1Bwana akamwambia Ayubu: 2“Je, mwenye kushindana na Mwenyezi aweza kumsahihisha? Mwenye kumlaumu Mungu na ajibu.” 3Ndipo Ayubu akamjibu Bwana: 4“Mimi sistahili kabisa: ninawezaje kukujibu wewe? Nauweka mkono wangu juu ya kinywa changu. 5Nimesema mara moja, lakini sina jibu; naam, nimesema mara mbili, lakini sitasema tena.” 6Ndipo Bwana akasema na Ayubu kutoka upepo wa kisulisuli: 7“Jikaze kama mwanaume; nitakuuliza maswali, nawe yakupasa unijibu. 8“Je, utabatilisha hukumu yangu? Utanilaumu mimi ili kujihesabia haki mwenyewe? 9Je, una mkono kama wa Mungu, nawe waweza kutoa sauti ya ngurumo kama yake? 10Basi jivike mwenyewe utukufu na fahari, nawe uvae heshima na enzi. 11Fungulia ukali wa ghadhabu yako, mtafute kila mwenye kiburi umshushe, 12mwangalie kila mtu mwenye kiburi na umnyenyekeze, waponde waovu mahali wasimamapo. 13Wazike wote mavumbini pamoja; wafunge nyuso zao kaburini. 14Ndipo mimi mwenyewe nitakukubalia kuwa mkono wako mwenyewe wa kuume unaweza kukuokoa. 15“Mwangalie mnyama aitwaye Behemothi, niliyemuumba kama nilivyokuumba wewe, anayekula majani kama ngʼombe. 16Tazama basi nguvu alizo nazo kwenye viuno vyake, uwezo alio nao kwenye misuli ya tumbo lake! 17Mkia wake hutikisika kama mwerezi; mishipa ya mapaja yake imesukwa pamoja. 18Mifupa yake ni bomba za shaba, maungo yake ni kama fito za chuma. 19Yeye ni wa kwanza miongoni mwa kazi za Mungu, lakini Muumba wake anaweza kumsogelea kwa upanga wake. 20Vilima humletea yeye mazao yake, nao wanyama wote wa porini hucheza karibu naye. 21Hulala chini ya mimea ya yungiyungi, katika maficho ya matete kwenye matope. 22Hiyo mimea ya yungiyungi humficha kwenye vivuli vyake; miti mirefu karibu na kijito humzunguka. 23Wakati mto ufurikapo, yeye hapati mshtuko wa hofu; yeye yu salama, hata kama Yordani ingefurika hadi kwenye kinywa chake. 24Je, mtu yeyote anaweza kumkamata yeye akiwa macho, au kumnasa kwa mtego na kutoboa pua yake?
1Moreover Yahweh answered Job, 2“Shall he who argues contend with the Almighty? He who argues with God, let him answer it.” 3Then Job answered Yahweh, 4“Behold, I am of small account. What shall I answer you? I lay my hand on my mouth. 5I have spoken once, and I will not answer; Yes, twice, but I will proceed no further.” 6Then Yahweh answered Job out of the whirlwind, 7“Now brace yourself like a man. I will question you, and you will answer me. 8Will you even annul my judgment? Will you condemn me, that you may be justified? 9Or do you have an arm like God? Can you thunder with a voice like him? 10“Now deck yourself with excellency and dignity. Array yourself with honor and majesty. 11Pour out the fury of your anger. Look at everyone who is proud, and bring him low. 12Look at everyone who is proud, and humble him. Crush the wicked in their place. 13Hide them in the dust together. Bind their faces in the hidden place. 14Then I will also admit to you that your own right hand can save you. 15“See now, behemoth, which I made as well as you. He eats grass as an ox. 16Look now, his strength is in his thighs. His force is in the muscles of his belly. 17He moves his tail like a cedar. The sinews of his thighs are knit together. 18His bones are like tubes of brass. His limbs are like bars of iron. 19He is the chief of the ways of God. He who made him gives him his sword. 20Surely the mountains produce food for him, where all the animals of the field play. 21He lies under the lotus trees, in the covert of the reed, and the marsh. 22The lotuses cover him with their shade. The willows of the brook surround him. 23Behold, if a river overflows, he doesn’t tremble. He is confident, though the Jordan swells even to his mouth. 24Shall any take him when he is on the watch, or pierce through his nose with a snare?
1En de HEERE antwoordde Job, en zeide: 2Is het twisten met den Almachtige onderrichten? Wie God bestraft, die antwoorde daarop. 3Toen antwoordde Job den HEERE, en zeide: 4Zie, ik ben te gering; wat zou ik U antwoorden? Ik leg mijn hand op mijn mond. 5Eenmaal heb ik gesproken, maar zal niet antwoorden; of tweemaal, maar zal niet voortvaren. 6En de HEERE antwoordde Job uit een onweder, en zeide: 7Gord nu als een man uw lenden; Ik zal u vragen, en onderricht Mij. 8Zult gij ook Mijn oordeel te niet maken? Zult Gij Mij verdoemen, opdat gij rechtvaardig zijt? 9Hebt gij een arm gelijk God? En kunt gij, gelijk Hij, met de stem donderen? 10Versier u nu met voortreffelijkheid en hoogheid, en bekleed u met majesteit en heerlijkheid! 11Strooi de verbolgenheden uws toorns uit, en zie allen hoogmoedige, en verneder hem! 12Zie allen hoogmoedige, en breng hem ten onder; en verpletter de goddelozen in hun plaats! 13Verberg hen te zamen in het stof; verbind hun aangezichten in het verborgen! 14Dan zal Ik ook u loven, omdat uw rechterhand u zal verlost hebben. 15Zie nu Behemoth, welken Ik gemaakt heb nevens u; hij eet hooi, gelijk een rund. 16Zie toch, zijn kracht is in zijn lenden, en zijn macht in den navel zijns buiks. 17Als het hem lust, zijn staart is als een ceder; de zenuwen zijner schaamte zijn doorvlochten. 18Zijn beenderen zijn als vast koper; zijn gebeenten zijn als ijzeren handbomen. 19Hij is een hoofdstuk der wegen Gods; die hem gemaakt heeft, heeft hem zijn zwaard aangehecht. 20Omdat de bergen hem voeder voortbrengen, daarom spelen al de dieren des velds aldaar. 21Onder schaduwachtige bomen ligt hij neder, in een schuilplaats des riets en des slijks. 22De schaduwachtige bomen bedekken hem, elkeen met zijn schaduw; de beekwilgen omringen hem. 23Zie, hij doet de rivier geweld aan, en verhaast zich niet; hij vertrouwt, dat hij de Jordaan in zijn mond zou kunnen intrekken. 24Zou men hem voor zijn ogen kunnen vangen? Zou men hem met strikken den neus doorboren kunnen?
Bonyeza Enter ili kuuwekea mstari huu rangi, kuandika maelezo au kuunakili. Vitufe vya mishale vinakupeleka kwenye mstari unaofuata.
Namba za mistari hufuata tafsiri uliyochagua, na katika sura chache zinaweza kutofautiana kwa mstari mmoja.