1“Kwa nini Mwenyezi asiweke nyakati kwa ajili ya hukumu? Kwa nini wale wamjuao wazitafute siku kama hizo bila mafanikio? 2Watu husogeza mawe ya mpaka; huchunga makundi ya wanyama waliyonyangʼanya kwa nguvu. 3Huwanyangʼanya yatima punda wao, na kumchukua rehani fahali wa mjane. 4Humsukuma mhitaji kutoka njia, na kuwafanya maskini wote wa nchi kulazimika kujificha. 5Kama punda-mwitu jangwani, maskini huzunguka katika kazi zao za kutafuta chakula; mahali palipo jangwa huwapa chakula cha watoto wao. 6Hukusanya chakula mashambani na kuokota masazo katika mashamba ya mizabibu ya waovu. 7Kwa kukosa nguo, usiku kucha hukaa uchi; hawana chochote cha kujifunika baridi. 8Hutota kwa mvua za mlimani, nao huikumbatia miamba kwa ajili ya kukosa pa kujisitiri. 9Mtoto yatima hupokonywa matitini; mtoto wachanga wa maskini hunyakuliwa kwa ajili ya deni. 10Kwa kukosa nguo, hutembea uchi; hubeba miganda ya ngano, lakini huwa na njaa. 11Hukamua zeituni katika mawe ya kusagia; hukanyaga mashinikizo, lakini wanaona kiu. 12Kilio cha huzuni cha wanaokufa kinapaa kutoka mjini, nazo nafsi za waliojeruhiwa zinalilia msaada. Lakini Mungu hamlaumu mtu yeyote kwa kutenda mabaya. 13“Wako wale wanaoiasi nuru, wasiofahamu njia zake wala hawakai katika mapito yake. 14Wakati mwanga wa mchana unapotoweka, muuaji huinuka naye huwaua maskini na mhitaji; wakati wa usiku hunyemelea kama mwizi. 15Jicho la mzinzi hungojea wakati wa giza, naye hufikiri, ‘Hakuna jicho litakaloniona,’ naye huuficha uso wake. 16Katika giza, huvunja majumba, lakini wakati wa mchana hujifungia ndani; hawataki kufanya lolote nuruni. 17Kwa wote hawa, giza nene ndiyo asubuhi yao; hujifanya rafiki na vitisho vya gizani. 18“Lakini wao ni povu juu ya maji; sehemu yao juu ya nchi imelaaniwa, hivyo hakuna hata mmoja aendaye kwenye shamba la mizabibu. 19Kama vile joto na hari vinyakuavyo theluji iliyoyeyuka, ndivyo kuzimu kuwanyakuavyo waliotenda dhambi. 20Tumbo lililowazaa huwasahau, nao huwa karamu ya mabuu; watu waovu hawakumbukwi tena, lakini huvunjika kama mti. 21Huwafanya mawindo wanawake tasa na wasio na watoto, nao hawaonyeshi huruma kwa wajane. 22Lakini Mungu huwakokota wenye nguvu kwa uwezo wake; ingawa wamestawi, hawana hakika ya maisha. 23Aweza akawaacha wakapumzika wakijihisi salama, lakini macho yake yanaona njia zao. 24Kwa kitambo kidogo hutukuka, hatimaye hutoweka; hushushwa na kukusanywa kama wengine wote, hukatwa kama masuke ya nafaka. 25“Kama hili sivyo, ni nani awezaye kunithibitisha kuwa mwongo, na kuyafanya maneno yangu kuwa si kitu?”
