righteous stand firm forever. 26As vinegar to the teeth, and as smoke to the eyes, so is the sluggard to those who send him. 27The fear of Yahweh prolongs days, but the years of the wicked shall be shortened. 28The prospect of the righteous is joy, but the hope of the wicked will perish. 29The way of Yahweh is a stronghold to the upright, but it is a destruction to the workers of iniquity. 30The righteous will never be removed, but the wicked will not dwell in the land. 31The mouth of the righteous produces wisdom, but the perverse tongue will be cut off. 32The lips of the righteous know what is acceptable, but the mouth of the wicked is perverse.
1De spreuken van Salomo. Een wijs zoon verblijdt den vader; maar een zot zoon is zijner moeder droefheid. 2Schatten der goddeloosheid doen geen nut; maar de gerechtigheid redt van den dood. 3De HEERE laat de ziel des rechtvaardigen niet hongeren; maar de have der goddelozen stoot Hij weg. 4Die met een bedriegelijke hand werkt, wordt arm; maar de hand der vlijtigen maakt rijk. 5Die in den zomer vergadert, is een verstandig zoon; maar die in den oogst vast slaapt, is een zoon die beschaamd maakt. 6Zegeningen zijn op het hoofd des rechtvaardigen; maar het geweld bedekt den mond der goddelozen. 7De gedachtenis des rechtvaardigen zal tot zegening zijn; maar de naam der goddelozen zal verrotten. 8Die wijs van hart is, neemt de geboden aan; maar die dwaas is van lippen, zal omgeworpen worden. 9Die in oprechtheid wandelt, wandelt zeker; maar die zijn wegen verkeert, zal bekend worden. 10Die met het oog wenkt, richt smart aan; en een dwaas van lippen zal omgeworpen worden. 11De mond des rechtvaardigen is een springader des levens; maar het geweld bedekt den mond der goddelozen. 12Haat verwekt krakelen; maar de liefde dekt alle overtredingen toe. 13In de lippen des verstandigen wordt wijsheid gevonden; maar op den rug des verstandelozen de roede. 14De wijzen leggen wetenschap weg; maar den mond des dwazen is de verstoring nabij. 15Des rijken goed is een stad zijner sterkte; de armoede der geringen is hun verstoring. 16Het werk des rechtvaardigen is ten leven; de inkomst des goddelozen is ter zonde. 17Het pad tot het leven is desgenen die de tucht bewaart; maar die de bestraffing verlaat, doet dwalen. 18Die den haat bedekt, is van valse lippen, en die een kwaad gerucht voortbrengt, is een zot. 19In de veelheid der woorden ontbreekt de overtreding niet; maar die zijn lippen wederhoudt, is kloek verstandig. 20De tong des rechtvaardigen is uitgelezen zilver; het hart der goddelozen is weinig waard. 21De lippen des rechtvaardigen voeden er velen; maar de dwazen sterven door gebrek van verstand. 22De zegen des HEEREN, die maakt rijk; en Hij voegt er geen smart bij. 23Het is voor den zot als spel, schandelijkheid te doen; maar voor een man van verstand, wijsheid te plegen. 24De vreze des goddelozen, die zal hem overkomen; maar de begeerte der rechtvaardigen zal God geven. 25Gelijk een wervelwind voorbijgaat, alzo is de goddeloze niet meer; maar de rechtvaardige is een eeuwige grondvest. 26Gelijk edik den tanden, en gelijk rook den ogen is zo is de luie dengenen, die hem uitzenden. 27De vreze des HEEREN vermeerdert de dagen; maar de jaren der goddelozen worden verkort. 28De hoop der rechtvaardigen is blijdschap; maar de verwachting der goddelozen zal vergaan. 29De weg des HEEREN is voor den oprechte sterkte; maar voor de werkers der ongerechtigheid verstoring. 30De rechtvaardige zal in eeuwigheid niet bewogen worden; maar de goddelozen zullen de aarde niet bewonen. 31De mond des rechtvaardigen brengt overvloediglijk wijsheid voort; maar de tong der verkeerdheden zal uitgeroeid worden. 32De lippen des rechtvaardigen weten wat welgevallig is; maar de mond der goddelozen enkel verkeerdheid.
Bonyeza Enter ili kuuwekea mstari huu rangi, kuandika maelezo au kuunakili. Vitufe vya mishale vinakupeleka kwenye mstari unaofuata.
Namba za mistari hufuata tafsiri uliyochagua, na katika sura chache zinaweza kutofautiana kwa mstari mmoja.