1Usijisifu kwa ajili ya kesho, kwa kuwa hujui ni nini kitakachozaliwa kwa siku moja. 2Mwache mwingine akusifu, wala si kinywa chako mwenyewe; mtu mwingine afanye hivyo na si midomo yako mwenyewe. 3Jiwe ni zito na mchanga ni mzigo, lakini kukasirishwa na mpumbavu ni kuzito kuliko vyote viwili. 4Hasira ni ukatili na ghadhabu kali ni gharika, lakini ni nani awezaye kusimama mbele ya wivu? 5Afadhali karipio la wazi kuliko upendo uliofichika. 6Majeraha kutoka kwa rafiki yaonyesha uaminifu, bali kubusu kwa adui ni kwingi sana. 7Yeye aliyeshiba huchukia kabisa asali, bali kwa mwenye njaa hata kile kilicho kichungu kwake ni kitamu. 8Kama ndege atangatangavyo mbali na kiota chake, ndivyo alivyo mtu atangatangaye mbali na nyumbani mwake. 9Manukato na uvumba huleta furaha moyoni, nao uzuri wa rafiki huchipuka kutoka kwenye ushauri wake wa uaminifu. 10Usimwache rafiki yako wala rafiki wa baba yako, tena usiende nyumbani mwa ndugu yako wakati umepatwa na maafa. Bora jirani wa karibu kuliko ndugu aliye mbali. 11Mwanangu, uwe na hekima, nawe ulete furaha moyoni mwangu, ndipo nitakapoweza kumjibu yeyote anitendaye kwa dharau. 12Mtu mwenye busara huona hatari na kujificha, bali mjinga huendelea mbele nayo ikamtesa. 13Chukua vazi la yule awekaye dhamana kwa ajili ya mgeni; lishikilie iwe dhamana kama anafanya hivyo kwa ajili ya mwanamke mpotovu. 14Kama mtu akimbariki jirani yake kwa sauti kuu asubuhi na mapema, itahesabiwa kama ni laana. 15Mke mgomvi ni kama matone yasiyokoma ya siku ya mvua. 16Kumzuia yeye ni kama kuuzuia upepo au kukamata mafuta kwa kiganja cha mkono. 17Kama vile chuma kinoavyo chuma, ndivyo mtu amnoavyo mwenzake. 18Yeye autunzaye mtini atakula tunda lake, naye amtunzaye bwana wake ataheshimiwa. 19Kama uso uonekanavyo kwenye maji, ndivyo hivyo moyo wa mtu humwonyesha alivyo. 20Kuzimu na Uharibifu havishibi kadhalika macho ya mwanadamu. 21Kalibu ni kwa ajili ya fedha na tanuru kwa ajili ya dhahabu, bali mtu hupimwa kwa sifa azipokeazo. 22Hata ukimtwanga mpumbavu kwenye kinu, ukimtwanga kama nafaka kwa mchi, hutauondoa upumbavu wake. 23Hakikisha kuwa unajua hali ya makundi yako ya kondoo na mbuzi, angalia kwa bidii ngʼombe zako. 24Kwa kuwa utajiri haudumu milele, nayo taji haidumu vizazi vyote. 25Wakati majani makavu yameondolewa na mapya yamechipua, nayo majani toka milimani yamekusanywa, 26wana-kondoo watakupatia mavazi na mbuzi thamani ya shamba. 27Utakuwa na maziwa mengi ya mbuzi kukulisha wewe na jamaa yako, na kuwalisha watumishi wako wa kike.
