1Ndipo Elifazi Mtemani akajibu: 2“Je, mwanadamu aweza kuwa wa faida kwa Mungu? Je, hata mtu mwenye hekima aweza kumfaidi? 3Je, Mwenyezi angefurahia nini kama ungekuwa mwadilifu? Au je, yeye angepata faida gani kama njia zako zingekuwa kamilifu? 4“Je, ni kwa ajili ya utaua wako ndiyo maana anakukemea na kuleta mashtaka dhidi yako? 5Je, uovu wako si mkuu? Dhambi zako si hazina mwisho? 6Umedai dhamana kwa ndugu zako bila sababu; umewavua watu nguo zao, ukawaacha uchi. 7Hukumpa maji aliyechoka, nawe ulimnyima chakula mwenye njaa, 8ingawa ulikuwa mtu mwenye uwezo ukimiliki nchi: mtu uliyeheshimiwa, ukiishi ndani yake. 9Umewafukuza wajane mikono mitupu na kuzivunja nguvu za yatima. 10Ndiyo sababu mitego imekuzunguka pande zote, hatari ya ghafula inakutia hofu, 11ndiyo sababu ni giza sana huwezi kuona, tena ndiyo sababu mafuriko ya maji yamekufunika. 12“Je, Mungu hayuko katika mbingu za juu? Juu kuliko nyota zilizo juu sana! 13Hivyo wewe wasema, ‘Mungu anajua nini?’ Je, yeye huhukumu katika giza kama hilo? 14Mawingu mazito ni pazia lake, hivyo hatuoni sisi atembeapo juu ya anga la dunia. 15Je, utaifuata njia ya zamani, ambayo watu waovu waliikanyaga? 16Waliondolewa kabla ya wakati wao, misingi yao ikachukuliwa na mafuriko. 17Walimwambia Mungu, ‘Tuache sisi! Huyo Mwenyezi aweza kutufanyia nini?’ 18Lakini ndiye alizijaza nyumba zao na vitu vizuri, hivyo ninajitenga mbali na mashauri ya waovu. 19“Wenye haki wanaona maangamizi yao na kufurahi, nao wasio na hatia huwadhihaki, wakisema, 20‘Hakika adui zetu wameangamizwa, nao moto umeteketeza mali zao.’ 21“Mjue sana Mungu ili uwe na amani, ndipo mema yatakapokujia. 22Uyapokee mafundisho toka kinywani mwake, na maneno yake uyaweke moyoni mwako. 23Kama ukimrudia Mwenyezi, utarudishwa upya: Kama ukiuondoa uovu uwe mbali na hema lako, 24kama dhahabu yako ukiihesabu kama mavumbi, dhahabu yako ya Ofiri kama miamba ya mabondeni, 25ndipo Mwenyezi atakuwa dhahabu yako, naye atakuwa fedha yako iliyo bora. 26Hakika ndipo utakapojifurahisha kwa Mwenyezi, nawe utamwinulia Mungu uso wako. 27Utamwomba yeye, naye atakusikia, nawe utazitimiza nadhiri zako. 28Utakusudia jambo nalo litatendeka, nao mwanga utaangazia njia zako. 29Watu watakaposhushwa, nawe ukasema, ‘Wainue!’ ndipo atamwokoa aliyevunjika moyo. 30Atamwokoa hata yule ambaye ana hatia, ataokolewa kwa sababu ya usafi wa mikono yako.”
1Then Eliphaz the Temanite answered, 2“Can a man be profitable to God? Surely he who is wise is profitable to himself. 3Is it any pleasure to the Almighty, that you are righteous? Or does it benefit him, that you make your ways perfect? 4Is it for your piety that he reproves you, that he enters with you into judgment? 5Isn’t your wickedness great? Neither is there any end to your iniquities. 6For you have taken pledges from your brother for nothing, and stripped the naked of their clothing. 7You haven’t given water to the weary to drink, and you have withheld bread from the hungry. 8But as for the mighty man, he had the earth. The honorable man, he lived in it. 9You have sent widows away empty, and the arms of the fatherless have been broken. 10Therefore snares are around you. Sudden fear troubles you, 11or darkness, so that you can not see, and floods of waters cover you. 12“Isn’t God in the heights of heaven? See the height of the stars, how high they are! 13You say, ‘What does God know? Can he judge through the thick darkness? 14Thick clouds are a covering to him, so that he doesn’t see. He walks on the vault of the sky.’ 15Will you keep the old way, which wicked men have trodden, 16who were snatched away before their time, whose foundation was poured out as a stream, 17who said to God, ‘Depart from us;’ and, ‘What can the Almighty do for us?’ 18Yet he filled their houses with good things, but the counsel of the wicked is far from me. 19The righteous see it, and are glad. The innocent ridicule them, 20saying, ‘Surely those who rose up against us are cut off. The fire has consumed their remnant.’ 21“Acquaint yourself with him, now, and be at peace. Thereby good shall come to you. 22Please receive instruction from his mouth, and lay up his words in your heart. 23If you return to the Almighty, you shall be built up, if you put away unrighteousness far from your tents. 24Lay your treasure in the dust, the gold of Ophir among the stones of the brooks. 25The Almighty will be your treasure, and precious silver to you. 26For then you will delight yourself in the Almighty, and shall lift up your face to God. 27You shall make your prayer to him, and he will hear you. You shall pay your vows. 28You shall also decree a thing, and it shall be established to you. Light shall shine on your ways. 29When they cast down, you shall say, ‘be lifted up.’ He will save the humble person. 30He will even deliver him who is not innocent. Yes, he shall be delivered through the cleanness of your hands.”
