1Afadhali kula ukoko mkavu ukiwa na amani na utulivu kuliko kukaa kwenye nyumba ya karamu kukiwa na magomvi. 2Mtumishi mwenye hekima atatawala juu ya mwana aaibishaye, naye atashirikiana katika urithi kama mmoja wa hao ndugu. 3Kalibu ni kwa ajili ya fedha na tanuru ni kwa ajili ya dhahabu, bali Bwana huujaribu moyo. 4Mtu mwovu husikiliza midomo mibaya; mwongo husikiliza kwa makini ulimi wa madhara. 5Yeye anaye mdhihaki maskini huonyesha dharau kwa Muumba wake; yeyote afurahiaye maafa hataepuka kuadhibiwa. 6Wana wa wana ni taji la wazee, nao wazazi ni fahari ya watoto wao. 7Midomo yenye uwezo wa ushawishi haimfai mpumbavu: je, ni mibaya kiasi gani zaidi midomo ya uongo kwa mtawala! 8Kipawa ni kama kito cha thamani machoni pake yeye aliye nacho; kokote kigeukiapo, hufanikiwa. 9Yeye anayesamehe kosa hudumisha upendo, bali yeyote arudiaye jambo hutenganisha marafiki wa karibu. 10Karipio humwingia sana mtu mwenye kutambua kuliko mapigo mia kwa mpumbavu. 11Mtu mbaya hupenda kuasi tu; mjumbe asiye na huruma atatumwa dhidi yake. 12Ni afadhali ukutane na dubu aliyenyangʼanywa watoto wake, kuliko mpumbavu katika upumbavu wake. 13Ikiwa mtu atalipa baya kwa jema, kamwe ubaya hautaondoka katika nyumba yake. 14Kuanzisha ugomvi ni kama kutoboa bwawa la maji; kwa hiyo acha jambo hilo kabla mabishano hayajaanza. 15Yeye asemaye kuwa asiye na haki ana haki, naye asemaye kuwa mwenye haki hana haki: Bwana huwachukia sana wote wawili. 16Fedha ina faida gani mikononi mwa mpumbavu, wakati yeye hana haja ya kupata hekima? 17Rafiki hupenda wakati wote naye ndugu amezaliwa kwa ajili ya wakati wa shida. 18Mtu mjinga hupana mkono ili kuweka rehani, naye huweka dhamana kwa jirani yake. 19Yeye apendaye ugomvi apenda dhambi; naye ainuaye sana lango lake hutafuta uharibifu. 20Mtu mwenye moyo mpotovu hawezi kufanikiwa; naye ambaye ulimi wake ni mdanganyifu huanguka kwenye taabu. 21Kuwa na mwana mpumbavu huleta huzuni; hakuna furaha kwa baba wa mpumbavu. 22Moyo wenye furaha ni dawa nzuri, bali roho iliyopondeka hukausha mifupa. 23Mtu mwovu hukubali rushwa kwa siri ili kupotosha njia ya haki. 24Mtu wa ufahamu huitazama hekima, lakini macho ya mpumbavu huhangaika hadi kwenye miisho ya dunia. 25Mwana mpumbavu huleta huzuni kwa baba yake na uchungu kwa yeye aliyemzaa. 26Si vizuri kumwadhibu mtu asiye na hatia, au kuwapiga sana maafisa kwa ajili ya uadilifu wao. 27Mtu mwenye maarifa hutumia maneno kwa kujizuia, naye mtu mwenye ufahamu ana moyo wa utulivu. 28Hata mtu mpumbavu hudhaniwa kuwa na hekima kama akinyamaza, na mwenye ufahamu kama akiuzuia ulimi wake.
