1Mwanamke mwenye hekima huijenga nyumba yake, bali mpumbavu huibomoa nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe. 2Yeye ambaye njia zake ni nyofu humcha Bwana, bali yeye ambaye njia zake zimepotoka humdharau Mungu. 3Mazungumzo ya mpumbavu huleta fimbo mgongoni mwake, bali mwenye hekima hulindwa na maneno ya midomo yake. 4Pale ambapo hakuna mafahali, hori ni tupu, bali kutokana na nguvu za fahali huja mavuno mengi. 5Shahidi mwaminifu hadanganyi, bali shahidi wa uongo humimina uongo. 6Mwenye mzaha huitafuta hekima na haipati, bali maarifa huja kwa urahisi kwa anayepambanua. 7Kaa mbali na mtu mpumbavu, kwa maana hutapata maarifa katika midomo yake. 8Hekima ya mwenye busara ni kufikiria njia zake, bali upumbavu wa wapumbavu ni udanganyifu. 9Wapumbavu hudhihaki kujirekebisha kutoka dhambi, bali wema hupatikana miongoni mwa wanyofu. 10Kila moyo hujua uchungu wake wenyewe, wala hakuna yeyote awezaye kushiriki furaha yake. 11Nyumba ya mwovu itaangamizwa, bali hema la mnyofu litastawi. 12Iko njia ionekanayo kuwa sawa kwa mtu, bali mwisho wake huelekeza mautini. 13Hata katika kicheko moyo waweza kuuma, nayo furaha yaweza kuishia katika majonzi. 14Wasio na imani watapatilizwa kikamilifu kwa ajili ya njia zao, naye mtu mwema atapewa thawabu kwa ajili ya njia yake. 15Mtu mjinga huamini kila kitu, bali mwenye busara hufikiria hatua zake. 16Mtu mwenye hekima humcha Bwana na kuepuka mabaya, bali mpumbavu hukasirika kwa hamaki na uzembe. 17Mtu anayekasirika kwa haraka hufanya mambo ya upumbavu, naye mtu wa hila huchukiwa. 18Mjinga hurithi upumbavu, bali wenye busara huvikwa maarifa kichwani kama taji. 19Watu wabaya watasujudu mbele ya watu wema, nao waovu kwenye malango ya wenye haki. 20Maskini huepukwa hata na majirani zao, bali matajiri wana marafiki wengi. 21Yeye anayemdharau jirani yake hutenda dhambi, bali amebarikiwa yeye aliye na huruma kwa mhitaji. 22Je, wale wanaopanga ubaya hawapotoki? Bali wale wanaopanga kilicho chema hupata upendo na uaminifu. 23Kazi zote zinazofanywa kwa bidii huleta faida, bali mazungumzo matupu huelekea umaskini tu. 24Utajiri wa wenye hekima ni taji yao, bali upumbavu wa wapumbavu huzaa upumbavu. 25Shahidi wa kweli huokoa maisha, bali shahidi wa uongo ni mdanganyifu. 26Yeye amchaye Bwana ana ngome salama, na kwa watoto wake itakuwa kimbilio. 27Kumcha Bwana ni chemchemi ya uzima, ili kumwepusha mtu na mitego ya mauti. 28Wingi wa watu ni utukufu wa mfalme, bali pasipo watu mkuu huangamia. 29Mtu mwenye subira ana ufahamu mwingi, bali anayekasirika haraka huonyesha upumbavu. 30Moyo wenye amani huupa mwili uzima, bali wivu huozesha mifupa. 31Yeye amwoneaye maskini huonyesha dharau kwa Muumba wao, bali yeyote anayemhurumia mhitaji humheshimu Mungu. 32Waovu huangamizwa kwa matendo yao maovu, bali hata katika kifo wenye haki hupata kimbilio. 33Hekima hukaa katika moyo wa mwenye ufahamu bali haijulikani miongoni mwa wapumbavu. 34Haki huinua taifa, bali dhambi ni aibu kwa watu wote. 35Mfalme hupendezwa na mtumishi mwenye hekima, bali ghadhabu yake humwangukia mtumishi mwenye kuaibisha.
1Every wise woman builds her house, but the foolish one tears it down with her own hands. 2He who walks in his uprightness fears Yahweh, but he who is perverse in his ways despises him. 3The fool’s talk brings a rod to his back, but the lips of the wise protect them. 4Where no oxen are, the crib is clean, but much increase is by the strength of the ox. 5A truthful witness will not lie, but a false witness pours out lies. 6A scoffer seeks wisdom, and doesn’t find it, but knowledge comes easily to a discerning person. 7Stay away from a foolish man, for you won’t find knowledge on his lips. 8The wisdom of the prudent is to think about his way, but the folly of fools is deceit. 9Fools mock at making atonement for sins, but among the upright there is good will. 10The heart knows its own bitterness and joy; he will not share these with a stranger. 11The house of the wicked will be overthrown, but the tent of the upright will flourish. 12There is a way which seems right to a man, but in the end it leads to death. 13Even in laughter the heart may be sorrowful, and mirth may end in heaviness. 14The unfaithful will be repaid for his own ways; likewise a good man will be rewarded for his ways. 15A simple man believes everything, but the prudent man carefully considers his ways. 16A wise man fears, and shuns evil, but the fool is hot headed and reckless. 17He who is quick to become angry will commit folly, and a crafty man is hated. 18The simple inherit folly, but the prudent are crowned with knowledge. 19The evil bow down before the good, and the wicked at the gates of the righteous. 20The poor person is shunned even by his own neighbor, but the rich person has many friends. 21He who despises his neighbor sins, but blessed is he who has pity on the poor. 22Don’t they go astray who plot evil? But love and faithfulness belong to those who plan good. 23In all hard work there is profit, but the talk of the lips leads only to poverty. 24The crown of the wise is their riches, but the folly of fools crowns them with folly. 25A truthful witness saves souls, but a false witness is deceitful. 26In the fear of Yahweh is a secure fortress, and he will be a refuge for his children. 27The fear of Yahweh is a fountain of life, turning people from the snares of death. 28In the multitude of people is the king’s glory, but in the lack of people is the destruction of the prince. 29He who is slow to anger has great understanding, but he who has a quick temper displays folly. 30The life of the body is a heart at peace, but envy rots the bones. 31He who oppresses the poor shows contempt for his Maker, but he who is kind to the needy honors him. 32The wicked is brought down in his calamity, but in death, the righteous has a refuge. 33Wisdom rests in the heart of one who has understanding, and is even made known in the inward part of fools. 34Righteousness exalts a nation, but sin is a disgrace to any people. 35The king’s favor is toward a servant who deals wisely, but his wrath is toward one who causes shame.
