1Mtu anayeendelea kuwa na shingo ngumu baada ya maonyo mengi, ataangamia ghafula, wala hapati dawa. 2Wenye haki wanapostawi, watu hufurahi; waovu watawalapo, watu hulia kwa huzuni. 3Mtu apendaye hekima huleta furaha kwa baba yake, bali aambatanaye na makahaba hutapanya mali yake. 4Kwa haki mfalme huipa nchi uthabiti, bali mfalme aliye na tamaa ya rushwa huiangamiza. 5Yeyote amsifuye jirani yake isivyostahili, anautandaza wavu kuitega miguu yake. 6Mtu mbaya hutegwa na dhambi yake mwenyewe bali mwenye haki huweza kuimba na kufurahi. 7Mwenye haki hujali haki kwa ajili ya maskini, bali mwovu hajishughulishi na hilo. 8Wenye mzaha huuchochea mji, bali watu wenye hekima hugeuzia mbali hasira. 9Kama mwenye hekima akienda mahakamani na mpumbavu, mpumbavu hukasirika na kudhihaki, wala hakuna amani. 10Watu wamwagao damu humchukia mtu mwadilifu na hutafuta kumuua mtu mnyofu. 11Mpumbavu huonyesha hasira yake yote, bali mwenye hekima hujizuia. 12Kama mtawala akisikiliza uongo, maafisa wake wote huwa waovu. 13Mtu maskini na mtu anayeonea wanafanana kwa jambo hili: Bwana hutia nuru macho yao wote wawili. 14Kama mfalme akiwaamua maskini kwa haki, kiti chake cha enzi kitakuwa thabiti siku zote. 15Fimbo ya maonyo hutia hekima, bali mtoto aliyeachiwa bila maonyo humwaibisha mama yake. 16Wakati waovu wanapostawi, pia dhambi vivyo hivyo, lakini wenye haki wataliona anguko lao. 17Mrudi mwanao, naye atakupa amani, atakufurahisha nafsi yako. 18Mahali pasipo na ufunuo, watu kujizuia, bali ana heri mtu yule aishikaye sheria. 19Mtumishi hawezi kuonywa kwa maneno matupu, ajapoelewa, hataitikia. 20Je, unamwona mtu azungumzaye kwa haraka? Kuna matumaini zaidi kwa mpumbavu kuliko yeye. 21Kama mtu akimdekeza mtumishi wake tangu ujanani, atamletea sikitiko mwishoni. 22Mtu mwenye hasira huchochea ugomvi, naye mtu mwenye hasira ya haraka hutenda dhambi nyingi. 23Kiburi cha mtu humshusha, bali mtu mwenye roho ya unyenyekevu hupata heshima. 24Anayekubaliana na mwizi ni adui wa nafsi yake mwenyewe; huapishwa lakini hathubutu kushuhudia. 25Kuwaogopa watu huwa ni mtego, bali yeyote amtumainiaye Bwana atakuwa salama. 26Wengi hutafuta kusikilizwa na mtawala, bali mtu hupata haki kutoka kwa Bwana. 27Mwenye haki huwachukia sana wasio waaminifu; waovu huwachukia sana wenye haki.
1He who is often rebuked and stiffens his neck will be destroyed suddenly, with no remedy. 2When the righteous thrive, the people rejoice; but when the wicked rule, the people groan. 3Whoever loves wisdom brings joy to his father; but a companion of prostitutes squanders his wealth. 4The king by justice makes the land stable, but he who takes bribes tears it down. 5A man who flatters his neighbor spreads a net for his feet. 6An evil man is snared by his sin, but the righteous can sing and be glad. 7The righteous care about justice for the poor. The wicked aren’t concerned about knowledge. 8Mockers stir up a city, but wise men turn away anger. 9If a wise man goes to court with a foolish man, the fool rages or scoffs, and there is no peace. 10The bloodthirsty hate a man of integrity; and they seek the life of the upright. 11A fool vents all of his anger, but a wise man brings himself under control. 12If a ruler listens to lies, all of his officials are wicked. 13The poor man and the oppressor have this in common: Yahweh gives sight to the eyes of both. 14The king who fairly judges the poor, his throne shall be established forever. 15The rod of correction gives wisdom, but a child left to himself causes shame to his mother. 16When the wicked increase, sin increases; but the righteous will see their downfall. 17Correct your son, and he will give you peace; yes, he will bring delight to your soul. 18Where there is no revelation, the people cast off restraint; but one who keeps the law is blessed. 19A servant can’t be corrected by words. Though he understands, yet he will not respond. 20Do you see a man who is hasty in his words? There is more hope for a fool than for him. 21He who pampers his servant from youth will have him become a son in the end. 22An angry man stirs up strife, and a wrathful man abounds in sin. 23A man’s pride brings him low, but one of lowly spirit gains honor. 24Whoever is an accomplice of a thief is an enemy of his own soul. He takes an oath, but dares not testify. 25The fear of man proves to be a snare, but whoever puts his trust in Yahweh is kept safe. 26Many seek the ruler’s favor, but a man’s justice comes from Yahweh. 27A dishonest man detests the righteous, and the upright in their ways detest the wicked.