1Better is a dry morsel with quietness, than a house full of feasting with strife. 2A servant who deals wisely will rule over a son who causes shame, and shall have a part in the inheritance among the brothers. 3The refining pot is for silver, and the furnace for gold, but Yahweh tests the hearts. 4An evildoer heeds wicked lips. A liar gives ear to a mischievous tongue. 5Whoever mocks the poor reproaches his Maker. He who is glad at calamity shall not be unpunished. 6Children’s children are the crown of old men; the glory of children are their parents. 7Arrogant speech isn’t fitting for a fool, much less do lying lips fit a prince. 8A bribe is a precious stone in the eyes of him who gives it; wherever he turns, he prospers. 9He who covers an offense promotes love; but he who repeats a matter separates best friends. 10A rebuke enters deeper into one who has understanding than a hundred lashes into a fool. 11An evil man seeks only rebellion; therefore a cruel messenger shall be sent against him. 12Let a bear robbed of her cubs meet a man, rather than a fool in his folly. 13Whoever rewards evil for good, evil shall not depart from his house. 14The beginning of strife is like breaching a dam, therefore stop contention before quarreling breaks out. 15He who justifies the wicked, and he who condemns the righteous, both of them alike are an abomination to Yahweh. 16Why is there money in the hand of a fool to buy wisdom, since he has no understanding? 17A friend loves at all times; and a brother is born for adversity. 18A man void of understanding strikes hands, and becomes collateral in the presence of his neighbor. 19He who loves disobedience loves strife. One who builds a high gate seeks destruction. 20One who has a perverse heart doesn’t find prosperity, and one who has a deceitful tongue falls into trouble. 21He who becomes the father of a fool grieves. The father of a fool has no joy. 22A cheerful heart makes good medicine, but a crushed spirit dries up the bones. 23A wicked man receives a bribe in secret, to pervert the ways of justice. 24Wisdom is before the face of one who has understanding, but the eyes of a fool wander to the ends of the earth. 25A foolish son brings grief to his father, and bitterness to her who bore him. 26Also to punish the righteous is not good, nor to flog officials for their integrity. 27He who spares his words has knowledge. He who is even tempered is a man of understanding. 28Even a fool, when he keeps silent, is counted wise. When he shuts his lips, he is thought to be discerning.
1Een droge bete, en rust daarbij, is beter, dan een huis vol van geslachte beesten met twist. 2Een verstandig knecht zal heersen over een zoon, die beschaamd maakt, en in het midden der broederen zal hij erfenis delen. 3De smeltkroes is voor het zilver, en de oven voor het goud; maar de HEERE proeft de harten. 4De boosdoener merkt op de ongerechtige lip; een leugenaar neigt het oor tot de verkeerde tong. 5Die den arme bespot, smaadt deszelfs Maker; die zich verblijdt in het verderf, zal niet onschuldig zijn. 6De kroon de ouden zijn de kindskinderen, en der kinderen sieraad zijn hun vaderen. 7Een voortreffelijke lip past een dwaze niet, veelmin een prins een leugenachtige lip. 8Het geschenk is in de ogen zijner heren een aangenaam gesteente; waarhenen het zich zal wenden, zal het wel gedijen. 9Die de overtreding toedekt, zoekt liefde; maar die de zaak weder ophaalt, scheidt den voornaamsten vriend. 10De bestraffing gaat dieper in den verstandige, dan den zot honderd maal te slaan. 11Zekerlijk, de wederspannige zoekt het kwaad; maar een wrede bode zal tegen hem gezonden worden. 12Dat een beer, die van jongen beroofd is, een man tegemoet kome, maar niet een zot in zijn dwaasheid. 13Die kwaad voor goed vergeldt, het kwaad zal van zijn huis niet wijken. 14Het begin des krakeels is gelijk een, die het water opening geeft; daarom verlaat den twist, eer hij zich vermengt. 15Wie den goddeloze rechtvaardigt, en den rechtvaardige verdoemt, zijn den HEERE een gruwel, ja, die beiden. 16Waarom toch zou in de hand des zots het koopgeld zijn, om wijsheid te kopen, dewijl hij geen verstand heeft? 17Een vriend heeft te aller tijd lief; en een broeder wordt in de benauwdheid geboren. 18Een verstandeloos mens klapt in de hand, zich borg stellende bij zijn naaste. 19Die het gekijf liefheeft, heeft de overtreding lief; die zijn deur verhoogt, zoekt verbreking. 20Wie verdraaid is van hart, zal het goede niet vinden; en die verkeerd is met zijn tong, zal in het kwaad vallen. 21Wie een zot genereert, die zal hem tot droefheid zijn; en de vader des dwazen zal zich niet verblijden. 22Een blij hart zal een medicijn goed maken; maar een verslagen geest zal het gebeente verdrogen. 23De goddeloze zal het geschenk uit den schoot nemen, om de paden des rechts te buigen. 24In het aangezicht des verstandigen is wijsheid; maar de ogen des zots zijn in het einde der aarde. 25Een zotte zoon is een verdriet voor zijn vader, en bittere droefheid voor degene, die hem gebaard heeft. 26Het is niet goed, den rechtvaardige ook te doen boeten, dat de prinsen iemand slaan zouden om hetgeen recht is. 27Wie wetenschap weet, houdt zijn woorden in; en een man van verstand is kostelijk van geest. 28Een dwaas zelfs, die zwijgt, zal wijs geacht worden, en die zijn lippen toesluit, verstandig.
Bonyeza Enter ili kuuwekea mstari huu rangi, kuandika maelezo au kuunakili. Vitufe vya mishale vinakupeleka kwenye mstari unaofuata.
Namba za mistari hufuata tafsiri uliyochagua, na katika sura chache zinaweza kutofautiana kwa mstari mmoja.