1Mwanangu, usisahau mafundisho yangu, bali zitunze amri zangu moyoni mwako, 2kwa kuwa zitakuongezea miaka mingi ya maisha yako na kukuletea mafanikio. 3Usiache kamwe upendo na uaminifu vitengane nawe; vifunge shingoni mwako, viandike katika ubao wa moyo wako. 4Ndipo utapata kibali na jina zuri mbele za Mungu na mwanadamu. 5Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote wala usizitegemee akili zako mwenyewe; 6katika njia zako zote mkiri yeye, naye atayanyoosha mapito yako. 7Usiwe mwenye hekima machoni pako mwenyewe; mche Bwana ukajiepushe na uovu. 8Hii itakuletea afya mwilini mwako, na mafuta kwenye mifupa yako. 9Mheshimu Bwana kwa mali zako na kwa malimbuko ya mazao yako yote; 10ndipo ghala zako zitakapojaa hadi kufurika, viriba vyako vitafurika kwa mvinyo mpya. 11Mwanangu, usiidharau adhabu ya Bwana na usichukie kukaripiwa naye, 12kwa sababu Bwana huwaadibisha wale awapendao, kama vile baba afanyavyo kwa mwana apendezwaye naye. 13Heri mtu yule aonaye hekima, mtu yule apataye ufahamu, 14kwa maana hekima ana faida kuliko fedha na mapato yake ni bora kuliko ya dhahabu safi. 15Hekima ana thamani kuliko marijani; hakuna chochote unachokitamani kinachoweza kulinganishwa naye. 16Maisha marefu yako katika mkono wake wa kuume; katika mkono wake wa kushoto kuna utajiri na heshima. 17Njia zake zinapendeza, mapito yake yote ni amani. 18Yeye ni mti wa uzima kwa wale wanaomkumbatia; wale wamshikao watabarikiwa. 19Kwa hekima Bwana aliiweka misingi ya dunia, kwa ufahamu aliziweka mbingu mahali pake; 20kwa maarifa yake vilindi viligawanywa, nayo mawingu yanadondosha umande. 21Mwanangu, hifadhi maamuzi mema na busara, usiache vitoke machoni pako; 22ndipo vitakapokuwa uzima nafsini mwako na pambo la neema shingoni mwako. 23Kisha utaenda katika njia yako salama, wala mguu wako hautajikwaa; 24ulalapo, hautaogopa; ulalapo usingizi wako utakuwa mtamu. 25Usiogope maafa ya ghafula au maangamizi yanayowapata waovu, 26kwa kuwa Bwana atakuwa tumaini lako na kuepusha mguu wako kunaswa katika mtego. 27Usizuie wema kwa wale wanaostahili ikiwa katika uwezo wako kutenda. 28Usimwambie jirani yako, “Njoo baadaye, nitakupa kesho”: wakati wewe unacho kitu kile karibu nawe. 29Usifanye hila ya kumdhuru jirani yako, ambaye anaishi karibu na wewe akikuamini. 30Usimshtaki mtu bila sababu, wakati hajakutenda dhara lolote. 31Usimwonee wivu mtu mwenye jeuri wala kuchagua njia yake iwayo yote, 32kwa kuwa Bwana humchukia mtu mpotovu, lakini siri yake iko kwa mwenye haki. 33Laana ya Bwana i juu ya nyumba ya mwovu, lakini yeye huibariki nyumba ya mwenye haki. 34Huwadhihaki wale wanaodhihaki, lakini huwapa neema wale wanyenyekevu. 35Wenye hekima hurithi heshima, bali huwaaibisha wapumbavu.
1My son, don’t forget my teaching; but let your heart keep my commandments: 2for length of days, and years of life, and peace, will they add to you. 3Don’t let kindness and truth forsake you. Bind them around your neck. Write them on the tablet of your heart. 4So you will find favor, and good understanding in the sight of God and man. 5Trust in Yahweh with all your heart, and don’t lean on your own understanding. 6In all your ways acknowledge him, and he will make your paths straight. 7Don’t be wise in your own eyes. Fear Yahweh, and depart from evil. 8It will be health to your body, and nourishment to your bones. 9Honor Yahweh with your substance, with the first fruits of all your increase: 10so your barns will be filled with plenty, and your vats will overflow with new wine. 11My son, don’t despise Yahweh’s discipline, neither be weary of his reproof: 12for whom Yahweh loves, he reproves; even as a father reproves the son in whom he delights. 13Happy is the man who finds wisdom, the man who gets understanding. 14For her good profit is better than getting silver, and her return is better than fine gold. 15She is more precious than rubies. None of the things you can desire are to be compared to her. 16Length of days is in her right hand. In her left hand are riches and honor. 17Her ways are ways of pleasantness. All her paths are peace. 18She is a tree of life to those who lay hold of her. Happy is everyone who retains her. 19By wisdom Yahweh founded the earth. By understanding, he established the heavens. 20By his knowledge, the depths were broken up, and the skies drop down the dew. 21My son, let them not depart from your eyes. Keep sound wisdom and discretion: 22so they will be life to your soul, and grace for your neck. 23Then you shall walk in your way securely. Your foot won’t stumble. 24When you lie down, you will not be afraid. Yes, you will lie down, and your sleep will be sweet. 25Don’t be afraid of sudden fear, neither of the desolation of the wicked, when it comes: 26for Yahweh will be your confidence, and will keep your foot from being taken. 27Don’t withhold good from those to whom it is due, when it is in the power of your hand to do it. 28Don’t say to your neighbor, “Go, and come again; tomorrow I will give it to you,” when you have it by you. 29Don’t devise evil against your neighbor, since he dwells securely by you. 30Don’t strive with a man without cause, if he has done you no harm. 31Don’t envy the man of violence. Choose none of his ways. 32For the perverse is an abomination to Yahweh, but his friendship is with the upright. 33Yahweh’s curse is in the house of the wicked, but he blesses the habitation of the righteous. 34Surely he mocks the mockers, but he gives grace to the humble. 35The wise will inherit glory, but shame will be the promotion of fools.
