Ruka hadi kwenye maudhui
Beta

Uzi bado haujatafsiriwa kikamilifu kwa Kiswahili. Kile ambacho bado hakijatafsiriwa kinaonyeshwa kwa Kiingereza.

Tafuta

Matokeo ya “neema”

Mistari 162 imepatikana katika Neno: Bibilia Takatifu.

  1. Mwanzo 33:5Esau akainua macho akawaona wale wanawake na watoto. Akauliza, “Hawa uliofuatana nao ni nani?” Yakobo akamjibu, “Ni watoto ambao Mungu amempa mtumishi wako kwa neema.”
  2. Mwanzo 41:29Miaka saba ya neema inakuja katika nchi yote ya Misri,
  3. Mwanzo 41:30lakini itafuata miaka saba ya njaa. Ndipo neema yote ya Misri itasahaulika na njaa itaikumba nchi.
  4. Mwanzo 41:31“Neema iliyokuwa katika nchi haitakumbukwa, kwa sababu njaa itakayofuata itakuwa kali mno.
  5. Mwanzo 41:34Farao na aweke wenye amri nchini kote wakusanye sehemu ya tano ya mavuno ya Misri katika miaka hii saba ya neema.
  6. Mwanzo 41:35Wakusanye chakula chote katika miaka hii saba ya neema inayokuja na kuhifadhi nafaka chini ya mamlaka ya Farao, iwe akiba ya chakula katika miji.
  7. Mwanzo 41:47Katika ile miaka saba ya neema nchi ilizaa mazao kwa wingi sana.
  8. Mwanzo 41:48Yosefu akakusanya chakula chote kilichozalishwa katika ile miaka saba ya neema nchini Misri, akakihifadhi katika ghala za miji. Katika kila mji kulihifadhiwa chakula kilichozalishwa katika mashamba yaliyouzunguka mji huo.
  9. Mwanzo 41:53Ile miaka saba ya neema huko Misri ikaisha,
  10. Kutoka 34:6Bwana akapita mbele ya Mose, akitangaza, “Bwana, Bwana, Mungu mwenye huruma na neema, asiye mwepesi wa hasira, mwingi wa upendo na uaminifu,
  11. 1 Samweli 2:21Bwana akawa mwenye neema kwa Hana, naye akapata mimba akazaa wana watatu na binti wawili. Wakati huo, kijana Samweli akaendelea kukua mbele za Bwana.
  12. 2 Mambo ya Nyakati 30:9Kama mkimrudia Bwana ndipo wale ndugu zenu waliotekwa pamoja na watoto wenu watakapoonewa huruma na wale waliowateka na kuwaachia warudi katika nchi hii, kwa kuwa Bwana Mungu wenu ni mwenye neema na huruma, hatageuzia uso wake mbali nanyi kama ninyi mkimrudia yeye.”
  13. Ezra 7:9Ezra alianza safari yake kutoka Babeli tangu siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza, naye akawasili Yerusalemu siku ya kwanza ya mwezi wa tano, kwa maana mkono wa neema wa Mungu wake ulikuwa juu yake.
  14. Ezra 8:18Kwa sababu mkono wa neema wa Mungu wetu ulikuwa juu yetu, walituletea Sherebia, mtu mwenye uwezo kutoka wazao wa Mahli mwana wa Lawi, mwana wa Israeli, na wana wa Sherebia pamoja na ndugu zao wanaume kumi na wanane.
  15. Ezra 8:22Niliona aibu kumwomba mfalme askari na wapanda farasi wa kutulinda njiani kutokana na adui zetu, kwa sababu tulikwisha kumwambia mfalme, “Mkono wa neema wa Mungu wetu uko juu ya kila mmoja anayemtafuta, lakini hasira yake kubwa ni dhidi ya wote wamwachao.”
  16. Ezra 9:8“Lakini sasa, kwa muda mfupi, Bwana Mungu wetu amekuwa na neema kwa kutuachia mabaki na kutupa mahali imara katika mahali pake patakatifu, hivyo Mungu wetu atupa mwanga machoni petu na unafuu katika utumwa wetu.
  17. Nehemia 2:8Naomba nipewe barua nipeleke kwa Asafu, mtunzaji wa msitu wa mfalme, ili anipe miti ya kutengeneza boriti kwa ajili ya malango ya ngome ya Hekalu, na ukuta wa mji, na makao yangu nitakapoishi.” Kwa kuwa mkono wenye neema wa Mungu wangu ulikuwa juu yangu, mfalme akanijalia ombi langu.
  18. Nehemia 2:18Pia niliwaambia kuhusu mkono wenye neema wa Mungu wangu uliokuwa juu yangu, na kile mfalme alichokuwa ameniambia. Wakajibu, “Haya! Tuanze kujenga tena.” Kwa hiyo wakaanza kazi hii njema.
  19. Nehemia 9:17Wakakataa kusikiliza na kushindwa kukumbuka miujiza uliyoifanya miongoni mwao. Wakawa na shingo ngumu, na katika uasi wao wakamchagua kiongozi ili warudi kwenye utumwa wao. Lakini wewe ni Mungu mwenye kusamehe, mwenye neema na mwingi wa huruma, si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa upendo. Kwa hiyo hukuwaacha,
  20. Nehemia 9:31Lakini kwa rehema zako kuu hukuwakomesha wala kuwaacha, kwa kuwa wewe ni Mungu mwenye neema na rehema.
  21. Zaburi 45:2Wewe ni bora kuliko watu wengine wote na midomo yako imepakwa neema, kwa kuwa Mungu amekubariki milele.