1“Why aren’t times laid up by the Almighty? Why don’t those who know him see his days? 2There are people who remove the landmarks. They violently take away flocks, and feed them. 3They drive away the donkey of the fatherless, and they take the widow’s ox for a pledge. 4They turn the needy out of the way. The poor of the earth all hide themselves. 5Behold, as wild donkeys in the desert, they go out to their work, seeking diligently for food. The wilderness yields them bread for their children. 6They cut their provender in the field. They glean the vineyard of the wicked. 7They lie all night naked without clothing, and have no covering in the cold. 8They are wet with the showers of the mountains, and embrace the rock for lack of a shelter. 9There are those who pluck the fatherless from the breast, and take a pledge of the poor, 10So that they go around naked without clothing. Being hungry, they carry the sheaves. 11They make oil within the walls of these men. They tread wine presses, and suffer thirst. 12From out of the populous city, men groan. The soul of the wounded cries out, yet God doesn’t regard the folly. 13“These are of those who rebel against the light. They don’t know its ways, nor stay in its paths. 14The murderer rises with the light. He kills the poor and needy. In the night he is like a thief. 15The eye also of the adulterer waits for the twilight, saying, ‘No eye shall see me.’ He disguises his face. 16In the dark they dig through houses. They shut themselves up in the daytime. They don’t know the light. 17For the morning is to all of them like thick darkness, for they know the terrors of the thick darkness. 18“They are foam on the surface of the waters. Their portion is cursed in the earth. They don’t turn into the way of the vineyards. 19Drought and heat consume the snow waters, so does Sheol those who have sinned. 20The womb shall forget him. The worm shall feed sweetly on him. He shall be no more remembered. Unrighteousness shall be broken as a tree. 21He devours the barren who don’t bear. He shows no kindness to the widow. 22Yet God preserves the mighty by his power. He rises up who has no assurance of life. 23God gives them security, and they rest in it. His eyes are on their ways. 24They are exalted; yet a little while, and they are gone. Yes, they are brought low, they are taken out of the way as all others, and are cut off as the tops of the ears of grain. 25If it isn’t so now, who will prove me a liar, and make my speech worth nothing?”
1Waarom zouden van den Almachtige de tijden niet verborgen zijn, dewijl zij, die Hem kennen, Zijn dagen niet zien? 2Zij tasten de landpalen aan; de kudden roven zij, en weiden ze. 3Den ezel der wezen drijven zij weg; den os ener weduwe nemen zij te pand. 4Zij doen de nooddruftigen wijken van den weg; te zamen versteken zich de ellendigen des lands. 5Ziet, zij zijn woudezels in de woestijn; zij gaan uit tot hun werk, makende zich vroeg op ten roof; het vlakke veld is hem tot spijs, en den jongeren. 6Op het veld maaien zij zijn voeder, en den wijnberg des goddelozen lezen zij af. 7Den naakten laten zij vernachten zonder kleding, die geen deksel heeft tegen de koude. 8Van den stroom der bergen worden zij nat, en zonder toevlucht zijnde, omhelzen zij de steenrotsen. 9Zij rukken het weesje van de borst, en dat over den arme is, nemen zij te pand. 10Den naakte doen zij weggaan zonder kleed, en hongerig, die garven dragen. 11Tussen hun muren persen zij olie uit, treden de wijnpersen, en zijn dorstig. 12Uit de stad zuchten de lieden, en de ziel der verwonden schreeuwt uit; nochtans beschikt God niets ongerijmds. 13Zij zijn onder de wederstrevers des lichts; zij kennen Zijn wegen niet, en zij blijven niet op Zijn paden. 14Met het licht staat de moorder op, doodt den arme en den nooddruftige; en des nachts is hij als een dief. 15Ook neemt het oog des overspelers de schemering waar, zeggende: Geen oog zal mij zien; en hij legt een deksel op het aangezicht. 16In de duisternis doorgraaft hij de huizen, die zij zich des daags afgetekend hadden; zij kennen het licht niet. 17Want de morgenstond is hun te zamen de schaduw des doods; als men hen kent, zijn zij in de strikken van des doods schaduw. 18Hij is licht op het vlakke der wateren; vervloekt is hun deel op de aarde; hij wendt zich niet tot den weg der wijngaarden. 19De droogte mitsgaders de hitte nemen de sneeuwwateren weg; alzo het graf dergenen, die gezondigd hebben. 20De baarmoeder vergeet hem, het gewormte is hem zoet, zijns wordt niet meer gedacht; en het onrecht wordt gebroken als een hout. 21De onvruchtbare, die niet baart, teert hij af, en aan de weduwe doet hij niets goeds. 22Ook trekt hij de machtigen door zijn kracht; staat hij op, zo is men des levens niet zeker. 23Stelt hem God in gerustigheid, zo steunt hij daarop; nochtans zijn Zijn ogen op hun wegen. 24Zij zijn een weinig tijds verheven, daarna is er niemand van hen; zij worden nedergedrukt; gelijk alle anderen worden zij besloten; en gelijk de top ener aar worden zij afgesneden. 25Indien het nu zo niet is, wie zal mij leugenachtig maken, en mijn rede tot niet brengen?
Bonyeza Enter ili kuuwekea mstari huu rangi, kuandika maelezo au kuunakili. Vitufe vya mishale vinakupeleka kwenye mstari unaofuata.
Namba za mistari hufuata tafsiri uliyochagua, na katika sura chache zinaweza kutofautiana kwa mstari mmoja.