1Mijn zoon! vergeet mijn wet niet, maar uw hart beware mijn geboden. 2Want langheid van dagen, en jaren van leven, en vrede zullen zij u vermeerderen. 3Dat de goedertierenheid en de trouw u niet verlaten; bind ze aan uw hals, schrijf zij op de tafel uws harten. 4En vind gunst en goed verstand, in de ogen Gods en der mensen. 5Vertrouw op den HEERE met uw ganse hart, en steun op uw verstand niet. 6Ken Hem in al uw wegen, en Hij zal uw paden recht maken. 7Zijt niet wijs in uw ogen; vrees den HEERE, en wijk van het kwade. 8Het zal een medicijn voor uw navel zijn, en een bevochtiging voor uw beenderen. 9Vereer den HEERE van uw goed, en van de eerstelingen al uwer inkomsten; 10Zo zullen uw schuren met overvloed vervuld worden, en uw perskuipen van most overlopen. 11Mijn zoon! verwerp de tucht des HEEREN niet, en wees niet verdrietig over Zijn kastijding; 12Want de HEERE kastijdt dengene, dien Hij liefheeft, ja, gelijk een vader den zoon, in denwelken hij een welbehagen heeft. 13Welgelukzalig is de mens, die wijsheid vindt, en de mens, die verstandigheid voortbrengt! 14Want haar koophandel is beter dan de koophandel van zilver, en haar inkomst dan het uitgegraven goud. 15Zij is kostelijker dan robijnen en al; wat u lusten mag, is met haar niet te vergelijken. 16Langheid der dagen is in haar rechterhand, in haar linkerhand rijkdom en eer. 17Haar wegen zijn wegen der liefelijkheid, en al haar paden vrede. 18Zij is een boom des levens dengenen, die ze aangrijpen, en elkeen, die ze vasthoudt, wordt gelukzalig. 19De HEERE heeft de aarde door wijsheid gegrond, de hemelen door verstandigheid bereid. 20Door Zijn wetenschap zijn de afgronden gekloofd, en de wolken druipen dauw. 21Mijn zoon! laat ze niet afwijken van uw ogen; bewaar de bestendige wijsheid en bedachtzaamheid. 22Want zij zullen het leven voor uw ziel zijn, en een aangenaamheid voor uw hals. 23Dan zult gij uw weg zeker wandelen, en gij zult uw voet niet stoten. 24Zo gij nederligt, zult gij niet schrikken; maar gij zult nederliggen en uw slaap zal zoet wezen. 25Vrees niet voor haastigen schrik, noch voor de verwoesting der goddelozen, als zij komt. 26Want de HEERE zal met uw hoop wezen, en Hij zal uw voet bewaren van gevangen te worden. 27Onthoud het goed van zijn meesters niet, als het in het vermogen uwer hand is te doen. 28Zeg niet tot uw naaste: Ga heen, en kom weder, en morgen zal ik geven, dewijl het bij u is. 29Smeed geen kwaad tegen uw naaste, aangezien hij met vertrouwen bij u woont. 30Twist met een mens niet zonder oorzaak, zo hij u geen kwaad gedaan heeft. 31Zijt niet nijdig over een man des gewelds, en verkies geen van zijn wegen. 32Want de afwijker is den HEERE een gruwel; maar Zijn verborgenheid is met den oprechte. 33De vloek des HEEREN is in het huis des goddelozen; maar de woning der rechtvaardigen zal Hij zegenen. 34Zekerlijk, de spotters zal Hij bespotten, maar den zachtmoedigen zal Hij genade geven. 35De wijzen zullen eer beerven; maar elkeen der zotten neemt schande op zich.
Bonyeza Enter ili kuuwekea mstari huu rangi, kuandika maelezo au kuunakili. Vitufe vya mishale vinakupeleka kwenye mstari unaofuata.
Namba za mistari hufuata tafsiri uliyochagua, na katika sura chache zinaweza kutofautiana kwa mstari mmoja.