1Akiwa ndani ya tumbo la nyangumi, Yona alimwomba Bwana Mungu wake. 2Akasema: “Katika shida yangu nalimwita Bwana, naye akanijibu. Kutoka kina cha kaburi niliomba msaada, nawe ukasikiliza kilio changu. 3Ulinitupa kwenye kilindi, ndani kabisa ya moyo wa bahari, mikondo ya maji ilinizunguka, mawimbi yako yote na viwimbi vilipita juu yangu. 4Nikasema, ‘Nimefukuziwa mbali na uso wako, hata hivyo nitatazama tena kuelekea Hekalu lako takatifu.’ 5Maji yaliyonimeza yalinitisha, kilindi kilinizunguka; mwani ulijisokota kichwani pangu. 6Nilizama chini sana mpaka pande za mwisho za milima, makomeo ya hiyo nchi yalinifungia hata milele. Lakini uliuleta uhai wangu kutoka shimoni, Ee Bwana Mungu wangu. 7“Wakati uhai wangu ulipokuwa unatoka, nilikukumbuka wewe, Bwana, nayo maombi yangu yalikufikia wewe, katika Hekalu lako takatifu. 8“Wale watu wanaongʼangʼana na sanamu zisizofaa hupoteza neema ile ambayo ingekuwa yao. 9Lakini mimi, kwa wimbo wa shukrani, nitakutolea dhabihu. Lile nililowekea nadhiri nitalitimiza. Wokovu watoka kwa Bwana.” 10Basi Bwana akamwamuru yule nyangumi, naye akamtapika Yona katika nchi kavu.
1Then Jonah prayed to Yahweh, his God, out of the fish’s belly. 2He said, “I called because of my affliction to Yahweh. He answered me. Out of the belly of Sheol I cried. You heard my voice. 3For you threw me into the depths, in the heart of the seas. The flood was all around me. All your waves and your billows passed over me. 4I said, ‘I have been banished from your sight; yet I will look again toward your holy temple.’ 5The waters surrounded me, even to the soul. The deep was around me. The weeds were wrapped around my head. 6I went down to the bottoms of the mountains. The earth barred me in forever: yet have you brought up my life from the pit, Yahweh my God. 7“When my soul fainted within me, I remembered Yahweh. My prayer came in to you, into your holy temple. 8Those who regard lying vanities forsake their own mercy. 9But I will sacrifice to you with the voice of thanksgiving. I will pay that which I have vowed. Salvation belongs to Yahweh.” 10Yahweh spoke to the fish, and it vomited out Jonah on the dry land.
1En Jona bad tot den HEERE, zijn God, uit het ingewand van den vis. 2En hij zeide: Ik riep uit mijn benauwdheid tot den HEERE, en Hij antwoordde mij; uit den buik des grafs schreide ik, en Gij hoordet mijn stem. 3Want Gij hadt mij geworpen in de diepte, in het hart der zeeen, en de stroom omving mij; al Uw baren en Uw golven gingen over mij henen. 4En ik zeide: Ik ben uitgestoten van voor Uw ogen; nochtans zal ik den tempel Uwer heiligheid weder aanschouwen. 5De wateren hadden mij omgeven tot de ziel toe, de afgrond omving mij; het wier was aan mijn hoofd gebonden. 6Ik was nedergedaald tot de gronden der bergen; de grendelen der aarde waren om mij henen in eeuwigheid; maar Gij hebt mijn leven uit het verderf opgevoerd, o HEERE, mijn God! 7Als mijn ziel in mij overstelpt was, dacht ik aan den HEERE, en mijn gebed kwam tot U, in den tempel Uwer heiligheid. 8Die de valse ijdelheden onderhouden, verlaten hunlieder weldadigheid. 9Maar ik zal U offeren met de stem der dankzegging; wat ik beloofd heb, zal ik betalen. Het heil is des HEEREN. 10De HEERE nu sprak tot den vis; en hij spuwde Jona uit op het droge.
Bonyeza Enter ili kuuwekea mstari huu rangi, kuandika maelezo au kuunakili. Vitufe vya mishale vinakupeleka kwenye mstari unaofuata.
Namba za mistari hufuata tafsiri uliyochagua, na katika sura chache zinaweza kutofautiana kwa mstari mmoja.