1Don’t boast about tomorrow; for you don’t know what a day may bring. 2Let another man praise you, and not your own mouth; a stranger, and not your own lips. 3A stone is heavy, and sand is a burden; but a fool’s provocation is heavier than both. 4Wrath is cruel, and anger is overwhelming; but who is able to stand before jealousy? 5Better is open rebuke than hidden love. 6Faithful are the wounds of a friend; although the kisses of an enemy are profuse. 7A full soul loathes a honeycomb; but to a hungry soul, every bitter thing is sweet. 8As a bird that wanders from her nest, so is a man who wanders from his home. 9Perfume and incense bring joy to the heart; so does earnest counsel from a man’s friend. 10Don’t forsake your friend and your father’s friend. Don’t go to your brother’s house in the day of your disaster: better is a neighbor who is near than a distant brother. 11Be wise, my son, and bring joy to my heart, then I can answer my tormentor. 12A prudent man sees danger and takes refuge; but the simple pass on, and suffer for it. 13Take his garment when he puts up collateral for a stranger. Hold it for a wayward woman! 14He who blesses his neighbor with a loud voice early in the morning, it will be taken as a curse by him. 15A continual dropping on a rainy day and a contentious wife are alike: 16restraining her is like restraining the wind, or like grasping oil in his right hand. 17Iron sharpens iron; so a man sharpens his friend’s countenance. 18Whoever tends the fig tree shall eat its fruit. He who looks after his master shall be honored. 19Like water reflects a face, so a man’s heart reflects the man. 20Sheol and Abaddon are never satisfied; and a man’s eyes are never satisfied. 21The crucible is for silver, and the furnace for gold; but man is refined by his praise. 22Though you grind a fool in a mortar with a pestle along with grain, yet his foolishness will not be removed from him. 23Know well the state of your flocks, and pay attention to your herds: 24for riches are not forever, nor does even the crown endure to all generations. 25The hay is removed, and the new growth appears, the grasses of the hills are gathered in. 26The lambs are for your clothing, and the goats are the price of a field. 27There will be plenty of goats’ milk for your food, for your family’s food, and for the nourishment of your servant girls.
1Beroem u niet over den dag van morgen; want gij weet niet, wat de dag zal baren. 2Laat u een vreemde prijzen, en niet uw mond; een onbekende, en niet uw lippen. 3Een steen is zwaar, en het zand gewichtig; maar de toornigheid des dwazen is zwaarder dan die beide. 4Grimmigheid en overloping van toorn is wreedheid; maar wie zal voor nijdigheid bestaan? 5Openbare bestraffing is beter dan verborgene liefde. 6De wonden des liefhebbers zijn getrouw; maar de kussingen des haters zijn af te bidden. 7Een verzadigde ziel vertreedt het honigzeem; maar aan een hongerige ziel is alle bitter zoet. 8Gelijk een vogel is, die uit zijn nest omdoolt, alzo is een man, die omdoolt uit zijn plaats. 9Olie en reukwerk verblijdt het hart; alzo is de zoetigheid van iemands vriend, vanwege den raad der ziel. 10Verlaat uw vriend, noch den vriend uws vaders niet; en ga ten huize uws broeders niet op den dag van uw tegenspoed. Beter is een gebuur die nabij is, dan een broeder, die verre is. 11Zijt wijs, mijn zoon, en verblijd mijn hart; opdat ik mijn smader wat te antwoorden heb. 12De kloekzinnige ziet het kwaad, en verbergt zich; de slechten gaan henen door, en worden gestraft. 13Als iemand voor een vreemde borg geworden is, neem zijn kleed, en pand hem voor een onbekende vrouw. 14Die zijn vriend zegent met luider stem, zich des morgens vroeg opmakende, het zal hem tot een vloek gerekend worden. 15Een gedurige druiping ten dage des slagregens en een kijfachtige huisvrouw zijn even gelijk. 16Elkeen, die haar verbergt, zou den wind verbergen, en de olie zijner rechterhand, die roept. 17Ijzer scherpt men met ijzer; alzo scherpt een man het aangezicht zijns naasten. 18Die den vijgeboom bewaart, zal zijn vrucht eten; en die zijn heer waarneemt, zal geeerd worden. 19Gelijk in het water het aangezicht is tegen het aangezicht, alzo is des mensen hart tegen den mens. 20De hel en het verderf worden niet verzadigd; alzo worden de ogen des mensen niet verzadigd. 21De smeltkroes is voor het zilver, en de oven voor het goud; alzo is een man naar zijn lof te proeven. 22Al stiet gij den dwaas in een mortier met een stamper, in het midden van het gestoten graan, zijn dwaasheid zou van hem niet afwijken. 23Zijt naarstig, om het aangezicht uwer schapen te kennen; zet uw hart op de kudden. 24Want de schat is niet tot in eeuwigheid; of zal de kroon van geslacht tot geslacht zijn? 25Als het gras zich openbaart, en de grasscheuten gezien worden, laat de kruiden der bergen verzameld worden. 26De lammeren zullen zijn tot uw kleding, en de bokken de prijs des velds. 27Daartoe zult gij genoegzaamheid van geitenmelk hebben tot uw spijze, tot spijze van uw huis, en leeftocht uwer maagden.
Bonyeza Enter ili kuuwekea mstari huu rangi, kuandika maelezo au kuunakili. Vitufe vya mishale vinakupeleka kwenye mstari unaofuata.
Namba za mistari hufuata tafsiri uliyochagua, na katika sura chache zinaweza kutofautiana kwa mstari mmoja.