  22. Zaburi 86:15Lakini wewe, Ee Bwana, ni Mungu wa huruma na neema, si mwepesi wa hasira, bali ni mwingi wa upendo na uaminifu.
  23. Zaburi 103:8Bwana ni mwingi wa huruma na mwenye neema; si mwepesi wa hasira, bali amejaa upendo.
  24. Zaburi 111:4Amefanya maajabu yake yakumbukwe, Bwana ni mwenye neema na huruma.
  25. Zaburi 116:5Bwana ni mwenye neema na haki, Mungu wetu ni mwingi wa huruma.
  26. Zaburi 119:29Niepushe na njia za udanganyifu, kwa neema unifundishe sheria zako.
  27. Zaburi 145:8Bwana ni mwenye neema na mwingi wa huruma, si mwepesi wa hasira, bali ni mwingi wa upendo.
  28. Mithali 1:9Hayo yatakuwa taji la maua la neema kichwani pako, na mkufu wa kuipamba shingo yako.
  29. Mithali 3:22ndipo vitakapokuwa uzima nafsini mwako na pambo la neema shingoni mwako.
  30. Mithali 3:34Huwadhihaki wale wanaodhihaki, lakini huwapa neema wale wanyenyekevu.
  31. Mithali 4:9Atakuvika shada la neema kichwani mwako na kukupa taji ya utukufu.”
  32. Mithali 22:11Yeye apendaye moyo safi na yeye ambaye maneno yake ni ya neema, mfalme atakuwa rafiki yake.
  33. Mhubiri 10:12Maneno yatokayo kinywani mwa mtu mwenye hekima yana neema, bali mpumbavu huangamizwa na midomo yake mwenyewe.
  34. Isaya 26:10Ingawa neema yaonyeshwa kwa waovu, hawajifunzi haki, hata katika nchi ya unyofu huendelea kutenda mabaya wala hawazingatii utukufu wa Bwana.
  35. Isaya 30:18Hata hivyo Bwana anatamani kutupatia neema, anainuka ili kuwaonyesha huruma. Kwa kuwa Bwana ni Mungu wa haki. Wamebarikiwa wote wanaomngojea yeye!
  36. Hosea 6:11“Pia kwa ajili yako, Yuda, mavuno yameamriwa. “Wakati wowote ningerejesha neema ya watu wangu,
  37. Hosea 14:2Chukueni maneno pamoja nanyi, mkamrudie Bwana. Mwambieni: “Samehe dhambi zetu zote na utupokee kwa neema, ili tuweze kutoa matunda yetu kama sadaka za mafahali.
  38. Yoeli 2:13Rarueni mioyo yenu na siyo mavazi yenu. Mrudieni Bwana, Mungu wenu, kwa maana yeye ndiye mwenye neema na mwingi wa huruma, si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa upendo, huona huruma, hujizuia kuleta maafa.
  39. Yoeli 3:1“Katika siku hizo na wakati huo, nitakaporejesha neema ya Yuda na Yerusalemu,
  40. Yona 2:8“Wale watu wanaongʼangʼana na sanamu zisizofaa hupoteza neema ile ambayo ingekuwa yao.
  41. Yona 4:2Akamwomba Bwana, “Ee Bwana, hili si lile nililolisema nilipokuwa ningali nyumbani? Hii ndiyo sababu niliharikisha kukimbilia Tarshishi. Nikifahamu kuwa wewe ni Mungu mwenye neema na huruma, si mwepesi wa hasira na umejaa upendo, ni Mungu ambaye hughairi katika kupeleka maafa.
  42. Zekaria 12:10“Nami nitamiminia nyumba ya Daudi na wakazi wa Yerusalemu roho ya neema na maombi. Watanitazama mimi, yule waliyemchoma. Nao watamwombolezea kama mtu anayemwombolezea mwanawe wa pekee na kusikitika kwa uchungu kama anayemsikitikia mzaliwa wake wa kwanza wa kiume.
  43. Malaki 1:9“Basi mwombeni Mungu awe na neema kwetu. Je, kwa sadaka kama hizo kutoka mikononi mwenu, atawapokea?” asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.
  44. Luka 2:40Naye yule mtoto akakua na kuongezeka nguvu, akiwa amejaa hekima, na neema ya Mungu ilikuwa juu yake.
  45. Luka 4:22Wote waliokuwako wakamsifu na kuyastaajabia maneno yake yaliyojaa neema, wakaulizana, “Je, huyu si mwana wa Yosefu?”
  46. Yohana 1:14Neno alifanyika mwili, akakaa miongoni mwetu, nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba, amejaa neema na kweli.
  47. Yohana 1:16Kutokana na ukamilifu wake, sisi sote tumepokea neema juu ya neema.
  48. Yohana 1:17Kwa kuwa sheria ilitolewa kwa mkono wa Mose, lakini neema na kweli imekuja kupitia Yesu Kristo.
  49. Matendo ya Mitume 4:33Mitume wakatoa ushuhuda wa kufufuka kwa Bwana Yesu kwa nguvu nyingi na neema ya Mungu ilikuwa juu yao wote.
  50. Matendo ya Mitume 6:8Stefano, akiwa amejaa neema na nguvu za Mungu, alifanya ishara na miujiza mikubwa miongoni mwa watu.

Tunaonyesha 50 ya kwanza. Fanya utafutaji wako uwe mahususi zaidi ili upate matokeo machache.

Urahisi wa kusoma

Chagua kinachokusaidia. Chaguo lako linahifadhiwa kwenye kifaa hiki.

Ukubwa wa maandishi

Unapendelea mipangilio ya kifaa chako mwenyewe (kukuza, kisoma skrini, hali ya giza)? Inafanya kazi hapa pia.