Tafuta
Matokeo ya “nuru”
Mistari 191 imepatikana katika Neno: Bibilia Takatifu.
- Mwanzo 1:3Mungu akasema, “Iwepo nuru,” nayo nuru ikawepo.
- Mwanzo 1:4Mungu akaona ya kuwa nuru ni njema, ndipo Mungu akatenganisha nuru na giza.
- Mwanzo 1:5Mungu akaiita nuru “mchana,” na giza akaliita “usiku.” Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya kwanza.
- Mwanzo 1:15nayo iwe mianga kwenye nafasi ya anga ya kutia nuru juu ya dunia.” Ikawa hivyo.
- Mwanzo 1:18itawale usiku na mchana, na ikatenganishe nuru na giza. Mungu akaona kuwa hili ni jema.
- Mwanzo 15:17Wakati jua lilipokuwa limezama na giza limeingia, tanuru la moshi na mwali wa moto unaowaka vikatokea na kupita kati ya vile vipande vya nyama.
- Mwanzo 19:28Akatazama upande wa Sodoma na Gomora, kuelekea nchi yote ya tambarare, akaona moshi mzito ukipanda kutoka kwenye nchi, kama moshi utokao kwenye tanuru.
- Kutoka 9:8Kisha Bwana akamwambia Mose na Aroni, “Chukueni majivu ya tanuru, naye Mose ayarushe angani mbele ya Farao.
- Kutoka 9:10Basi wakachukua majivu kwenye tanuru na kusimama mbele ya Farao. Mose akayarusha hewani, nayo majipu yenye kufura yakatokea miilini mwa watu na wanyama.
- Kutoka 14:20ikakaa kati ya majeshi ya Misri na Israeli. Usiku kucha wingu likaleta giza upande mmoja na nuru kwa upande mwingine, kwa hiyo hakuna aliyemkaribia mwenzake usiku kucha.
- Kutoka 19:18Mlima Sinai ulikuwa umefunikwa na moshi, kwa sababu Bwana alishuka juu yake katika moto. Moshi wa moto huo ulipanda juu kama moshi kutoka kwenye tanuru kubwa na mlima wote ukatetemeka kwa nguvu nyingi,
- Mambo ya Walawi 26:26Nitakapowaondolea upatikanaji wa mkate wenu, wanawake kumi wataoka mkate wenu katika tanuru moja, nao wataugawa mkate kidogo kwa kupima. Mtakula, lakini hamtashiba.
- Hesabu 4:9“Watachukua kitambaa cha buluu na kufunika kinara cha taa kilicho kwa ajili ya nuru, pamoja na taa zake, mikasi yake, sinia zake, magudulia yake yote yaliyotumika kuwekea mafuta.
- Hesabu 6:25Bwana akuangazie nuru ya uso wake na kukufadhili;
- Kumbukumbu la Torati 4:20Lakini kwenu ninyi, Bwana amewatoa kutoka kwenye tanuru ya kuyeyushia chuma, katika Misri kuwa watu wa urithi wake kama mlivyo sasa.
- 1 Wafalme 3:21Asubuhi yake, nikaamka ili kumnyonyesha mwanangu, naye alikuwa amekufa! Lakini nilipomwangalia sana katika nuru ya asubuhi, niliona kuwa hakuwa yule mwana niliyekuwa nimemzaa.”
- 1 Wafalme 8:51kwa maana ni watu wako na urithi wako, uliowatoa Misri, kutoka kwenye lile tanuru la kuyeyushia chuma.
- Nehemia 3:11Malkiya mwana wa Harimu, na Hashubu mwana wa Pahath-Moabu walikarabati sehemu nyingine pamoja na Mnara wa Matanuru.
- Nehemia 12:38Kundi la pili la waimbaji lilielekea upande wa kushoto. Niliwafuata juu ya ukuta, pamoja na nusu ya watu kupitia Mnara wa Tanuru mpaka kwenye Ukuta Mpana,
- Ayubu 3:4Siku ile na iwe giza; Mungu juu na asiiangalie; nayo nuru isiiangazie.
- Ayubu 3:5Giza na kivuli kikuu kiikalie tena; wingu na likae juu yake; weusi na uifunike nuru yake.
- Ayubu 3:20“Mbona nuru inawaangazia wale walio taabuni, na hao wenye uchungu kupewa uhai,
- Ayubu 10:22nchi ya giza kuu sana, yenye uvuli wa giza na machafuko, mahali ambapo hata nuru ni giza.”
- Ayubu 12:22Hufunua mambo ya ndani ya gizani, na kuyaleta nuruni yale yaliyositirika sana.
- Ayubu 18:18Ameondolewa nuruni na kusukumiwa gizani, naye amefukuzwa mbali atoke duniani.
