1Sikilizeni wanangu, mafundisho ya baba yenu; sikilizeni kwa makini na mpate ufahamu. 2Ninawapa mafundisho ya maana, kwa hiyo msiyaache mafundisho yangu. 3Nilipokuwa mvulana mdogo katika nyumba ya baba yangu, ningali mchanga na mtoto pekee kwa mama yangu, 4baba alinifundisha akisema, “Yashike maneno yangu yote kwa moyo wako wote; yashike maagizo yangu na wewe utaishi. 5Pata hekima, pata ufahamu; usiyasahau maneno yangu wala usiyaache. 6Usimwache hekima naye atakuweka salama; mpende, naye atakulinda. 7Hekima ni bora kuliko vitu vyote; kwa hiyo jipe hekima. Hata ikikugharimu vyote ulivyo navyo, pata ufahamu. 8Mstahi, naye atakukweza; mkumbatie, naye atakuheshimu. 9Atakuvika shada la neema kichwani mwako na kukupa taji ya utukufu.” 10Sikiliza mwanangu, kubali ninachokuambia, nayo miaka ya maisha yako itakuwa mingi. 11Ninakuongoza katika njia ya hekima na kukuongoza katika mapito yaliyonyooka. 12Utembeapo, hatua zako hazitazuiliwa; ukimbiapo, hutajikwaa. 13Mkamate sana elimu, usimwache aende zake; mshike, maana yeye ni uzima wako. 14Usiuweke mguu wako katika njia ya waovu wala usitembee katika njia ya watu wabaya. 15Epukana nayo, usisafiri katika njia hiyo; achana nayo, na uelekee njia yako. 16Kwa kuwa hawawezi kulala mpaka watende uovu; wanashindwa hata kusinzia mpaka wamwangushe mtu. 17Wanakula mkate wa uovu, na kunywa mvinyo wa jeuri. 18Njia ya wenye haki ni kama nuru ya kwanza ya mapambazuko, ambayo hungʼaa zaidi na zaidi mpaka mchana mkamilifu. 19Lakini njia ya waovu ni kama giza nene; hawajui kinachowafanya wajikwae. 20Mwanangu, yasikilize kwa makini yale ninayokuambia; sikiliza kwa makini maneno yangu. 21Usiruhusu yaondoke machoni pako, yahifadhi ndani ya moyo wako; 22kwa sababu ni uzima kwa wale wanaoyapata na afya kwa mwili wote wa mwanadamu. 23Zaidi ya yote, linda moyo wako, kuliko yote uyalindayo, maana ndiko zitokako chemchemi za uzima. 24Epusha kinywa chako na ukaidi; weka mazungumzo machafu mbali na midomo yako. 25Macho yako na yatazame mbele, kaza macho yako moja kwa moja mbele yako. 26Sawazisha mapito ya miguu yako na njia zako zote ziwe zimethibitika. 27Usigeuke kulia wala kushoto; epusha mguu wako na ubaya.
1Listen, sons, to a father’s instruction. Pay attention and know understanding; 2for I give you sound learning. Don’t forsake my law. 3For I was a son to my father, tender and an only child in the sight of my mother. 4He taught me, and said to me: “Let your heart retain my words. Keep my commandments, and live. 5Get wisdom. Get understanding. Don’t forget, neither swerve from the words of my mouth. 6Don’t forsake her, and she will preserve you. Love her, and she will keep you. 7Wisdom is supreme. Get wisdom. Yes, though it costs all your possessions, get understanding. 8Esteem her, and she will exalt you. She will bring you to honor, when you embrace her. 9She will give to your head a garland of grace. She will deliver a crown of splendor to you.” 10Listen, my son, and receive my sayings. The years of your life will be many. 11I have taught you in the way of wisdom. I have led you in straight paths. 12When you go, your steps will not be hampered. When you run, you will not stumble. 13Take firm hold of instruction. Don’t let her go. Keep her, for she is your life. 14Don’t enter into the path of the wicked. Don’t walk in the way of evil men. 15Avoid it, and don’t pass by it. Turn from it, and pass on. 16For they don’t sleep, unless they do evil. Their sleep is taken away, unless they make someone fall. 17For they eat the bread of wickedness, and drink the wine of violence. 18But the path of the righteous is like the dawning light, that shines more and more until the perfect day. 19The way of the wicked is like darkness. They don’t know what they stumble over. 20My son, attend to my words. Turn your ear to my sayings. 21Let them not depart from your eyes. Keep them in the midst of your heart. 22For they are life to those who find them, and health to their whole body. 23Keep your heart with all diligence, for out of it is the wellspring of life. 24Put away from yourself a perverse mouth. Put corrupt lips far from you. 25Let your eyes look straight ahead. Fix your gaze directly before you. 26Make the path of your feet level. Let all of your ways be established. 27Don’t turn to the right hand nor to the left. Remove your foot from evil.