1Een man, die, dikwijls bestraft zijnde, den nek verhardt, zal schielijk verbroken worden, zodat er geen genezen aan zij. 2Als de rechtvaardigen groot worden, verblijdt zich het volk; maar als de goddeloze heerst, zucht het volk. 3Een man, die de wijsheid bemint, verblijdt zijn vader; maar die een metgezel der hoeren is, brengt het goed door. 4Een koning houdt het land staande door het recht; maar een, die tot geschenken genegen is, verstoort hetzelve. 5Een man, die zijn naaste vleit, spreidt een net uit voor deszelfs gangen. 6In de overtreding eens bozen mans is een strik; maar de rechtvaardige juicht en is blijde. 7De rechtvaardige neemt kennis van de rechtzaak der armen; maar de goddeloze begrijpt de wetenschap niet. 8Spotdrijvende lieden blazen een stad aan brand; maar de wijzen keren den toorn af. 9Een wijs man, met een dwaas man in rechten zich begeven hebbende, hetzij dat hij beroerd is of lacht, zo is er toch geen rust. 10Bloedgierige lieden haten den vrome; maar de oprechten zoeken zijn ziel. 11Een zot laat zijn gansen geest uit, maar de wijze wederhoudt dien achterwaarts. 12Een heerser, die op leugentaal acht geeft, al zijn dienaars zijn goddeloos. 13De arme en de bedrieger ontmoeten elkander; de HEERE verlicht hun beider ogen. 14Een koning, die de armen in trouw recht doet, diens troon zal in eeuwigheid bevestigd worden. 15De roede, en de bestraffing geeft wijsheid; maar een kind, dat aan zichzelf gelaten is, beschaamt zijn moeder. 16Als de goddelozen velen worden, wordt de overtreding veel; maar de rechtvaardigen zullen hun val aanzien. 17Tuchtig uw zoon, en hij zal u gerustheid aandoen, en hij zal uw ziel vermakelijkheden geven. 18Als er geen profetie is, wordt het volk ontbloot; maar welgelukzalig is hij, die de wet bewaart. 19Een knecht zal door de woorden niet getuchtigd worden; hoewel hij u verstaat, nochtans zal hij niet antwoorden. 20Hebt gij een man gezien, die haastig in zijn woorden is? Van een zot is meer verwachting dan van hem. 21Als men zijn knecht van jongs op weeldig houdt, hij zal in zijn laatste een zoon willen zijn. 22Een toornig man verwekt gekijf; en de grammoedige is veelvoudig in overtreding. 23De hoogmoed des mensen zal hem vernederen; maar de nederige van geest zal de eer vasthouden. 24Die met een dief deelt, haat zijn ziel; hij hoort een vloek, en hij geeft het niet te kennen. 25De siddering des mensen legt een strik; maar die op den HEERE vertrouwt, zal in een hoog vertrek gesteld worden. 26Velen zoeken het aangezicht des heersers; maar een ieders recht is van den HEERE. 27Een ongerechtig man is den rechtvaardige een gruwel; maar die recht is van weg, is den goddeloze een gruwel.
Bonyeza Enter ili kuuwekea mstari huu rangi, kuandika maelezo au kuunakili. Vitufe vya mishale vinakupeleka kwenye mstari unaofuata.
Namba za mistari hufuata tafsiri uliyochagua, na katika sura chache zinaweza kutofautiana kwa mstari mmoja.