1Kisha Ayubu akajibu: 2“Nimepata kusikia mambo mengi kama haya, nanyi nyote ni wafariji wenye kutaabisha! 3Je, maneno yenu mengi yasiyo na maana hayana mwisho? Mna nini hata mwendelee kushindana kwa maneno? 4Mimi pia ningeweza kuzungumza kama ninyi, kama mngekuwa katika hali yangu; ningeweza kutoa hotuba nzuri dhidi yenu, na kuwatikisia ninyi kichwa changu. 5Lakini kinywa changu kingewatia moyo; faraja kutoka midomoni mwangu, ingewaletea nafuu. 6“Lakini kama nikisema, maumivu yangu bado hayatulizwi; nami kama nikijizuia, wala hayaondoki. 7Ee Mungu, hakika umenichakaza; umewaangamiza kabisa watu wa nyumbani mwangu wote. 8Umenikunjakunja, nalo limekuwa ushahidi; nako kukonda kwangu kumeongezeka sana na kushuhudia dhidi yangu. 9Mungu amenishambulia na kunirarua katika hasira yake, na kunisagia meno yake; adui yangu hunikazia macho yake makali. 10Watu wamenifumbulia vinywa vyao kunidhihaki; hunipiga shavuni mwangu kwa dharau, na kuungana pamoja dhidi yangu. 11Mungu amenigeuzia kwa watu wabaya, na kunitupa katika makucha ya waovu. 12Mambo yote yalikuwa mazuri, lakini alinivunjavunja; amenikamata shingo na kuniponda. Amenifanya mimi kuwa shabaha yake; 13wapiga upinde wake wananizunguka. Bila huruma, huchoma figo zangu, na kuimwaga nyongo yangu juu ya nchi. 14Huniponda tena na tena; hunishambulia kama shujaa wa vita. 15“Nimejishonea nguo ya gunia juu ya mwili wangu nami nimekizika kipaji cha uso wangu kwenye vumbi. 16Uso wangu umekuwa mwekundu kwa kulia, macho yangu yamepigwa na giza kuu. 17Hata hivyo mikono yangu haijafanya jeuri, na maombi yangu ni safi. 18“Ee nchi, usiifunike damu yangu, nacho kilio changu kisinyamazishwe kamwe. 19Hata sasa shahidi wangu yuko mbinguni; wakili wangu yuko juu. 20Mwombezi wangu ni rafiki yangu macho yangu yamwagapo machozi kwa Mungu; 21kwa niaba ya mtu anamsihi Mungu kama mtu anavyosihi kwa ajili ya rafiki yake. 22“Ni miaka michache tu itapita kabla sijaenda safari ambayo sitarudi.
1Then Job answered, 2“I have heard many such things. You are all miserable comforters! 3Shall vain words have an end? Or what provokes you that you answer? 4I also could speak as you do. If your soul were in my soul’s place, I could join words together against you, and shake my head at you, 5but I would strengthen you with my mouth. The solace of my lips would relieve you. 6“Though I speak, my grief is not subsided. Though I forbear, what am I eased? 7But now, God, you have surely worn me out. You have made desolate all my company. 8You have shriveled me up. This is a witness against me. My leanness rises up against me. It testifies to my face. 9He has torn me in his wrath, and persecuted me. He has gnashed on me with his teeth. My adversary sharpens his eyes on me. 10They have gaped on me with their mouth. They have struck me on the cheek reproachfully. They gather themselves together against me. 11God delivers me to the ungodly, and casts me into the hands of the wicked. 12I was at ease, and he broke me apart. Yes, he has taken me by the neck, and dashed me to pieces. He has also set me up for his target. 13His archers surround me. He splits my kidneys apart, and does not spare. He pours out my gall on the ground. 14He breaks me with breach on breach. He runs on me like a giant. 15I have sewed sackcloth on my skin, and have thrust my horn in the dust. 16My face is red with weeping. Deep darkness is on my eyelids. 17Although there is no violence in my hands, and my prayer is pure. 18“Earth, don’t cover my blood. Let my cry have no place to rest. 19Even now, behold, my witness is in heaven. He who vouches for me is on high. 20My friends scoff at me. My eyes pour out tears to God, 21that he would maintain the right of a man with God, of a son of man with his neighbor! 22For when a few years have come, I shall go the way of no return.
1Maar Job antwoordde en zeide: 2Ik heb vele dergelijke dingen gehoord; gij allen zijt moeilijke vertroosters. 3Zal er een einde zijn aan de winderige woorden? Of wat stijft u, dat gij alzo antwoordt? 4Zou ik ook, als gijlieden, spreken, indien uw ziel ware in mijner ziele plaats? Zou ik woorden tegen u samenhopen, en zou ik over u met mijn hoofd schudden? 5Ik zou u versterken met mijn mond, en de beweging mijner lippen zou zich inhouden. 6Zo ik spreek, mijn smart wordt niet ingehouden; en houd ik op, wat gaat er van mij weg? 7Gewisselijk, Hij heeft mij nu vermoeid; Gij hebt mijn ganse vergadering verwoest. 8Dat Gij mij rimpelachtig gemaakt hebt, is tot een getuige; en mijn magerheid staat tegen mij op, zij getuigt in mijn aangezicht. 9Zijn toorn verscheurt, en Hij haat mij; Hij knerst over mij met Zijn tanden; mijn wederpartijder scherpt zijn ogen tegen mij. 10Zij gapen met hun mond tegen mij; zij slaan met smaadheid op mijn kinnebakken; zij vervullen zich te zamen aan mij. 11God heeft mij den verkeerde overgegeven, en heeft mij afgewend in de handen der goddelozen. 12Ik had rust, maar Hij heeft mij verbroken, en bij mijn nek gegrepen, en mij verpletterd; en Hij heeft mij Zich tot een doelwit opgericht. 13Zijn schutters hebben mij omringd; Hij heeft mijn nieren doorspleten, en niet gespaard; Hij heeft mijn gal op de aarde uitgegoten. 14Hij heeft mij gebroken met breuk op breuk; Hij is tegen mij aangelopen als een geweldige. 15Ik heb een zak over mijn huid genaaid; ik heb mijn hoorn in het stof gedaan. 16Mijn aangezicht is gans bemodderd van wenen, en over mijn oogleden is des doods schaduw. 17Daar toch geen wrevel in mijn handen is, en mijn gebed zuiver is. 18O, aarde! bedek mijn bloed niet; en voor mijn geroep zij geen plaats. 19Ook nu, zie, in den hemel is mijn Getuige, en mijn Getuige in de hoogten. 20Mijn vrienden zijn mijn bespotters; doch mijn oog druipt tot God. 21Och, mocht men rechten voor een man met God, gelijk een kind des mensen voor zijn vriend. 22Want weinige jaren in getal zullen er nog aankomen, en ik zal het pad henengaan, waardoor ik niet zal wederkeren.
Bonyeza Enter ili kuuwekea mstari huu rangi, kuandika maelezo au kuunakili. Vitufe vya mishale vinakupeleka kwenye mstari unaofuata.
Namba za mistari hufuata tafsiri uliyochagua, na katika sura chache zinaweza kutofautiana kwa mstari mmoja.