Ruka hadi kwenye maudhui
Beta

Uzi bado haujatafsiriwa kikamilifu kwa Kiswahili. Kile ambacho bado hakijatafsiriwa kinaonyeshwa kwa Kiingereza.

Ayubu 23

Sura hii ni sehemu ya: Gesprekken met de vrienden

1Ndipo Ayubu akajibu: 2“Hata leo malalamiko yangu ni chungu; mkono wake ni mzito juu yangu hata nikiugua. 3Laiti ningefahamu mahali pa kumwona; laiti ningeweza kwenda mahali akaapo! 4Ningeliweka shauri langu mbele zake, na kukijaza kinywa changu na hoja. 5Ningejua kwamba angenijibu nini, na kuelewa lile ambalo angelisema. 6Je, angenipinga kwa nguvu nyingi? La, asingenigandamiza. 7Hapo mtu mwadilifu angeweka shauri lake mbele zake, nami ningeokolewa milele na mhukumu wangu. 8“Lakini nikienda mashariki, hayupo; nikienda magharibi, simpati. 9Anapokuwa kazini pande za kaskazini, simwoni; akigeukia kusini, nako simwoni hata kidogo. 10Lakini anaijua njia niiendeayo; akiisha kunijaribu, nitatoka kama dhahabu. 11Nyayo zangu zimefuata hatua zake kwa karibu; nimeishika njia yake bila kukengeuka. 12Sijaziacha amri zilizotoka midomoni mwake; nimeyathamini maneno ya kinywa chake kuliko chakula changu cha kila siku. 13“Lakini yeye husimama peke yake; ni nani awezaye kumpinga? Yeye hufanya lolote atakalo. 14Hutimiliza maagizo yake dhidi yangu, na bado anayo mipango mingi kama hiyo ambayo ameiweka akiba. 15Hiyo ndiyo sababu ninaingiwa na hofu mbele zake; nifikiriapo haya yote ninamwogopa. 16Mungu ameufanya moyo wangu kuzimia; yeye Mwenyezi amenitia hofu. 17Hata hivyo sijanyamazishwa na giza, wala kwa giza nene linalofunika uso wangu.

Namba za mistari hufuata tafsiri uliyochagua, na katika sura chache zinaweza kutofautiana kwa mstari mmoja.

Urahisi wa kusoma

Chagua kinachokusaidia. Chaguo lako linahifadhiwa kwenye kifaa hiki.

Ukubwa wa maandishi

Unapendelea mipangilio ya kifaa chako mwenyewe (kukuza, kisoma skrini, hali ya giza)? Inafanya kazi hapa pia.