1Hoort, gij kinderen! de tucht des vaders, en merkt op, om verstand te weten. 2Dewijl ik ulieden goede leer geve, verlaat mijn wet niet. 3Want ik was mijns vaders zoon, teder, en een enige voor het aangezicht mijner moeder. 4Hij nu leerde mij, en zeide tot mij: Uw hart houde mijn woorden vast, onderhoud mijn geboden, en leef. 5Verkrijg wijsheid, verkrijg verstand; vergeet niet, en wijk niet van de redenen mijns monds. 6Verlaat ze niet, en zij zal u behoeden; heb ze lief, en zij zal u bewaren. 7De wijsheid is het voornaamste; verkrijg dan wijsheid, en verkrijg verstand met al uw bezitting. 8Verhef ze, en zij zal u verhogen; zij zal u vereren, als gij haar omhelzen zult. 9Zij zal uw hoofd een aangenaam toevoegsel geven, een sierlijke kroon zal zij u leveren. 10Hoor, mijn zoon! en neem mijn redenen aan, en de jaren des levens zullen u vermenigvuldigd worden. 11Ik onderwijs u in den weg der wijsheid; ik doe u treden in de rechte sporen. 12In uw gaan zal uw tred niet benauwd worden, en indien gij loopt, zult gij niet struikelen. 13Grijp de tucht aan, laat niet af; bewaar ze, want zij is uw leven. 14Kom niet op het pad der goddelozen, en treed niet op den weg der bozen. 15Verwerp dien, ga er niet door; wijk er van, en ga voorbij. 16Want zij slapen niet, zo zij geen kwaad gedaan hebben; en hun slaap wordt weggenomen, zo zij niet iemand hebben doen struikelen. 17Want zij eten brood der goddeloosheid, en drinken wijn van enkel geweld. 18Maar het pad der rechtvaardigen is gelijk een schijnend licht, voortgaande en lichtende tot den vollen dag toe. 19De weg der goddelozen is als donkerheid, zij weten niet, waarover zij struikelen zullen. 20Mijn zoon! merk op mijn woorden, neig uw oor tot mijn redenen. 21Laat ze niet wijken van uw ogen, behoud ze in het midden uws harten. 22Want zij zijn het leven dengenen, die ze vinden, en een medicijn voor hun gehele vlees. 23Behoed uw hart boven al wat te bewaren is, want daaruit zijn de uitgangen des levens. 24Doe de verkeerdheid des monds van u weg, en doe de verdraaidheid der lippen verre van u. 25Laat uw ogen rechtuit zien, en uw oogleden zich recht voor u heen houden. 26Weeg den gang uws voets, en laat al uw wegen wel gevestigd zijn. 27Wijk niet ter rechter hand of ter linkerhand, wend uw voet af van het kwade.
Bonyeza Enter ili kuuwekea mstari huu rangi, kuandika maelezo au kuunakili. Vitufe vya mishale vinakupeleka kwenye mstari unaofuata.
Namba za mistari hufuata tafsiri uliyochagua, na katika sura chache zinaweza kutofautiana kwa mstari mmoja.