1Elke wijze vrouw bouwt haar huis; maar die zeer dwaas is, breekt het af met haar handen. 2Die in zijn oprechtheid wandelt, vreest den HEERE; maar die afwijkt in zijn wegen, veracht Hem. 3In den mond des dwazen is een roede des hoogmoeds; maar de lippen der wijzen bewaren hen. 4Als er geen ossen zijn, zo is de krib rein; maar door de kracht van den os is der inkomsten veel. 5Een waarachtig getuige zal niet liegen; maar een vals getuige blaast leugens. 6De spotter zoekt wijsheid, en er is gene; maar de wetenschap is voor den verstandige licht. 7Ga weg van de tegenwoordigheid eens zotten mans; want gij zoudt bij hem geen lippen der wetenschap merken. 8De wijsheid des kloekzinnigen is zijn weg te verstaan; maar dwaasheid der zotten is bedriegerij. 9Elke dwaas zal de schuld verbloemen; maar onder de oprechten is goedwilligheid. 10Het hart kent zijn eigen bittere droefheid; en een vreemde zal zich met deszelfs blijdschap niet vermengen. 11Het huis der goddelozen zal verdelgd worden; maar de tent der oprechten zal bloeien. 12Er is een weg, die iemand recht schijnt; maar het laatste van dien zijn wegen des doods. 13Het hart zal ook in het lachen smart hebben; en het laatste van die blijdschap is droefheid. 14Die afkerig van hart is, zal van zijn wegen verzadigd worden; maar een goed man van zichzelven. 15De slechte gelooft alle woord; maar de kloekzinnige merkt op zijn gang. 16De wijze vreest, en wijkt van het kwade; maar de zot is oplopende toornig, en zorgeloos. 17Die haastig is tot toorn, zal dwaasheid doen; en een man van schandelijke verdichtselen zal gehaat worden. 18De slechten erven dwaasheid; maar de kloekzinnigen zullen zich met wetenschap kronen. 19De kwaden buigen voor het aangezicht der goeden neder, en de goddelozen voor de poorten des rechtvaardigen. 20De arme wordt zelfs van zijn vriend gehaat; maar de liefhebbers des rijken zijn vele. 21Die zijn naaste veracht, zondigt; maar die zich der nederigen ontfermt, die is welgelukzalig. 22Dwalen zij niet, die kwaad stichten? Maar weldadigheid en trouw is voor degenen, die goed stichten. 23In allen smartelijke arbeid is overschot; maar het woord der lippen strekt alleen tot gebrek. 24Der wijzen kroon is hun rijkdom; de dwaasheid der zotten is dwaasheid. 25Een waarachtig getuige redt de zielen; maar die leugens blaast, is een bedrieger. 26In de vreze des HEEREN is een sterk vertrouwen, en Hij zal Zijn kinderen een Toevlucht wezen. 27De vreze des HEEREN is een springader des levens, om af te wijken van de strikken des doods. 28In de menigte des volks is des konings heerlijkheid; maar in gebrek van volk is eens vorsten verstoring. 29De lankmoedige is groot van verstand; maar die haastig is van gemoed, verheft de dwaasheid. 30Een gezond hart is het leven des vleses; maar nijd is verrotting der beenderen. 31Die den arme verdrukt, smaadt deszelfs Maker; maar die zich des nooddruftigen ontfermt, eert Hem. 32De goddeloze zal heengedreven worden in zijn kwaad; maar de rechtvaardige betrouwt zelfs in zijn dood. 33Wijsheid rust in het hart des verstandigen; maar wat in het binnenste der zotten is, wordt bekend. 34Gerechtigheid verhoogt een volk, maar de zonde is een schandvlek der natien. 35Het welbehagen des konings is over een verstandigen knecht; maar zijn verbolgenheid zal zijn over dengene, die beschaamd maakt.
Bonyeza Enter ili kuuwekea mstari huu rangi, kuandika maelezo au kuunakili. Vitufe vya mishale vinakupeleka kwenye mstari unaofuata.
Namba za mistari hufuata tafsiri uliyochagua, na katika sura chache zinaweza kutofautiana kwa mstari mmoja.