- Ayubu 24:13“Wako wale wanaoiasi nuru, wasiofahamu njia zake wala hawakai katika mapito yake.
- Ayubu 24:16Katika giza, huvunja majumba, lakini wakati wa mchana hujifungia ndani; hawataki kufanya lolote nuruni.
- Ayubu 25:3Je, majeshi yake yaweza kuhesabika? Ni nani asiyeangaziwa na nuru yake?
- Ayubu 26:10Amechora mstari wa upeo juu ya uso wa maji, ameweka mpaka wa nuru na giza.
- Ayubu 28:11Hutafuta vyanzo vya mito na kuvileta vitu vilivyofichika katika nuru.
- Ayubu 29:24Walipokata tamaa niliwaonyesha uso wa furaha; nuru ya uso wangu ilikuwa ya thamani kwao.
- Ayubu 30:26Lakini nilipotazamia mema, mabaya yalinijia; nilipotafuta nuru, ndipo giza lilipokuja.
- Ayubu 33:30ili aigeuze nafsi yake toka shimoni, ili nuru ya uzima imwangazie.
- Ayubu 38:15Waovu huzuiliwa nuru yao, nao mkono wao ulioinuliwa huvunjwa.
- Ayubu 38:19“Njia ya kufika kwenye makao ya nuru ni ipi? Nako maskani mwa giza ni wapi?
- Zaburi 4:6Wengi wanauliza, “Ni nani awezaye kutuonyesha jema lolote?” Ee Bwana, tuangazie nuru ya uso wako.
- Zaburi 12:6Maneno ya Bwana ni safi, kama fedha iliyosafishwa katika tanuru, iliyosafishwa mara saba.
- Zaburi 13:3Nitazame, unijibu, Ee Bwana Mungu wangu. Yatie nuru macho yangu, ama sivyo nitalala usingizi wa mauti.
- Zaburi 19:8Maagizo ya Bwana ni kamili, nayo hufurahisha moyo. Amri za Bwana huangaza, zatia nuru machoni.
- Zaburi 21:9Wakati utakapojitokeza utawafanya kama tanuru ya moto. Katika ghadhabu yake Bwana atawameza, moto wake utawateketeza.
- Zaburi 27:1Bwana ni nuru yangu na wokovu wangu, nimwogope nani? Bwana ni ngome ya uzima wangu, nimhofu nani?
- Zaburi 34:5Wale wamtazamao hutiwa nuru, nyuso zao hazifunikwi na aibu kamwe.
- Zaburi 36:9Kuwa pamoja nawe ni kijito cha uzima, katika nuru yako twaona nuru.
- Zaburi 43:3Tuma hima nuru yako na kweli yako na viniongoze; vinilete mpaka mlima wako mtakatifu, mpaka mahali unapoishi.
- Zaburi 44:3Sio kwa upanga wao waliipata nchi, wala si mkono wao uliwapatia ushindi; ilikuwa ni kitanga cha mkono wako wa kuume, na nuru ya uso wako, kwa kuwa uliwapenda.
- Zaburi 49:19atajiunga na kizazi cha baba zake, ambao hawataona kamwe nuru ya uzima.
- Zaburi 56:13Kwa kuwa umeniokoa toka kwenye mauti na miguu yangu kwenye kujikwaa, ili niweze kuenenda mbele za Mungu katika nuru ya uzima.
- Zaburi 67:1Mungu aturehemu na kutubariki, na kutuangazia nuru za uso wake,
- Zaburi 78:14Aliwaongoza kwa wingu mchana na kwa nuru kutoka kwenye moto usiku kucha.
- Zaburi 88:9nuru ya macho yangu imefifia kwa ajili ya huzuni. Ee Bwana, ninakuita kila siku, ninakunyooshea wewe mikono yangu.
Tunaonyesha 50 ya kwanza. Fanya utafutaji wako uwe mahususi zaidi ili upate matokeo machache.
Vifungu vilivyoelezwa
Mistari hii ina maelezo kamili: muktadha, tabaka tatu na wakati wa familia.
- Zaburi 23:1De HEER is mijn herder, ook in het donkere dalA song about God who cares, like a shepherd for his sheep.
- Yeremia 29:11Plannen voor vrede, na zeventig jaarPeople far from home receive a letter full of hope.
- Mathayo 7:1Oordeel niet: eerst de balk, dan de splinterJesus tells a funny story about a plank in your eye.
- Luka 15:20De vader die rent: een verhaal met een open eindeA son comes home, and his father runs to meet him.
- Yohana 3:16Zo lief had God de wereld: een nachtelijk gesprekA man comes to Jesus at night with his questions.
- Warumi 8:28Alles werkt mee ten goede, midden in het zuchtenWhen everything is hard, God sighs along with us.
- Wafilipi 4:13Alles aankunnen: tevreden in gebrek en overvloedPaul is in prison, and still he is happy.