1Toen antwoordde Elifaz, de Themaniet, en zeide: 2Zal ook een man Gode voordelig zijn? Maar voor zichzelven zal de verstandige voordelig zijn. 3Is het voor den Almachtige nuttigheid, dat gij rechtvaardig zijt; of gewin, dat gij uw wegen volmaakt? 4Is het om uw vreze, dat Hij u bestraft, dat Hij met u in het gericht komt? 5Is niet uw boosheid groot, en uwer ongerechtigheden geen einde? 6Want gij hebt uw broederen zonder oorzaak pand afgenomen, en de klederen der naakten hebt gij uitgetogen. 7Den moede hebt gij geen water te drinken gegeven, en van den hongerige hebt gij het brood onthouden. 8Maar was er een man van geweld, voor dien was het land, en een aanzienlijk persoon woonde daarin. 9De weduwen hebt gij ledig weggezonden, en de armen der wezen zijn verbrijzeld. 10Daarom zijn strikken rondom u, en vervaardheid heeft u haastelijk beroerd. 11Of gij ziet de duisternis niet, en des water overvloed bedekt u. 12Is niet God in de hoogte der hemelen? Zie toch het opperste der sterren aan, dat zij verheven zijn. 13Daarom zegt gij: Wat weet er God van? Zal Hij door de donkerheid oordelen? 14De wolken zijn Hem een verberging, dat Hij niet ziet; en Hij bewandelt den omgang der hemelen. 15Hebt gij het pad der eeuw waargenomen, dat de ongerechtige lieden betreden hebben? 16Die rimpelachtig gemaakt zijn, als het de tijd niet was; een vloed is over hun grond uitgestort; 17Die zeiden tot God: Wijk van ons! En wat had de Almachtige hun gedaan? 18Hij had immers hun huizen met goed gevuld; daarom is de raad der goddelozen verre van mij. 19De rechtvaardigen zagen het, en waren blijde, en de onschuldige bespotte hen; 20Dewijl onze stand niet verdelgd is, maar het vuur hun overblijfsel verteerd heeft. 21Gewen u toch aan Hem, en heb vrede; daardoor zal u het goede overkomen. 22Ontvang toch de wet uit Zijn mond, en leg Zijn redenen in uw hart. 23Zo gij u bekeert tot den Almachtige, gij zult gebouwd worden; doe het onrecht verre van uw tenten. 24Dan zult gij het goud op het stof leggen, en het goud van Ofir bij den rotssteen der beken; 25Ja, de Almachtige zal uw overvloedig goud zijn, en uw krachtig zilver zijn; 26Want dan zult gij u over den Almachtige verlustigen, en gij zult tot God uw aangezicht opheffen. 27Gij zult tot Hem ernstiglijk bidden, en Hij zal u verhoren; en gij zult uw geloften betalen. 28Als gij een zaak besluit, zo zal zij u bestendig zijn; en op uw wegen zal het licht schijnen. 29Als men iemand vernederen zal, en gij zeggen zult: Het zij verhoging; dan zal God den nederige van ogen behouden. 30Ja, Hij zal dien bevrijden, die niet onschuldig is, want hij wordt bevrijd door de zuiverheid uwer handen.
Bonyeza Enter ili kuuwekea mstari huu rangi, kuandika maelezo au kuunakili. Vitufe vya mishale vinakupeleka kwenye mstari unaofuata.
Namba za mistari hufuata tafsiri uliyochagua, na katika sura chache zinaweza kutofautiana kwa mstari mmoja.